Advertise Here

Sunday, November 3, 2013

Jeans & T-Shirt R.I.O.T. Police ni leo hii ndani ya Makumbusho ya Taifa.

Kanisa lashauriwa kutumia Mitandao ya Kijamiii kueneza Injili.

Waziri wa habari nchini Nigeria Bwana Labaran Maku, amelishauri Kanisa Katoliki Nchini Nigeria kuanza mchakato wa matumizi ya njia za mawasiliano ya Jamii katika azma ya Uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili. Mchakato huu uliwezeshe Kanisa pia kuziinjilisha njia za mawasiliano ya kijamii kwani kwa kiasi kikubwa zimekuwa ni sababu ya kumong'onyoka kwa misingi ya maadili na utu wema.

Ili kutekeleza wajibu na dhamana hii nyeti, kuna haja kwa Kanisa nchini Nigeria kuwekeza katika majiundo makini kwa Mapadre na Watawa watakaoweza kutumia mitandao hii kwa umakini mkubwa kama sehemu ya Uinjilishaji, kwani kwa sasa kuna idadi kubwa ya vijana wanaoperuzi kwenye mitandao na wakati mwingine wanaambulia mitandao inayowayumbisha katika maisha yao kijamii na kimaadili.

Kanisa lijitahidi kuwa na mitandao hii katika taasisi zake za elimu na huduma jamii na wala zisiwe kwa ajili ya viongozi wachache tu wa Kanisa. Kwa kuwekeza katika mitandao ya kijamii, idadi kubwa ya watu wanaweza kupata fursa ya kusikia Habari Njema ya Wokovu ikitangazwa kwao! Hii ni kutokana na huruma na upendo wa Mungu kwa watu wake kwamba, leo hii watu wanaweza kuwasiliana kwa haraka na kwa upesi zaidi ikilinganishwa na miaka kadhaa iliyopita.

Mitandao ya kijamii anasema Bwana Labaran Maku inaweza kutumika kusoma Biblia, kuhubiri na kufundisha mambo msingi ya maisha. Ikiwa kama itatumika vyema, ulimwengu unaweza kuwa ni mahali pazuri zaidi pa kuishi. Bwana Maku ameyasema hayo hivi karibuni wakati alipokuwa anatoa mhadhara kwenye Seminari ya Kumbu kumbu ya Bigard iliyoko mjini Enugu, Nigeria.

- Radio Vaticana -

Saturday, November 2, 2013

Mke wa Makamu wa Rais wa Kenya aenda Zimbabwe kwa Maombi.

Mrs Ruto said the charges against Mr Ruto came as a shock to the family.
Rachel Ruto, Mke wa Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto
Rachel Ruto ambaye ni Mke wa Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto yupo Zimbabwe kwa Kikao cha Maombi na Mtume wa Spirit Embassy(Zimbabwe) Mtume Ubert Angels.

Mrs. Ruto ambaye ni rafiki wa Karibu wa Mke wa Mtume Ubert Angels, Beverly Angels amewasili Zimbabwe jana Mchana na ni Mgeni Rasmi katika Kongamano la Mwaka la wanawake lililoandaliwa na Spirit Embassy.

Kongamano hilo lililoanza jana jioni katika Jengo la "Spirit Embassy Royal Towers" katika Mji wa Harare, limekusanya zaidi ya Wageni wa Kimataifa 500.

Moja ya wageni muhimu katika Kongamano hilo ni Pastor Dona Ndifoni kutoka Marekani, na Kongamano hilo linadumu kwa Siku Mbili.

Asilimia 80 ya Mapato ya Tamasha la Krismasi kujenga kituo cha Wasiojiweza.

Bw. Alex Msama
Maandalizi ya msimu wa sikukuu yameanza na kwa mara ya kwanza mwaka huu kutakuwa na Tamasha la Krismasi ambalo litazunguka katika mikoa kadhaa nchini.
 
Mwandaaji ambaye pia huandaa Tamasha la Pasaka, Alex Msama amesema amefikia uamuzi huo kutokana na msukumo wa mashabiki wa burudani ya nyimbo za Injili ambao wamekuwa wakitaka awaandalie kitu kingine.

“Marafiki wa Tamasha la Pasaka walinishauri niandae jingine wakati huu wa Sikukuu ya Krismasi kwa kuwa ni wakati wa mapumziko marefu na ni mwisho wa mwaka,” alisema Msama.

“Mwishoni mwa mwaka watu wengi husafiri kuelekea makwao hivyo kulifanya Dar es Salaam peke yake kutawanyima watu wengi uhondo huo.”

Pia waandaaji wa Tamasha hilo la Krismasi wametangaza kuwa asilimia 80 ya mapato yatakayokusanywa kwenye tamasha hilo mwaka huu yatatumika kwenye ujenzi wa kituo cha wasiojiweza Pugu jijini Dar es Salaam.

Tamasha la Krismasi linaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Pasaka kila mwaka, linatarajiwa kufanyika Desemba 25 jijini Dar es salaam.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, ilieleza kuwa asilimia nyingine 20 itatumika kulipia ada yatima wanaosoma shule mbalimbali hapa nchini.

“Asilimia 80 ya mapato tutaipeleka kwenye ujenzi wa kituo chetu cha wasiojiweza tunachotarajia kukijenga Pugu, Dar es Salaam, huwa hatubahatishi tunapodhamiria jambo letu,” alisema Msama.

Kwa mujibu wa Msama, hivi sasa wanasubiri hati kutoka Wizara ya Ardhi kuhusiana na umiliki wa eneo hilo, na kwamba suala hilo litakapokamilika ndipo mchakato wa ujenzi utakapoanza, na wana imani jambo hilo halitachukua muda mrefu.

Alieleza kuwa wakati wanaanzisha Tamasha la Pasaka mwaka 2000, dhamira yao ilikuwa kila mwaka kusaidia wasiojiweza.

“Niwashukuru wadau mbalimbali waliotusaidia kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho na mpaka sasa tuna karibu sh milioni 120. Gharama nzima ya ujenzi ni kati ya sh milioni 800 hadi bilioni moja utakapokamilika.

“Dhamira yetu ni kuwa na kituo ambacho kitasaidia Watanzania wa mikoa mbalimbali ambao hawana uwezo katika masuala ya mavazi, elimu, vyakula na mengine mengi,” alisema Msama.

Alieleza kuwa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi imeamua lifanyike Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Desemba 25 na siku inayofuata watatazama mkoa gani waupe heshima.

Alisema hilo litakuwa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu na litakuwa na tofauti kubwa ukilinganisha na mengine yaliyowahi kuandaliwa na kampuni yake.

- Mwananchi & Tanzania Daima -

Friday, November 1, 2013

Mtandao wa "The Kenyan Daily Post" umetoa Orodha ya Waimbaji na Watangazaji wanaomuabudu Mungu katika Roho na Kweli.


Mtandao wa The Kenyan Daily Post umetoa Orodha ya Waimbaji wa Nyimbo za Injili na Watangazaji wa vipindi vya Kikristo pamoja Radio za Kikristo wa Nchini kenya wanaomuabudu Mungu katika Roho na Kweli.

Utoaji wa orodha hii umetokana na Skendo mbalimbali zinazowakumba waimbaji wa Nyimbo za Injili, ikiwa ni pamoja na skendo za ngono, ulevi na kutanguliza pesa kuliko huduma.

Yafuatayo ni Majina yaliyoorodheshwa kwa Mujibu wa mtandao wa Kenyan Daily Post kuwa Watu hawa ndio wanaomuabudu Mungu katika roho na Kweli.

Watangazaji wa Radio na Tv
1.Njugush na Joyce Omondi (Kubamba)
Watangazaji wa Citizen Tv ambao kwa sasa wapo Masomoni.

2. Anthony Ndiema
mtangazaji wa Kipindi Maarufu cha "Tuzuka" cha KTN. Ni mume wa Mke mmoja na Kiongozi wa Kanisa huko Kenya, na ni Mtu ambaye ni wa kiroho zaidi.

3. Lawrence Thuku
Japokuwa si mtu maarufu sana, kipindi chake kinachorushwa na Radio isiyo Maarufu sana ya "Truth FM" kimekuwa kikigusa Maisha ya watu wengi. Hajawahi kusikika katika "Scandal" yoyote.

4. Faith Muturi (Cross-Over Chart)
Japokuwa amekuwa akitangaza kipindi hicho na watu wenye Scandal mbalimbali hasa za Kupenda pesa Dj Sadic na Dj Mo, ni Mtu ambaye yupo vizuri Kiroho na pia ni Kiongozi wa Kuabudu kanisani kwao.

5. Mwinjilisti Lucy Ngunjiri (Kameme FM)
Ni mtu ambaye pia yupo vizuri kiroho, na ni moja ya Watangazaji wenye wasikilizaji wengi sana. Sauti yake pindi anapokuwa kwenye Kipindi imekuwa ikiwaponya watu wengi pasipo hata kuwagusa.

Waimbaji wa Nyimbo za Injili
1. Daddy Owen
Amekuwa kwenye Tasnia ya Muziki wa Injili kwa Kipindi kirefu sasa, na ameweza kutunza heshima yake. Wimbo wake wa "Kapungala" ulimfanya ajulikane zaidi, na aliomba kabla ya kurekodi wimbo huo.

2. Rufftone
Huyu ni Baba wa tasnia ya Muziki wa injili Nchini Kenya, na hajawahi kutajwa katika "Scandal" yoyote ile kwa zaidi ya Miaka 10 ya Uimbaji wake. Rufftone ni kiongozi katika Kanisa analosali na Wachungaji wamekuwa wakimpenda sana kutokana na Kujiheshimu kwake.

3. Mr. Googz
Huyu aliacha kuimba Miziki ya kidunia na Kuamua kuanza kuimba muziki wa Injili na Kuja kuwa Mchungaji. Mr. Googz aliachia wimbo ujulikanao kama "Gospel Celebrity", Wimbo uliokuwa ukiwataka Waimbaji wengine wa Nyimbo za Injili kuacha kumkejeli Mungu. Ni Muimbaji ambao amekuwa akichukia sana dhambi.

4. Ben Githae
Ni Muimbaji ambaye aina ya Muziki wake umekuwa ukiwagusa sana watu wa Rika mbalimbali. Ni mtu ambaye anajali sana Ukristo na mara nyingi amekuwa akiombea sana watu wanaoenda kwenye kumbi za Miziki ya kidunia ili waokoke.

5. Solomon Mukubwa
Ni kiongozi wa Nyimbo za kuabudu na Mara nyimbo Nyimbo zake zimekuwa zikiwaponya watu pasipo hata kuwagusa. Aliomba sana na kufunga kwa miezi mitatu kabla ya kutoa wimbo wake wa "Mfalme wa Amani".

6. Gloria Muliro
Ni moja ya Waimbaji wenye Mafanikio makubwa sana nchini Kenya ambaye ameolewa na Mchungaji. Muimbaji huyu anamiliki Kanisa, na pia ana tabia ya Kuomba na Kufunga kabla ya kutoa wimbo wowote ule. Siku za Karibuni amekataa Ombi la Willy Paul ya kuimba kwenye wimbo wake kwasababu Willy Paul ni Muimbaji mwenye Scandal nyingi sana na hana hofu ya Mungu.

7. Eunice Njeri
Ni Muimbaji wa nyimbo za kuabudu na Mtu anaeweka mkazo sana kwenye Maswala ya wokovu. Kwake yeye kutengeneza wimbo, ni mpaka aende Milimani kuzungumza na Mungu ili ampe wimbo wa kutengeneza.

8. Mercy Wairegi
Naye pia ni Kiongozi wa Kuabudu, na Mtu pia anayejali sana Maswala ya Wokovu.


ZINGATIA: Orodha hii ni kwa Mujibu wa Mtandao wa The Kenyan Daily Post