Advertise Here

Monday, March 5, 2012

Martha Mwaipaja azungumzia ndoa yake na Mch. John Said.

Martha mwaipaja akiwa na Mumewe Mch. John Said

Siku ya Jana ilikuwa ni Furaha ya Ajabu kwa Wanandoa hawa Wawili baada ya kufunga Ndoa katika Kanisa la Udhihirisho wa Injili, lililopo maeneo ya Kipunguni B Ukonga, jijini Dar es salaam, na kufuatiwa na Shughuli ya Kuwapongeza wanandoa hao iliyofanyika na Katika Ukumbi wa Delux, ulioko maeneo ya Sinza jijini Dar es saalam.


Gospel News Media ilipata nafasi ya Kuzungumza na wanandoa hao, mara tu baada ya Kufunga ndoa. Na haya ndo yalikuwa Mazungumzo yetu………
 

Gospel News Media; Martha, unaizungumziaje siku ya Leo?

Martha Mwaipaja; Kiukweli, siku ya Leo ni siku ya tofauti sana, kwasababu ni Siku 1 na huwa haijirudii maishani Mwote. Kwahiyo ni Siku maalum sana kwangu.

Gospel News Media; Unahisi kwa nini amekuwa Mch. John na si Mwanaume Mwingine?

Martha Mwaipaja; Nahisi ni Mpango wa Mungu, kwasababu ningeweza kuwa na Mwanaume mwingine, lakini Mpango wa Mungu ni Mimi kuwa na Mch. John.

Gospel News Media; Nini unajivunia kwa Mch. John?

Martha Mwaipaja; Mume wangu Mch. John, anampenda sana Mungu.

Gospel News Media; Ni wakina nani ungependa sana kuwashukuru kwa Kufanikisha hili?

Martha Mwaipaja; Kwanza ni Wazazi wetu wote wa Pande mbili, jamaa na marafiki, pamoja na Wageni wote waliofanikisha shughuli hii.

Gospel News Media; Nini Neno lako la Mwisho?

Martha Mwaipaja; Nawapenda na Nawathamini sana watu wote wanaonisapoti na Wanaoniombea kila siku iitwapo leo.
Baada ya Kuzungumza na Marhta Mwaipaja, ikafuata zamu ya Mume wake Mch. John Said…….
 

Gospel News Media; Kwa upande wako Mch. John, unaizungumziaje siku hii ya Leo?

Mch. John; Hii ni Siku ambayo ilikuwa ikinipa msongo wa Mawazo sana hapo awali juu ya Muonekaniko wetu. Niliwaza sana ni kwa namna gani Shughuli itakuwa. Lakini namshukuru Mungu, mana amefanya kuwa Siku ya furaha zaidi Kwetu.

Gospel News Media; Unahisi ni Kwanini amekuwa Martha, na si Mwanamke Mwingine?

Mch. John; Mungu alinipa Macho ya Rohoni hivyo nikamuona Martha. Martha ni Ubavu wangu ambao Mungu amenipa kwa ajili yangu.

Gospel News Media; Nini unajivunia kwa Martha?

Mch. John; Martha ni Mkweli, anampenda Mungu, Muwazi na pia Ananipenda.

Gospel News Media; Unapenda kuwashukuru wakina nani waliofanikisha hili?

Mch. John; Kwanza ni Mke wangu Martha, mana bila yeye sidhani kama hili lingetokea. Na Wazazi wote, pamoja na Wote waliojitoa kwa ajili ya kufanikisha shughuli hii.

Gospel News Media; Neno lako la Mwisho?

Mch. John; Wote waliojitoa kwa hili, Mungu atawalipa, mana tumetumia gharama kubwa sana, lakini hii yote ni kwasababu tukio hili huwa hilijirudii mara 2.

Gospel News Media; Asanteni sana kwa Ushirikiano wenu.

Martha na Mch. John; Asante pia.

Hata hivyo, Martha amesema kuwa watu wakae mkao wa Kupokea kitu kipya toka kwa kwake, kwani yuko mbioni kutoa Albam Mpya aliyoiita Jina la OMBI LANGU KWA MUNGU. Albam hiyo itakuwa na Nyimbo 8, na Kati ya hizo ni Ombi langu kwa Mungu, Yesu ni Mzuri, Kaa na Mimi tena, Jaribu la Mtu, Kweli Nimetambua, na Sifa Zivume. Kuhusu Albam hii Martha anasema, “kama Mipango ikienda kama ilivyopangwa, Albam hiyo nitaizindua Mwezi wa 4 Mwaka huu.”

Friday, March 2, 2012

Martha Mwaipaja asherehekea Send Off Party yake ndani ya Diamond Jubilee.

Martha akiwa na Mumewe mtarajiwa Mch. John

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Martha Mwaipaja, jana usiku ilikuwa ni Sherehe ya Send Off Party yake, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee (VIP HALL).
Siku chache zijazo, yaani kesho kutwa, Martha atakuwa akifunga ndoa na Mch. John Said wa Kanisa la UDHIHIRISHO WA INJILI lililopo maeneo ya Kipunguni B, Ukonga jijini Dar es salaam.

Martha akiwa na waimbaji mbalimbali wa Nyimbo za Injili

Akizungumzia sherehe hiyo, Mch. John anasema “Ndoa yetu itafungwa Jumapili ijayo March 4, 2012 katika kanisa la Ukonga, na kufuatiwa na Shughuli itakayofanyika katika Ukumbi wa Sinza Delux kuanzia mida ya Saa 1 usiku.”

Kitchen party ya Martha Mwaipaja, ilifanyika Jumapili iliyopita February 26, 2012.

BLOG HII INAWATAKIA HARUSI NJEMA, NA MAISHA MEMA YENYE FURAHA TELE.