Meya Rob Ford |
Meya wa mji wa Toronto nchini Canada, Rob Ford, ameasi ulevi baada ya
‘kuokoka’. Jambo hili limetokea baada ya Makansela wa baraza la jiji
kumpunguzia madaraka yake.
Bwana Rob Ford mwenye umri wa miaka 22 anasema ameamua kuasi pombe,
baada ya kuokoka na kumtambua Yesu huku akisema kuwa kamwe hatawahi
kuonja tone la pombe.
Kabla ya kumtambua Yesu, Bwana Rob aliahidi kuwapiga vita Makansela waliopiga kura kumpunguzia mamlaka.
Waziri mkuu wa Canada, Stephen Harper alisema kuwa madai dhidi ya Bwana Ford ni ya kusikitisha sana.
Meya huyo alikabiliwa na shinikizo kujiuzulu
baada ya kukiri kuwa aliwahi kutumia dawa ya kulevya aina ya Cocaine
wakati alipokuwa mlevi chakari.
Pia anakabiliwa na madai ya kumtongoza
mfanyakazi wake mmoja wa kike pamoja na kutumia lugha chafu, kuwatisha
wafanyakazi wake na kuwa na uhusiano wa kimapanzi na kahaba.
Kwenye mahojiano na moja ya vyombo vya habari
nchini humo, Ford alisema hajaonja mvinyo kwa wiki tatu na kuwa hatawahi
kamwe kunywa pombe.
"Nimeweza kumtambua Yesu kama mwokozi wangu.,’’ alisema Ford.
- BBC Swahili -