Mch. Antony Lusekelo |
MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi (GRC), Ubungo-Kibangu, Anthony
Lusekelo ‘Mzee wa Upako’, amelazimika kufanya maombezi kwa ajili ya
kulinda wanyama kutokana na kukithiri kwa ujangili wa kuuawa kwa
tembo.
Akizungumza katika ibada mojawapo ya Jumapili, Mchungaji Lusekelo alikemea vitendo hivyo kushamiri miongoni mwa jamii.
Alisema ni muhimu wanyama wakalindwa kwa kuwa ni rasilimali inayokuza uchumi wa nchi na kutaka waumini wake kufanya maombi mafupi ya kuombea suala hilo.
“Hatuwezi kukubali kuona wanyama kama tembo wanatokomea ni lazima tuliombee jambo hili, la sivyo hata vizazi vyetu vitashindwa kujua aina ya wanyama kwa sababu ya watu wachache kuwa na uroho wa fedha,” alisema.
Mchungaji huyo alisimama kwa muda akiombea suala hilo pamoja na waumini wake na kumuomba Mungu afanye ulinzi juu ya rasilimali hiyo.
Lusekelo alisema suala la ujangili lisipodhibitiwa kuna uwezekano wa wanyama kwisha na hata kuwa historia ya taifa kuwa na wanyama kama tembo.
“Hili suala si dogo kama tunavyofikiri, ni muhimu kuomba ulinzi wa Kimungu ili yeye aliyetubariki juu ya suala hilo aendelee kuwapa ulinzi wanyama hao,” alisema.

- Betty Kangonga -