Vatican imemfuta kazi Askofu mmoja mbadhirifu wa Ujerumani. Makao makuu
ya Kanisa Katoliki duniani yamesema kuwa Vatican imechukua hatua hiyo
kutokana na kiongozi huyo wa kanisa kufanya ubadhirifu.
Askofu
Franz-Peter Tebartz-van Elst amefutwa kazi kwa kufanya ubadhirifu wa
mamilioni ya fedha za Kanisa. Kabla ya hapo, askofu huyo alikuwa
analalamikiwa sana kwa kufanya ubadhirifu na watu walikuwa wanataka
afukuzwe kwenye Kanisa Katoliki.
Katika taarifa yake, Vatican imesema
kuwa, Kanisa Katoliki limemfukuza kwa muda Askofu Franz-Peter
Tebartz-van Elst wa Limburg, Ujerumani. Taarifa zinasema kuwa, askofu
huyo ametumia karibu Euro Milioni mbili na laki tisa kwa ajili ya
kujenga makazi yake, fedha ambazo zilitoka kwenye mfuko wa kodi za
masuala ya kidini wa Ujerumani.
Askofu huyo mwenye umri wa miaka 53
analaumiwa pia kwa kutumia Euro Milioni 31 kujengea eneo la Kanisa
katika mji wa kale wa Limburg wakati gharama ya ujenzi wa eneo hilo
ulikuwa ni Euro Milioni 5.5.
- Iran Swahili Radio -