Advertise Here

Monday, October 21, 2013

Harusi ya James Kalekwa na Frida Madenda.

James Kalekwa na Frida Madenda wakiwa wenye Furaha baada ya kuvishana Pete
Jumamosi ya Juzi ilikuwa ni Siku ya Harusi ya Bw. James Kalekwa na Frida Madenda iliyofanyika Mkoani Dodoma.

James Kalekwa ni Mwanataaluma, Mwandishi wa Vitabu na Mwalimu wa Neno la Mungu. Pia amekuwa akifundisha kupitia Mtandao huu kila siku za Jumatatu.

Unaweza kusoma Mafundisho ya James Kalekwa ya Jumatatu iliyopita kwa Kubofya Hapa

Hizi ni Baadhi tu ya Picha za Harusi ya Bw. James Kalekwa na Frida Madenda

Kwa tukio hili, leo hatutakuwa na Mafundisho ya James Kalekwa, Kwa Mafundisho yake mengine tembelea Mtandao huu Jumatatu Ijayo.

Mtandao huu unawatakia Maisha Mema yenye Furaha na Baraka tele.

Sunday, October 20, 2013

Kanisa Dar lachomwa Moto.

Kanisa la Baptist Vingunguti
KANISA la Baptist, lililoko Vingunguti jijini Dar es Salaam limechomwa moto usiku wa kuamkia Jana ambapo vitambaa na madhabahu vimeteketea kwa moto.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Marietha Minangi amesema kuwa, tukio hilo limetokea usiku wa saa nane, na hadi anazungumza na mwandishi, hakuna mtu aliyekuwa amekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda Minangi alisema, ilikuwa mapema mno kuhusisha tukio hilo na tofauti za imani za kidini. Alisema, polisi wanaendelea na uchunguzi.
 
Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Hezron Mwaisemba alimwambia mwandishi wa habari hizi kanisani hapo, kuwa wakiwa wamelala usiku kama saa nane na robo hivi, binti mwenye umri wa zaidi ya miaka ishirini aliwaamsha na kuwaambia kuwa, ameambiwa kanisa linawaka moto.

“Tuliamka na kuelekea kanisani, tukakuta kweli kanisa linaungua. Yule binti alituambia aligongewa dirisha na motto wa jirani akamwambia kuwa kanisa linawaka moto. Basi, tulipofika hapa tukakuta meza moja pamoja na ile ya madhabahuni vimeteketea kabisa.

"Tulikuta kisu na kiberiti na pembeni pale kulikuwa na moto walikusanya maboksi wakayachoma, naona lengo lilikuwa kuteketeza kabisa jengo hili. Kwa bahati nzuri tulifanikiwa kuzima moto kwa kutumia mchanga,” alisema Mchungaji Mwaisemba.

Mchungaji huyo alisema kuwa, tangu kanisa hilo lijengwe mahali pale mwaka 1992 limekuwa na uhusiano mzuri na majirani, hivyo wameshangazwa na kitendo hicho.

“Sijui huyo mtu au watu waliofanya kitendo hiki walikuwa na sababu gani. Sisi hapa tuna uhusiano mzuri sana na jamii yote hapa Vingunguti,” alisema.

Mchungaji huyo alisema kuwa, thamani ya vitu vilivyoungua moto inaweza kufika shilingi 200,000/=.

Hata hivyo, Mchungaji Mwaisemba alilalamika kuwa, ukiacha tukio hilo la kuchomwa moto kanisa lake lenye waumini wapatao 150 linakabiliwa na matukio mengi ya wizi, ambapo watu wasiojulikana wamekuwa wakifika kanisani hapo usiku na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo viti vinavyotumiwa na watoto wa shule ya awali inayomilikiwa na kanisa.
 

The Next Level Album Launching.

Tazama walichokifanya Glorious Worship Team kwenye Campus Night - Saut.

October 18, 2013 ilikuwa ni Siku ya Usiku wa Kusifu na Kuabudu ujulikanao kama Revival Flames Campus Night ndani ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustino, na Moja ya Vikundi vilivyohudumu ni Glorious Worship Team kutoka Dar es salaam.

Sasa tazama Video hii uone watu walivyokuwa Wakimsifu Masiha wakiongozwa na GWT toka Dar es salaam

Saturday, October 19, 2013

Yaliyojiri kwenye Revival Flames Campus Night ndani ya Saut - Mwanza.

USIKU wa kuamkia leo, ulikuwa ni Usiku wa kusifu na Kuabudu Maarufu kama Revival flames Campus Night iliyoandaliwa na Tafes Saut - Mwanza Campus na kufanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nyamalango kuanzia Mida kama ya Saa 3:00 Usiku na Kumalizika Mida kama ya Saa 10 usiku.

Vikundi mbalimbali vya Kusifu na Kuabudu vilihudumu katika Mkesha huo kama Vile Tafes Saut Praise & Worship Team, Tafes Choir, Huima Choir, n.k huku Neno la Mungu likitolewa na Pastor elisha Msanifu kutoka Kanisa la Highway of Holiness Cathedral lililopo Ilemela Jijini Mwanza.

Mbali ya vikundi hivyo kutoka chuo cha SAUT Mwanza, pia kundi Maarufu Maarufu la Glorious Worship Team(GWT) kutoka dar es salaam pia lilipata fursa ya Kuongoza sifa katika Usiku huo.

Sasa Tazama namna mambo yalivyokuwa Viwanjani hapo
Watumishi wa Mungu wakiwa Viwanjani hapo
Tafes Praise Team On Stage




Sasa mida kama ya Saa 7 hivi wakaingia glorious Worship Team na Mambo yakawa hiviiii...
Kwenye Mic ni Paul Clement



Emma Solo wa GWT

Sifa na Utukufu zirudi kwake yeye aliye Mkuu kupita wote Mbinguni na Duniani.

- Picha zote na Elia Migongo -