Mtoto aliyefufuka (katikati) |
Ni jumapili tulivu katika viwanja vya kanisa jipya la Ufufuo na Uzima jijini Arusha; ambapo Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Tanzania, Mch. Josephat Gwajima
ameendelea na ziara yake mkoani humo kwa kuwafundisha viongozi wapya wa
masomo ya kumtumikia Mungu maarufu kama Potential shepherd.
Mwisho wa
Ibada ya Asubuhi ambayo ilitawaliwa na mafundisho zaidi ilifungua pazia
kwa ibada ya jioni ambayo ilikuwa ni fursa kwa wale ambao hawakuweza
kuwepo asubuhi nao kushiriki.
Majira ya saa kumi kamili, sifa zilivuma na baadaye kufuatiwa na ukaribisho wa Mch. Gwajima kutoa neno la Uzima. majira ya saa kumi na mbili kasoro; akaingia mama mmoja katikati ya ibada akiwa amembeba mwanaye ambaye kwa muonekano wa awali alikuwa amelegea mwili wote yaani amekufa.
Mch. Gwajima akifundisha Kanisani hapo |
Mama huyo ambaye alikuwepo katika mafundisho ya asubuhi na kujiunga na
mafundisho hayo ya potential shepherd; aliendelea kusema kuwa baada ya
kuona mwanaye hapumui wala mapigo ya moyo hayasikiki hakuona msaada wa
haraka zaidi ya kumkimbiza kanisani hapo Ufufuo na Uzima.
Aliingia kanisani wakati Mch. Josephat Gwajima akiwa anahubiri hivyo
kupokelewa na Mchungaji Msaidizi aitwaye Yeconia Bihagaze ambaye
alimuombea mtoto huyo palepale na muda mfupi uliofuata mtoto alifufuka
kutoka kwa wafu. Mungu ameendelea kudhihirisha neno la Mchungaji
Josephat Gwajima ndani ya jiji la Arusha hali inayosababisha maelfu ya
watu kuingia na kutoka katika viwanja hivyo kwaajili ya maombezi.
- Gospel Kitaa & Ufufuo Blog -