Grace Ashy |
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Nchini Ghana Grace Ashy, amelilaumu Shirikisho la Soka la Nchini humo(GFA) pamoja na Timu ya Taifa ya Ghana "The Black Stars" kwa kutokumshukuru kwa namna yoyote Mwimbaji huyo na hata kutambua Mchango wake katika Mafanikio ya Timu hiyo ya Taifa ya Ghana.
Mwimbaji huyo Grace Ashy amekuwa akirekodi Nyimbo mbalimbali kuisifia timu hiyo ya Taifa na kuhamasisha watu kuiunga mkono timu hiyo lakini amesema kwasasa hatarekodi wimbo wowote kwakuwa Shirikisho hilo pamoja na Timu hiyo wameshindwa Kumshukuru kwa mchango wake huo wa kutunga Nyimbo hizo mara kwa mara.
Grace anasema, "Sina mpango wowote wa kufanya wimbo mpya kwa ajili ya "The Black Stars" ya Ghana. Nimefanya kwa sehemu yangu, na nimefanya yote hayo kwa pesa yangu mimi mwenyewe. Hakuna mtu yeyote ananidhamini. Toka mwaka 2006 mpaka leo, Nyimbo zote nilizorekodi kwa ajili ya Timu ya "The Black Stars" ni kutoka kwenye hazina yangu, na nimewatangaza kwa pesa yangu mwenyewe".
"Lakini si uongozi wa GFA wala wa timu ya "The Black Stars" uliowahi kuniita na kunishukuru au kujali kile nilichofanya. sijapata chochote kutoka kwenye nyimbo hizo. Nilifanya kwa ajili ya "The Black Stars" na sijutii kufanya hilo kwasababu nilifanya kwa ajili ya Mungu na Nchi yangu. Kwa hiyo nawatia Moyo watu mbalimbali kufanya hivyo kwa ajili ya Nchi yetu".