Advertise Here

Wednesday, October 16, 2013

Rose Muhando ashindwa kuhudhuria Tamasha la uimbaji Masasi.

SAM_0540
Askofu Oscar Mnung'a akitoa Tamko la Watu kurudishiwa Pesa zao baada ya Rose Muhando kushindwa kufika Viwanja vya Boma, Masasi
Katika hali isiyo ya kawaida, Madai mbalimbali ya kutokuhudhuria Matamasha yamezidi kumkumba Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Rose Muhando baada ya Mwimbaji huyo kutokuhudhuria Tamasha lililoandaliwa na Umoja na Akina Mama Wakikristo Masasi, Tamasha lililokuwa na lengo la Kukusanya Pesa kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Watoto Yatima huko Masasi.

Habari hiyo imeandikwa leo na Mtandao wa Lindi Yetu, huku kutokuhudhuria kwa Rose Muhando katika Tamasha hilo kukitajwa kuleta tafrani kwa Mashabiki waliokuwa tayari washachangia Tamasha hilo, huku Waandaaji wa Tamasha hilo wakilazimika kurudisha Pesa hizo kufutia hakikisho lililotolewa na Meneja wa Mwimbaji huyo Bw. Nathan Wami.
SAM_0517
Baadhi ya Mashabiki waliofika Viwanjani hapo kushuhudia Tamasha hilo
Mch. Carlos Raphael Marcus ambaye ni Makamu Askofu Dayosisi ya Masasi amesema kuwa, Wao walishakamilisha Malipo ya Tshs. Millioni 4 ambazo walilipa kwa Awamu 2, na Stakabadhi wanazo kuhakikisha walifanya hivyo, na ilivyotokea hivyo walimtafuta Meneja wa Rose Muhando Bw. Nathan ambaye aliwaomba radhi waandaje na kuomba arudishe Pesa hizo.

Kufuatia hali hiyo ya kutokutokea kwa Rose Muhando katika Viwanja vya Boma Masasi, Viongozi wa Dini akiwemo Askofu Oscar Mnung'a wa Dayosisi ya Kanisa Anglican Newala walilazimika kutoa Tamko la Mashabiki walioingia Uwanjani hapo kurudishiwa Pesa zao, zoezi lililomalizika kwa Amani licha ya Mashabiki wengi kusikitishwa na Kitendo hicho.