Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Nchini Kenya, Bahati |
Ikiwa Tuzo Mpya za Muziki wa Injili Nchini kenya za Xtreem Awards zikitarajiwa kutolewa kabla ya Mwisho wa Mwaka huu kwa Waimbaji mbalimbali wa Nyimbo za Injili nchini Kenya, Mwimbaji Bahati kutoka Kenya amejitoa katika Tuzo hizo.
Bahati amefikia Uamuzi huo wa kutokushiriki katika kinyang'anyiro hicho pamoja na kuteuliwa katika Category 3 tofauti kwa madai kuwa anatoa fursa kwa Waimbaji wapya kushiriki Tuzo hizo ili vipawa vyao nao vionekane.
Bahati anasema, "Ninamshukuru Mungu kwa hapa nilipofika pamoja na timu yangu nzima. Kila siku nafanya kazi kwa bidii ili watu wajivunie na waamini kuwa bado kuna mazuri yanakuja. Nimeamua kujitoa kwenye Mashindano ya Tuzo za Xtreem Awards, sisi kama Familia ili kutoa nafasi ya kutosha kwa Waimbaji wapya kuonesha Vipawa vyao. Bado tupo pamoja na Asanteni sana kwa Upendo wenu na Msaada wenu. Nawapenda sana".
Bahati ameteuliwa kushiriki katika Category ya "Teeniz Choice Artist/Group", "Teeniz Favourite Song" (Kupitia Wimbo wake wa "Mama") na "Video of the Year" kupitia Wimbo wake wa "Wangu" aliomshirikisha Mr. Seed.
Tuzo za Xtreem Awards ni Tuzo Mpya za Muziki wa Injili Nchini Kenya zenye lengo la Kutambua na Kutangaza vipawa vipya vya Waimbaji wa Nyimbo za Injili Nchini Kenya, na Zilizinduliwa rasmi Ijumaa ya Octoba 11, 2013 CRC na Mchakato wa kuwapata Washiriki ulifanyika Ijumaa iliyopita.