Advertise Here

Thursday, February 14, 2013

Facebook na Watumishi wa Mungu mbalimbali Leo.

T.D. Jakes Ministries Love is the power that helps you to perform. The enemy wants most to destroy your love. Love is what kept Christ nailed to the cross, not the nails themselves. Love is what causes Him to remain patient with us. He will love you when there are no apparent reasons to do so.
The Donnie McClurkin Show HAPPY VALENTINE'S DAY to those IN love! To those of us who aren't IN love, yet know the single art of LOVE, CONTINUE! GBY


DON MOEN (Praise & Worship Leader) "Having purified your souls by your obedience to the truth for a sincere brotherly love, love one another earnestly from a pure heart."
 
TB Joshua Ministries DO YOU HAVE A RELATIONSHIP WITH JESUS?John 21:17 – “He said to him the third time, ‘Simon, son of Jonah, do you love Me?’ Peter was grieved because He said to him the third time, ‘Do you love Me?’ And he said to Him, ‘Lord, You know all things; You know that I love You.’ Jesus said to him, ‘Feed My sheep’. ”
 
The main point of Christianity is not the work we do but the relationship we maintain and the atmosphere produced by our relationships. If you want to be strong in the Lord, you must maintain a strong relationship with Him. Before you can have a relationship with Jesus, it must be because of your love for Him. That was why Jesus repeated His question to Peter three times; He wanted the concept to be crystal clear that love is the centre. We must love nothing in comparison to God but in reference to Him alone. God is the only reason, the only concern and the only thing for a true Christian. Life does not start with a love for people but a love for God and that love overflows to people. If any man says he loves God, he is under obligation to care for his fellow man. Our relationship with God transcends time and influences all other relationships. How is your relationship with Jesus?
 
 Joyce Meyer Ministries God loves you more than you can imagine, He sent the ultimate Valentine's Day gift (John 3:16)
 
Pastor-Donis And-Nnunu Nkone Jamani Valentines Day siyo siku ya kumfurahisha Mchumba/boy friend/girl friend na kumkosea Mungu KWA MAKUSUDI ! Angalia saana usije ukaishia kusema "Bwana ametoa, Bwana ametwaa" kwa kuwa umeshindwa kumheshimu Mungu aliyekupa huyo mchumba. KUMBUKA KUMUHESHIMU MUNGU KWANZA ! Happy Valentines Day!
 
 Evangelist Munishi Colman No other book has done the things the Bible has done.The Bible tells of the only way for man to have peace witi God. It tells how man must be born again.

Millioni 200 kutumika kwa ajili ya Tamasha la Pasaka Mwaka huu.

mkurgenzi2. msama
Bw. Alex Msama

KIASI cha Sh. Milioni200 kitatumika kwa ajili  Tamasha la Pasaka mwaka huu, ambalo kwa mara ya kwanza litafanyika katika mikoa saba tofauti.


Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama alisema fedha hizo zitatumika kwa masuala mbalimbali ikiwemo kulipa wasanii, misaada katika masuala mbalimbali ya kijamii na gharama za kawaida mahali watakapofanya maonesho.


“Kila mwaka Tamasha la Pasaka linafanyika katika mikoa miwili, kwa maana ya Dar es Salaam na mkoa mwingine tutakaouchagua, lakini mwaka huu kwa mara ya kwanza litafanyika katika mikoa saba.


“Kwa hiyo gharama zake kidogo zitaongezeka na tunakadiria kwa mikoa yote hiyo kiasi cha Sh. Milioni 200 kitatumika maana tutakuwa na wasanii zaidi ya 30, tunaamini wengi watajumuika nasi kulipa viingilio ili kuwezesha dhamira yetu ya kupeleka ujumbe kwa njia ya muziki ufike,” alisema Msama.


Alisema tayari wamekubaliana Machi 31 mwaka huu ambayo ni siku ya Pasaka tamasha lifanyike Dar es Salaam, lakini baada ya hapo mikoa mingine itakayofuata wataitangaza.


Msama alisema dhamira yao safari hii kwenye tamasha hilo ni kuhamasisha umoja, amani na mshikamano miongoni mwa jamii ya kitanzania.


“Kila mwaka huwa tuna jambo ambalo tunaliangazia, safari hii tumeamua kuwa tamasha letu litasisitiza amani na upendo,” alisema Msama.


Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

 

  Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

Tuesday, February 12, 2013

Emmanuel Nyambita; Natamani sana kufanya Kazi na Mwimbaji Don Moen.

Emmanuel Nyambita
Emmanuel Nyamita ni Mwimbaji wa Nyimbo za Injili toka mkoani Mwanza ambaye kwasasa Makao yake Makuu yako Nchini Kenya katika Jiji la Nairobi.

Aina ya muziki anaoufanya, umekuwa kivutio tosha kwa kila anayemsikiliza na kumtazama. Kwa muda mrefu sana amekuwa akifanya Muziki wa LIVE huku akipiga Gitaa lake aina ya Acoustic ambalo alifundishwa na Bw. Joshua aliyekuwa akiishi Maeneo ya Nsumba Jijini Mwanza.
Emmenuel ambaye ni Mhitimu wa Shahada ya Elimu toka Chuo Kikuu cha Mt. Augustino cha Jijini Mwanza - Tanzania(2012), anasema alianza shughuli hizi za Uimbaji Mwaka 2000 akiwa nyumbani kwao.

Emmanuel anasema "Baada ya hapo nilianza kuwa serious nilipojiunga na Nsumba secondary iliyopo Jijini Mwanza, ambapo nilijiunga na kaka yangu na rafiki zake. Wao walikua Kidato cha 4 wakati Mimi nikiwa Kidato cha Kwanza. Hiyo ilikuwa Mwaka 2003.
 
Kwahiyo tukaimba pamoja nao kwa Mwaka 1 na Kisha wakaondoka na kuniacha peke yangu. Baadaye nikaunda Kundi nikiwa na Marafiki zangu tulilolipa Jina la LTS mpaka tunamaliza Kidato cha 4.

Nilibahatika kufaulu kidato cha 4 na hivyo kuchaguliwa Shule ya Serikali lakini sikujiunga na shule hiyo ya sekondari ya serikali na hivyo nikaamua kwenda shule Binafsi ya Ikizu High School sababu walikuwa wanafundisha somo la Muziki.
Emmanuel akiwa na Harris Kapiga katika kipindi cha Gospel Tracks kupitia Clouds Fm
Kwa bahati mbaya huko nako nikakuta Mwalimu wa Somo la Muziki kaondoka lakini palikuwa ni sehemu sahihi pa kukuza vipaji hasa vya Muziki mana kulikuwa kuna Talents Night, na pia uimbaji ulipewa kipaumbele sana.

Hapo shuleni nilikutana na Rafiki yangu aitwaye Gerlad Saul (kwa sasa yupo IFM) na kisha tukaunda kundi la "The Two Brothers" tukiwa wawili tu. Kwakweli tulikuwa tunafanya vizuri sana mpaka tunamaliza shule.
 
Baada ya hapo nikafanikiwa Kufaulu Masomo yangu na Kujiunga na Chuo Kikuu cha Mt. Augustino kilichopo Mwanza, Tanzania na kuendelea na Shughuli za Uimbaji mimi peke yangu."

ALBUM YAKE MPYA YA SASA
Emmanuel amefanikiwa kurekodi Album yake yenye Jina la NINARUDI, Albam aliyoifanya katika Studio ya 3J Studio ya Jijini Nairobi, chini ya Producer Allan Mayindo ikiwa katika Mfumo wa Audio Cd na Sasa anamalizia Video ya Nyimbo zake hizo katika Mfumo wa DVD na Muda wowote kuanzia Sasa itapatikana Madukani.

Album hiyo ina Nyimbo 7 zikiwemo Nyimbo kama Touch me, Wanataka kunitoa Roho, What do we do na Nyinginezo. Album hiyo itakuwa na Nyimbo zilizoimbwa kwa lugha 2 ya Kiswahili na Kiingereza. Na anasema aliamua kuimba kwa kutumia lugha ya kiingereza kwasababu ana lengo la kufanya muziki wa Kimataifa.
 

MALENGO YAKE YA BAADAE
Kwa Upande wa Malengo yake ya baadae, Emmanuel anasema anatamani sana Kufanya Muziki wa Injili katika level ya Kimataifa, na Pia anatamani sana kufanya Kazi na Mwimbaji wa Kimataifa wa Nyimbo za Injili Don Moen.

Kwa Maelezo zaidi, wasiliana Nae;
Email; e.nyambita@gmail.com
Facebook Account; Emmanuel Nyambita

JIANDAE KUJIPATIA NAKALA YAKO!!!

Monday, February 11, 2013

Vita vya Waislamu na Wakristo Geita, Mchungaji Auawa.

HUKO mkoani Geita, kuna vita kati ya Waislamu na Wakristo, kufuatia hatua ya Wakristo kuchinja mifugo kwa nia ya kuuziana wenyewe kwa wenyewe kwenye bucha walilotenga.

Jambo hilo linaelezwa kuzua tafrani kwa jamii ya Waislamu, kwani waliamua kuvamia eneo hilo na kuharibu bucha, pikipiki eneo hilo, na kusababisha watu kuingilia, na vita kuibuka, silaha za jadi zikitumika.

TUKIO:

Wakristo Mkoani Geita eneo la Katoro na Buselesele, waliamua kuachana na kununua nyama katika bucha za kawaida kwa madaikwamba hiyo ni ibada kwa waislamu, na hivyo wao hawako tayari kushiriki ibada hiyo, na badala yake watafanya ya kwao. Ndipo walipokwenda Kituo cha Polisi na kuomba kibali cha kuchinja, ambacho walipewa ilmradi wasiuze nyama hiyo.

hatimaye Wakrsito hao wakachinja na kuamua kupeleka kwenye bucha lao ambalo wamelitenga kwa ajili ya waumini wao kununua. Waislamu kuona hivyo, ndipo wakaenda kuripoti kituoi cha Polisi, na wakati Polisi (wachache) wanaongea na viongozi wa Kikristo eneo hilo ili kutatua na kurejesha amani, ndipo kundi la Waislamu likaja na kuanza kushambulia kilichokkuwa eneo hilo, wakivunja bucha, na pikipiki ya mkristo mmojawapo iliyokuwa eneo hilo.

Hatua hiyo imeelezwa kuibua hasia na kupelekea baadhi ya wat waliokuwa eneo hilo kuanza kujibu mashambulizi hayo, na mpaka hivi sasa inaripotiwa kuwa nguvu zaidi ya Jehi la Polisi haijafika eneo hilo, huku waumini wawili wa dini ya Kiislamu wakiwa katika hali mbaya kutokana na kipigo.

Silaha ni za jadi, na eneo hilo haliko salama kwa hivi sasa, kwani hata amduka mengine yamefungwa kuhofia usalama wa mali na maisha.

Akihojiwa na Beatrice Kamanga, katibu wa umoja wa makanisa ya Katoro na Buselesele, Mchungaji Silvanus Dominick, ameeleza kuwa kama hali haitatulizwa mara moja basi eneo hilo laweza kuleta madhara zaidi.

TAARIFA ZILIZOFIKA HIVI PUNDE:
Taarifa za hivi punde ni kuwa kuna Mchungaji ameuwawa kwa kushambuliwa na silaha mbalimbali ikiwemo mawe. Halikadhalika pia kuna msikiti ulichoma moto hapo awali.

- Gospel Kitaa -

Papa Benedict XVI atangaza rasmi kuachia madaraka.

Papa Benedict XVI
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict XVI ametangaza kuachia madaraka ya kuongoza kanisa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, uamuzi ambao ni wa kwanza tangu karne ya 15 kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la AFP.

Msemaji wa Papa, Federico Lombardi amesema kiongozi huyo wa juu kabisa wa Kanisa Katoliki duniani, ataachia ofisi rasmi tarehe 28 Februari, Mwaka huu saa mbili kamili asubuhi huku akiwa na Umri wa Miaka 85.

Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya Vatican wanasema safari hii, kuna uwezekano mikoba ya Baba Mtakatifu Benedict XVI ikarithiwa na Kardinali kutoka Afrika.

Kardinali Peter Turkson wa Ghana ametajwa kama mrithi-mtarajiwa wa nafasi hii nyeti ndani ya Kanisa Katoliki, linalokadiriwa kuwa na waumini zaidi ya bilioni moja dunia nzima.

Mwingine ni Kardinali Francis Arinze; mzaliwa wa Nigeria ambaye alichukua nafasi ya Benedict XVI kama Kardinali-Askofu wa Velletri-Segni alipoteuliwa kuwa Papa miaka nane iliyopita.

- Mwananchi -