Habari wapendwa, tupeane maarifa katika changamoto hii, ili tuwe na maelezo sahihi
tuwapo kazini katika shamba la Bwana.
Najiuliza
ivi je ni waandishi tofauti au ni yule katika Luka and Matendo? Na vipi sasa
uwasilishaji tofauti wa matukio yale yale-angalia pia Marco
and Mathayo?Ni vema sana kukifahamu kitabu chetu (Biblia) ambacho ni bora
kabisa kuliko vitabu vilivyowahi kuwako na kama vitakuwako vingine. Wakati
mwingine Watu wa Mungu tunapokutana na changamoto ktk Kitabu chetu tukisomapo
au hasa tukiuulizwa/kubanwa na wana dini,tunawahi kukemea pepo la upinzani na
kufoka ili mtu huyo anyamaze milele au tunakua na hofu kua ni kukaribia
kufanya makufuru kuchunguza/kufuatilia kila jambo ktk Neno!-mambo ambayo
KiBiblia hayana msingi hata chembe, ni ya kibinadamu tu.
Kama/kwakua hiki ni
Kitabu chetu cha ukweli na tunaamini kwa nguvu nyingi kua humo kuna maneno ya
ukweli, kuliko kukimbia wajibu wa kulielewa Neno/Maandiko kwa kukemea pepo la
kutoelewa ktkt ya watu( ana dini, majirani,wanafunzi tunaowafundisha, hadhira
tunayohihubiri), ni faida na busara kufanya kila jitihada kukielewa Kitabu
hiki kitamu mfano kukisoma na kukitakafari sana kila mara ili kupata kweli
nyingine nyingi zilizomo kuweza ongelea mada/jambo/changamoto kadhaa, kusoma
vyanzo vingine vya maarifa, kuuliza Viongozi wetu wa Kiroho au Mkristo
mwenzio, kuomba/kumuuliza Roho Mtakatifu afunue/anunurishe ndani yetu
pia hata kuuliza watu wengine wa dini waliosomea tu
Imani/Biblia kidarasani na njia nyingine bora na sahihi za kupata maarifa na
ufahamu wa jambo.
Tukiulizwa haya yafuatayo ya kitabu chetu tukiaminicho sana,
tunafanyaje? Tukemee pepo au tujibu kwa ujasiri na hakika kabisa? Tujadiliane
kwa haya chini.
Mdo.1:1=Mwandishi
Dr. Luka anatoa dokezo kwa Mpendwa Theofilo kuhusu kile
kitabu cha ‘’kwanza’’ alichoandika kuhusu aliyoyafanya na kufundisha
Yesu. Ni kitabu gani icho alichoandika kuhusu aliyoanza kufanya na kufundisha
Yesu? soma hii ina connect..Luka.1:1-4 Anasema Luka kua ‘’nimeona vema
kukuandikia mpendwa Theofilo upate kujua hakika ya mambo
uliyofundishwa.....’’. Kwaiyo inaonekana kwamba aliyeandika kitabu cha Luka(
see 1: 3) ndiye aliyeandika Matendo(check mstari 1:1) ambaye ni Mr. Luka
aliyekua tabibu( bila shaka utagundua pia aina ya uandishi na namna
alivyo-present coverage ya maisha ya Yesu ukilinganisha na injili nyingine
kama ya Marko na Mathayo. Mfano- Luka ananza kwa kusema- nimependa ktk
Kiingereza.. ‘‘Having perfect understanding of all things from the very first
to write you an ORDERLY account'', tafsiri nyingine zinasema..''I,
myself have carefully investigated everything from the beginning''.. ),
Kwa iyo huyu daktari baada ya kufanya ''careful investigation ndipo akaandika
in an orderly manner.. Sasa kwakua ukweli ndio huo, kumetokea nini hapa?
Tunawekaje uwiano hapa?
Mdo.9:4-7
hasa mstari 7…waliokua pamoja na Paul ktk msafara pia ‘’WALIISIKIA
ile sauti’’, si Paul tu lakini ktk
Mdo.22:1-10 hasa mstari 9..Paul anaposhuhudia/anajitetea mbele
ya kundi la waliompiga vibaya kidogo wamuue,anasema….waliokua naye ktk msafara
‘HAWAKUSIKIA ile sauti’.Hapa Mwandishi ni mmoja, ndani ya kitabu kimoja na
tukio lilelile moja.
Pia
Mathayo.27:24-28 hasa mstari 28 ..Wakamvua Yesu nguo na kumvika
vazi JEKUNDU (scarlet robe) lakini Marco.15:15-17 hasa mstari
17..Wakamvika vazi la rangi ya ZAMBARAU (purple).Hapa waandishi ni wawili
tofauti ila tukio lilelile.
Kama
mtu wa Mungu tena mwana wa Mungu ambaye Biblia kwako ni Kitabu chenye maneno ya Baba, Bwana na Roho wetu,
unasemaje juu ya hili?
Swali limeulizwa Na: Edwin Seleli