Kabula George |
Nimezaliwa
miaka 30 iliyopita katika kijiji cha Kimiza Wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza.
Masomo ya elimu shule ya msingi nilipata Kimiza mkoani Mwanza na baada ya
haapo niliendelea na masomo ya sekondari jijini Dar es Salaam.
Huduma
ya uimbaji nilianza nikiwa mdogo nikiwa kanisa la Romani kabla ya kujiunga na
kwaya ya Uinjilisti ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Usharika wa Tabata Kinyerezi.
Mwaka
2005 ndipo nilianza rasmi uimbaji kama solo artis na kufanikiwa kurekodi albamu
yangu ya kwanza iliyojulikanaa kwa jina la AMANI. Hata hivyo albamu hiyo niliifanyia
marekebisha na kuamua kuirudia nikachukua nyimbo kama Nkomoji ulioimbwa kwa
lugha ya Kisukuma wenye maana ya kombozi. Milele, Tanzania na T unakulilia.
Niliongezea
nyimbo nyingine na kuipa jina jipya la Pesa iki ikiwa na nyimbo 9 kama, Milele, Pesa, Ninamjua, Nkomoji, Tanzania, Tunakulilia, Yatima, Nakupa utuku na
Niguse.
Niguse.
Mwaka
2009 nilifanikiwa kutoka na albamu yangu ya pili iliyojulikana kwa jina la
‘Ushindi’ ikiwa na nyimbo nane ambazo ni Ushindi, Hakuna muweza, Tunaishi kwa
Neema, Yerusalemu, Nikikumbuka, Dhihirisha, Yesu Wasitahili na Mshukuruni
Bwana.
Mwaka
2011 nilifanikiwa kurekodi albamu yangu ya tatu inayokwenda kwa jina la
Nitang’ara Tu, ikiwa na nyimbo sita ambazo ni Nitang’ara tu, Majaribu,
Nimesogea, Nataka kumuona Yesu, Ni Mwema na Peleleza ikiwa katika mfumo wa DVD
na iko sokoni.
Mbali
na uimbaji pia namtumikia Mungu katika huduma ya kuhubiri na nimekuwa
nikisafiri katika nchi mbalimbali kwa ajili ya kuimba na kuhubiri. Nina abudu
katika Huduma ya Neno la Upatanisho (WRM) iliyochini ya Nabii Nicolaus Suguye.
Albamu
ya Nitang’ara tu nimeamua kuiboresha tena kwani nataka kurekodi video mpya na
nitaongeza baadhi ya nyimbo.
Katika albamu hii nitachukua nyimbo kama Nitang’ara
tu, Majaribu, Nimesogea na Nataka kumuona Yesu, kisha nitachukua wimbo wa Pesa
kutoka albamu ya kwanza na tatu kutoka albamu ya pili iitwayo Ushindi. Nyimbo hizo
ni Tunaishi kwa Neema, Yerusalemu na Dhihirisha.
Sikiliza Wimbo wake huu ujulikanao Kama "Pesa"
Wasiliana na Kabula George kwa Namba zifuatazo:
+255 658 140 336
+255 757 140 336
Facebook: Kabula George