KAMA maandiko
yanavyosema Mwenye Nacho Huongezewa na Ombeni Mtapewa Basi Maandiko
Hayo Yamejidhilisha Pale Wakati wa Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la
Lutherani Katika Kitongoji cha Makungu Kijiji cha Igwachanya Wilayani
Wanging'ombe Mkoani Njombe Ambapo Idadi ya watu na Kiasi Cha Fedha
Kilichopo patikana Huwezi Kuamini Kwa Macho yako Kama Sio Tomaso.
Zaidi ya Shilingi Milioni Mbili Pamoja na Ahadi zimeweza Kupatikana Jana Katika Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la KKKT Mtaa wa Nazareth Usharika wa Usuka Wilayani Wanging'ombe,Kiserikali ni Kitongoji cha Makungu Kijiji cha Igwachanya Kata ya Igwachanya Kufuatia Udogo wa Kanisa Lililopo na Kupelekea Waumini Hao Kutumia Hema Katika Kuendeshea Ibada zao siku Zote za Bwana Kwa Kipindi cha Miaka Mitatu Sasa.
Aidha Wananchi na Waumini wa Kitongoji Hicho Wameeleza Kutumia Hema Hilo wakati wa Jua na Mvua Katika Ibada zao Hali Iliyopelekea Kuchukua Uamuzi wa Kuanza Kujenga Kanisa Ambalo lipo katika Hatua za Awali za Msingi na Kisha Kuamua Kuitisha Harambee ya Kuchangia Ujenzi Huo.

Waumini wakichangia vifaa mbalimbali kama Mabati |
Risala ya
Ujenzi wa Kanisa Hilo Iliyosomwa na Mwanjilisti wa Igwachanya Bi.Lonika
Yelemia Yombwi Imebainisha Malengo ya Dhati Katika Kujenga Kanisa Hilo
Litakalo Gharimu zaidi ya Shilingi Milioni Kumi Hadi Kukamilika kwake na
Kwamba Waumini wa Mtaa Huo Tayari wameshaanza Kwa Kuandaa Tofali Elfu
Kumi,Mawe Pamoja na Kukamilisha Ujenzi wa Msingi.
Hali ya Kanisa kwa sasa |
Kufuatia
Taarifa Hiyo iliyoibua Hisia za Waumini na Wageni Mbalimbali
walioshiriki Harambee Hiyo Ilimfanya Mgeni Rasmi Bwana Belshaza Muhanga
Ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Igwachanya Kutoa Neno Lililomgusa
Kila Mmoja Hadi Kupelekea Kufanikisha Zaidi ya Shilingi Milioni Mbili.
Miongoni Mwa Maneno yaliyosemwa na Bwana Belshaza Kutoka Kwenye Maandiko Matakatifu ni Pamoja na Kwamba Kushindwa Kutoa Sadaka Kubwa Wakati Unayo ni Kumuibia Mwenye Mungu Kwani Kila Kitu ni Mali yake,Maneno Ambayo yalitabiri Ukweli Katika shughuli Hiyo Muhimu na Kufanikisha Kiasi Hicho.

Mara Baada ya Kuzungumza na Kuchangia Mchango wake Huo
Pamoja na Ahadi ya Shilingi Laki Mbili Kutoka Kwa Mbunge wa Jimbo la
Njombe Magharibi Mhandisi Gerson Lwenge Ndipo Bwana Belshaza Akasimama
na Kutangaza Mafaniko ya Harambee Hiyo.
Kwa Upande wake Mchungaji wa Usharika wa Usuka Ambaye Alishiriki Ibada Hiyo Bwana Gideon Mtagawa Amepongeza Jitihada Kubwa na Mafanikio yaliyopatikana Kupitia Mgeni Rasmi Aliyeweza Kuhamasisha Harambee Hiyo.
Ombeni Nanyi Mtapewa,Njooni Kwangu Msumbukao na Mnaolemewa Na Mizigo nami Nitawapumzisha.

Na: Gabriel Kilamlya (Njombe)