Askofu
mkuu Zygmunt Zimowski, Rais wa Baraza la Kipapa la shughuli za
kichungaji kwa ajili ya wafanyakazi katika sekta ya afya, hivi karibuni,
alizindua mradi wa kupima na tiba kwa wagonjwa wa Ukimwi, Jimbo
Katoliki Shinyanga, Tanzania.
Ni mradi unaoendeshwa kati ya Mfuko wa
Msamaria mwema, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania pamoja na Kampuni
ya dawa kutoka Marekani ijulikanayo kama Gilead Sciences.
Zaidi
ya watu 120, 000 wanatarajiwa kufaidika na mradi huu inayojikita
katika: sheria na kanuni za tiba; maadili na utu wema. Watoto yatima
watapewa kipaumbele cha pekee.
Mradi huu ni kielelezo cha mshikakano wa
dhati katika mchakato wa kumhudumia mtu mzima: kiroho na kimwili
unaofanywa na Makanisa mahalia kama sehemu ya Uinjilishaji wa kina.
Baraza la Kipapa la huduma za kichungaji kwa ajili ya wafanyakazi katika
sekta ya afya linapenda kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Baraza la
Maaskofu Katoliki Tanzania katika Jimbo Katoliki la Shinyanga.
Hizi ni juhudi zilizofanywa kwa ushirikiano mkubwa kati ya Marehemu Askofu Aloysius Balina wa Jimbo Katoliki Shinyanga pamoja na Monsinyo Jean Marie Mupendawatu, Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la shughuli za kichungaji kwa ajili ya wafanyakazi katika sekta ya afya, ambaye mara kadhaa alitembelea Tanzania ili kuangalia uwezekano wa utekelezaji wa mradi huu kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wa Ukimwi nchini Tanzania.

- Radio Vaticana -