Reinhard Bonnke |
BAJETI
iliyowasilishwa na Kamati ya Maandalizi ili kufanikisha mkutano wa Injili wa
mhubiri wa kimataifa, Mwinjilisti
Reinhard Bonnke unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania
Agosti 21 hadi 25, mwaka huu ni dola 199,314.38 sawa na Shilingi za kitanzania
318,903,000
Kamati
hiyo inaongozwa na Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG, Magnus Mhiche
(mwenyekiti), Mchungaji Kiongozi wa huduma ya The Oasis Healing Ministry,
Prosper Ntepa (makamu mwenyekiti), Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste
Tanzania-Pentecoste Council of Tanzania (PCT), Askofu David Mwasota (katibu),
na Askofu Bathlomew Sheggah, ambaye ni mhamasishaji.
Wataalamu wa kufunga jukwaa ambalo litatumika katika mkutano wa Bonnke |
Hadi
Jumatano Agosti 14, kamati hiyo ilikuwa imepokea dola 60,000 sawa na Shilingi
za kitanzania karibu milioni 100. Kwa mujibu wa bajeti hiyo, waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali ambao watahudhuria mkutano (press conference)
kabla ya Bonnke kuanza kuhubiri, watatia kibindoni shilingi laki moja kila
mmoja. Bajeti kwa ajili ya tukio hilo tu imepangwa kuwa dola za Marekani
1,212.50 sawa na shilingi za kitanzania 1,940,000.00
Katika bajeti hiyo imeelezwa kuwa viongozi watano wa kamati hiyo kila mmoja atapata malipo ya shilingi za kitanzania 200,000 kwa ajili ya mawasiliano na shilingi 350, 000 kwa ajili ya mafuta ya gari kwa siku moja. Bajeti hiyo inaonesha kutenga shilingi za kitanzania 2,100,000 kwa ajili ya wamama watakaokesha kuombea mkutano huo. Bajeti kamili imewatengea Wamama Shilingi za kitanzania 11,180,000.
Gari lililobeba vifaa vya kujenga jukwaa likiwa tayari uwanjani |
Bajeti kamili imekaa kama ifuatavyo:
Hospitality Tsh 765, 0000 USD 478.13
Protocol Tsh 9,665,000 USD 6,040.63
Counselling
& Follow-up Tsh 10,779,000 USD
6,736.88
Transport Tsh 32,300,000 USD 20,187.50
Security
Tsh 9,902,000 USD 6,188.75
Intercessory Tsh 7,800,000
USD 4,875.00
Ushers Tsh 4,600,000 USD 2,875.00
Music
and Praise Tsh 8,400,000 USD 5,250.00
Admin
& Central Committee Tsh
50,940,000.00 USD 31,837.50
Women
Tsh 11, 180, 000 USD 6,987.50
Publicity Tsh 83,100,000 USD
51,937.50
Interpretation Tsh 3,000,000 USD 1,875.00
Technical Tsh 4,000,000 USD 2,500.00
Fire
Conference Tsh 6,000,00 USD 3,750.00
Youth Tsh 5,000,000 USD
3,125.00
Bajeti hiyo haigusi gharama za malazi ya Bonnke na watumishi atakaoambatana nao akiwemo Mchungaji Daniel Kolenda. Zinahusisha malipo katika ukumbi wa watu maalum katika uwanja wa ndege (VIP Lounge) kwa siku mbili watu 11 ambapo zimeombwa shilingi za kitanzania 2,200,000.