Katibu Mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Mchungaji Yakobo Mapambano akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake |
Hatimaye Uongozi wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga umetangaza Jumla ya
fedha zilizopatikana katika harambee iliyoendeshwa na Mbunge wa Jimbo la
Sengerema William Ngeleja kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari ya Bishop
Nkola inayomilikiwa na kanisa hilo.
Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga, Mchungaji Yakobo Mapambano amewaambia waandishi wa habari kuwa lengo
lilikuwa ni kupata Milioni 350, na Jumla ya pesa katika changizo
zilizopatikana mpaka sasa ni Shilingi Milioni 263, Laki 2, Elfu 4 na Mia
tisa.
Katika harambee hiyo kanisa lilipokea Michango kutoka kwa Prince Mobutu(Mtoto wa Rais wa zamani wa Zaire,
Mobutu Seseseko), Askofu Mkuu wa AICT Nchini Kenya, Silas Yego, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nasoro Rufunga, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Annarose Nyamubi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja, Mbunge
wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele, Mbunge wa viti maalum Rachel
Mashishanga na watu mbalimbali wenye mapenzi mema juu ya Jambo hili.
- Kadama Malunde (Shinyanga) -