Advertise Here

Saturday, November 3, 2012

How to have a Great Marriage?

 
“My command is this: Love each other as I have loved you” – John 15:12. Love as Jesus loved! Be willing to lay down your life to bless your spouse. Few would ever want to get rid of a spouse who truly practices this principle.

The ingredients for having a great marriage are the same as having any great relationship: communication, honesty,
commitment, kindness, and attention. If your aim is to bless your spouse and make them happy, it is very likely they
will eventually respond by loving you.

If you are the only one in your marriage practicing this, it can be difficult. But your only other choice is to treat them badly in return. How can that produce anything good?

You are God’s representative. He put you where you are so He could express His love through you. God loves your spouse whether you think they deserve it or not. The Bible teaches us to put the interests of others first.
 
Romans 12:10 says; “Be devoted to one another in brotherly love. Honor one another above yourselves.” Which is a higher priority for you: your happiness or your spouse’s happiness? “But,” you say, “I’ve done all that and they are not reciprocating. They just take advantage of me.”

First, without your efforts your marriage could already be dead and gone. Second, you will be judged only for what you did in life not what your spouse did. Third, God’s law of giving will eventually work: As you continue to give love love will be returned to you. It WILL work, even if God has to take your current spouse to Heaven so He can give you one who will return your love.

Commit yourself to the happiness and well-being of your spouse. Keep acting on God’s Word and showing love to them. Put them before yourself. God will work on your behalf.

SAY THIS: With God’s help, I will have a great marriage.

Friday, November 2, 2012

Semina ya "Challenges After Campus Life" na Samuel Sasali.

Samuel Sasali akizungumza kwenye Semina
 ALL the way from Dar es salaam to Mwanza, ni Samuel Sasali a.k.a Papaa katika Semina maalum ya Wanachuo wa St. Augustine University of Tanzania iliyopewa jina la "Challenges After Campus Life".
Wanachuo wakifuatilia Semina kwa Makini
Semina ikiendelea
 Ikiwa leo ndo ilikuwa Siku ya Kwanza ya Semina ambayo ilifanyika katika Kanisa la T.A.G lililopo Nyamalango Malimbe, pembezoni kabisa mwa Chuo cha SAUT.
Imeeleweka????
Daniel Liberati(M/Kiti Tafes Saut-Kushoto), Remmy Paschal(Katibu Tafes Saut-Katikati), na Samwel Madaha(M/Kiti Tafes Mkoa wa Mwanza-Kulia)
Semina hii imeandaliwa na TAFES Saut kwa kushirikiana na Mtumishi Samuel Sasali, ikiwa na lengo la kuwaandaa wanachuo hawa kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali pindi wamalizapo masomo yao chuoni.
Watumishi wa Mungu wakifuatila Semina kwa Makini
Haachwi mtu hapo
 Semina hiyo itakayodumu kwa Siku 2, itamalizika Siku ya Kesho kwa kufanyika katika Ukumbi wa M1 uliopo ndani ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustino.
Sam Sasali akiendelea na Semina
Mtangazaji wa Alive Fm Adolph Nzwalla akijitambulisha kwa wanasemina
Sadaka ni sehemu ya Ibada, na ilipofika wakati wa kutoa Sadaka Maombi yakafanyika kwanza.
Sadaka Mkononi
Happy people
Sehemu ya wanasemina
 Semina ilimalizika mida kama ya Saa 2 Usiku hivi ili kumpa nafasi Mtumishi huyu kuandaa Materials a.k.a Nondo kwa ajili ya Semina ya Kesho.
Papaa baada ya kumaliza kutoa Ujumbe wa leo
M/Kiti Tafes Mkoa wa Mwanza Bw. Samwel Madaha akiwasalimu wanasemina
Kwa leo tumalize hiviiiiiiii..........
Blogger Sowane Emmanuel akiwa na Papaa baada ya Kumalizika kwa Semina
Kutoka Kushoto ni Yusuph Magupa, Sam Papaa, Ruth Lyanga na Adolph Nzwalla
 Tukutane Kesho Ukumbi wa M1 kwa Muendelezo wa Semina hii tukiwa na Mtumishi Samuel Sasali, ambaye pia ni Christian Blogger.

Be Blessed!

Padre aliyezama Baharini azikwa Kama Chifu wa Kihehe kwa kupigiwa Mizinga 20.

Ndugu wa Marehemu Padre Salutarius wakiwa kwenye Kaburi baada ya Mazishi
 PADRE Salutarius Massawe ambaye alikuwa Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Consolatha amezikwa kwa heshima za kichifu wa kabila la wahehe mkaoni Iringa kwa kupigiwa Mizinga 20 angani.

Katika mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Mapadre ya Jimbo la Iringa, yaliyoko Tosamaganga nje kidogo ya Mji wa Iringa, pamoja na maefu ya ndugu, jamaa, marafiki, watawa na wakuu wa Shirika la Consolatha kutoka nchi za afrika, marehemu alipewa heshima za kipekee na wananchi wa Iringa huku vilio na zimanzi vikitawala kila kona ya mji huo wakati maiti yake ikipitishwa kwa ajili ya kuaga.
Maandamano ya kuutoa Mwili wa Marehemu katika Kanisa Kuu la Jimbo la Iringa
Padre Massawe alifariki Mjini Bagamayo wakati akiogelea katika bahari ya Hindi na wakuu wenzake wa Shirika la Consolatha kutoka nchi mbalimbali waliokuwa na Mkutano katika Kituo cha Kiroho cha Consolatha kilichoko Bunju jijini Dar es Salaam, na baadaye kuhitimisha kwa mapumziko mafupi mjini Bagamoyo. Wakati wa Misa iliyoongozwa na askofu wa Jimbo la Iringa.

- The Habari -

Thursday, November 1, 2012

Usaili wa AFLEWO kwa Mwaka 2013, kufanyika Ijumaa na Jumamosi ya Wiki hii.

 
Kama Unataka kuwa Muhudumu kwenye Tamasha la AFLEWO 2013, Usaili wa Kuhudumu kama Muimbaji utafanyika Ijumaa hii pale DPC kuanzia saa 12 Jioni mpaka saa 2 usiku.

Kama unataka kuhudumu kwenye upande wa Maombi, Publicity na Marketing, Hospitality, au Usher Usajili utafanyika Jumamosi hii katika Kanisa la City Christian Centre kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 5 asubuhi.

Wednesday, October 31, 2012

Boko Haram waua waumini 7 wa Kanisa Katoliki Nchini Nigeria.

http://www.ibn-tv.com/wp-content/uploads/2012/10/Nigeria5.jpg
Mji wa Kaduna Nchini Nigeria
 TAKRIBAN watu saba wameuawa nchini Nigeria na wengine wengi wakijeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga katika kanisa la kikatoliki Kaskazini mwa Nigeria.

Maafisa wanasema kuwa gari lililokuwa limebeba mabomu liliingia katika kanisa hilo na kulipua mabomu huku athari zake zikitoboa shimo katika paa la kanisa hilo.

Shambulio hilo lilitokea mjini Kaduna, eneo ambalo limekuwa likilengwa sana na wapiganaji wa Boko Haram kwa mashambulizi katika siku za hivi karibuni.

Rais Goodluck Jonathan ameahidi kongeza juhudi za kupambana na ugaidi na vurugu nchini humo. Aidha Rais Goodluck alitaja shambulizi hilo kama kitu kisicho kubalika na ambacho kinatishia usalama na uthabiti wa nchi hiyo.

Mwandishi wa BBC mjini huko aliarifu kuwa shambulio hilo lilitokana na bomu lilotegwa kwenye gari lililopuliwa na mtu aliyejitoa mhanga na kugonga gari hilo kwenye ukuta wa kanisa.

Anasema uharibifu mkubwa ulitokea ndani ya jengo na kwamba mapaa ya maduka na nyumba za karibu yaling’oka.

Afisa mmoja wa kanisa hilo alisema watu kama wanne waliuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Kumetokea mashambulio kadha ya kidini katika jimbo hilo, mengi yamefanywa na kundi la wapiganaji wa kiislamu, Boko Haram.