Waziri
wa habari nchini Nigeria Bwana Labaran Maku, amelishauri Kanisa
Katoliki Nchini Nigeria kuanza mchakato wa matumizi ya njia za
mawasiliano ya Jamii katika azma ya Uinjilishaji wa kina unaogusa
mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili. Mchakato huu uliwezeshe Kanisa
pia kuziinjilisha njia za mawasiliano ya kijamii kwani kwa kiasi
kikubwa zimekuwa ni sababu ya kumong'onyoka kwa misingi ya maadili na
utu wema.
Ili kutekeleza wajibu na dhamana hii nyeti, kuna haja kwa Kanisa nchini Nigeria kuwekeza katika majiundo makini kwa Mapadre na Watawa watakaoweza kutumia mitandao hii kwa umakini mkubwa kama sehemu ya Uinjilishaji, kwani kwa sasa kuna idadi kubwa ya vijana wanaoperuzi kwenye mitandao na wakati mwingine wanaambulia mitandao inayowayumbisha katika maisha yao kijamii na kimaadili.
Kanisa lijitahidi kuwa na mitandao hii katika taasisi zake za elimu na huduma jamii na wala zisiwe kwa ajili ya viongozi wachache tu wa Kanisa. Kwa kuwekeza katika mitandao ya kijamii, idadi kubwa ya watu wanaweza kupata fursa ya kusikia Habari Njema ya Wokovu ikitangazwa kwao! Hii ni kutokana na huruma na upendo wa Mungu kwa watu wake kwamba, leo hii watu wanaweza kuwasiliana kwa haraka na kwa upesi zaidi ikilinganishwa na miaka kadhaa iliyopita.
Mitandao ya kijamii anasema Bwana Labaran Maku inaweza kutumika kusoma Biblia, kuhubiri na kufundisha mambo msingi ya maisha. Ikiwa kama itatumika vyema, ulimwengu unaweza kuwa ni mahali pazuri zaidi pa kuishi. Bwana Maku ameyasema hayo hivi karibuni wakati alipokuwa anatoa mhadhara kwenye Seminari ya Kumbu kumbu ya Bigard iliyoko mjini Enugu, Nigeria.

- Radio Vaticana -