Na: Mchungaji Mwangasa
Shetani
yupo na anafanya kazi lakini watu wengine hawaamini kama shetani yupo. Mtu
anaweza kuingiwa au kutupiwa mashetani asiweze kula wala kunywa. Pia mashetani
yanaweza kumfanya mtu akonde na kuwa mwembamba.
Marko 9:18 “na kila ampagaapo,
humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na
wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze”.
Pepo
anaweza kumwekea mtu kifafa,kutaliwa na laana. Marko 9:20 “Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye
akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu”.
Dalili
za mtu aliyechukuliwa Msukule
1. Anaanza
kuwatokea jamaa zake baada ya kufariki.Kuwa anaonekana mtu aliyekufa ni dalili
ya watu wa familia kuwa na mashetani.
2. Baada ya kufariki
anatokea mtu ndani ya familia anang’ang’ania
au kulazimisha mazishi yafanyike siku hiyo hiyo.
3. Baada ya
mazishi, siku ya pili au ya tatu kaburi la marehemu huyo linaanza kutitia, hii ni
kwa sababu mtu aliyechukuliwa msukule anakuwa bado ndani ya mwili.
4. Marehemu
anaonekana ama mrefu au mfupi sana zaidi ya kipimo cha mwanzo kipindi cha uhai
wake. Hapa yawezekana wamepima gogo refu au fupi Ukiona vile Anza kuomba na
kuita “Njoo kwa Jina la Yesu”
5. Kifo cha
ghafla. Binadamu ni kama gari jipya hivyo haiwezekani likawa jipya halafu
likaharibika bila sababu,hivyo ni lazima augue. Hospitali wanaweza kusema
amepata mshtuko wa moyo.Na roho ya kifo huwa inatumwa kwa muda inakaa ndani
mwako wala siyo siku moja hivyo jifunze kufuta tarehe ya ya kifo kilichopangwa
kwa Jina la Yesu.
6. Mgogoro kwenye
familia baada ya msiba. Watu wengine wana macho ya rohoni,moyo unachoongea jua
kipo.
7. Maneno ya marehemu
wakati anakata roho. Mfano “hao wanakuja, hao wananichukua”. Haya maneno yana maana
sana,maneno haya yazingatie hivyo ita mtu huyo aliyechukuliwa.
8. Maiti inabadilika
sura. Wachawi wanaweza kumchukua mtu na kukuachia kitu. Mara baada ya kugundua
kachukuliwa anza kuomba kwa Yesu na tumia maandiko.
9. Watu wanalazimisha
kulia. Watu hao waweza kuwa ndugu au watu wengine kama vile majirani. Mfano mfiwa
aweza kuambiwa “wewe umefiwa na mama halafu hulii?”. Nia yao ni wewe(mfiwa)
ukiri kuwa ndugu yako kafariki. Ukiona hivyo kataa kukiri haraka kuwa mtu waka
amekufa. Mfano Yesu alisema Lazaro hajafa bali amelala. Lengo la kulazimisha watu
kulia ni kurahisisha mtu kuchukuliwa, mana wasipolia hawawezi kumchukua na
kwenda naye.
10. Wanajitokeza watu
wanazuia wachungaji(walokole) wasimwombee.Wanaweza kusema hiyo “siyo imani
yetu” au “kaombee huko lakini siyo hapa”.
11. Wanandugu
wanakataa watu wasiombe wakisema hata akirudi sisi kwetu ni uchuro.
12. Ndugu wa marehemu
wanawaita na kuwapa dawa ili marehemu asije kukutokea tena.
Kwa hiyo ni muhimu inapotokea kuna kifo au tukio limetokea na kuna dalili zilizotajwa, ni vema kuliita Jina la Yesu.
- Ufufuo na Uzima -