Kiwewe na Matumaini katika Pozi |
MSANII wa Kundi la Ze Komedi, Robert Augustino ‘Kiwewe’ na mwenzake
Tumaini Martin ‘Matumaini’ wameamua kuacha anasa na kumrudia Mungu kwa
kuokoka.
Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema
kilichosababisha kuchukua uamuzi huo kwa wakati mmoja ni kutokana na
manzingira waliyolelewa tangu wakiwa wadogo, yaani kumjua Mungu.
“Niliamua kufanya uamuzi sahihi ambao naamini utanibadilishia maisha
yangu kwa kiasi kikubwa, kwa kufuata mambo yanayompendeza Mungu na siyo
starehe za ujana,” alisema Kiwewe huku akiungwa mkono na Matumaini na wakabainisha kuwa kwasasa wanasali kwa Mchungaji Josephat Gwajima.
Wasanii hao walisema, ili kuhakikisha wanaungana na Mungu katika kila jambo, wameamua kuanzisha kundi lao la muziki wa Injili, lijulikanalo kama Comedians Gospel linaloundwa na wao pamoja na Mkono.
CHANZO: Grobal Publishers