Kidumu |
Mwanamuziki Kidumu mwenye asili ya Burundi aishiye Kenya ameelezea
sababu zinazomfanya kuimba Muziki mchanganyiko yaani Muziki wa injili
pamoja na Muziki wa Kidunia.
Kidumu amesema kuwa yeye si Mchungaji wala si Mwalimu wa Dini, ila yeye ni Msanii anayeishi kwa kufuata wito wa Mungu.
"Gospel
ilivyo si kama watu wengi wanavyoifikiria. Msanii ni kioo cha Jamii, na
kila ninalolifanya linafundisha jamii katika mambo yanayowaathiri sana.
Daddy Owen alipoimba wimbo wa "Mbona" alikuwa akizungumzia namna watu
wenye ulemavu wanavyonyanyapaliwa. Jamii inapaswa kuelimishwa kuhusu
Magonjwa, Upendo, Amani, Ukabila, Siasa pamoja na mambo mengine
yanayowagusa. Hicho ndicho ninachokifanya." Amesema Kidumu.
Anasema Wokovu si kuimba tu kuhusiana na Habari za kwenda Mbinguni, au kujaza Jina Yesu kwenye Mistari ya wimbo, bali pia ni Kutoa taarifa zenye manufaa kwa jamii.