Emmanuel Nyambita |
Emmanuel Nyamita ni Mwimbaji wa Nyimbo za Injili toka mkoani Mwanza ambaye kwasasa Makao yake Makuu yako Nchini Kenya katika Jiji la Nairobi.
Aina ya muziki anaoufanya, umekuwa kivutio tosha kwa kila anayemsikiliza na kumtazama. Kwa muda mrefu sana amekuwa akifanya Muziki wa LIVE huku akipiga Gitaa lake aina ya Acoustic ambalo alifundishwa na Bw. Joshua aliyekuwa akiishi Maeneo ya Nsumba Jijini Mwanza.
Emmenuel ambaye ni Mhitimu wa Shahada ya Elimu toka Chuo Kikuu cha Mt. Augustino cha Jijini Mwanza - Tanzania(2012), anasema alianza shughuli hizi za Uimbaji Mwaka 2000 akiwa nyumbani kwao.
Emmanuel anasema "Baada ya hapo nilianza kuwa serious nilipojiunga na Nsumba secondary iliyopo Jijini Mwanza, ambapo nilijiunga na kaka yangu na rafiki zake. Wao walikua Kidato cha 4 wakati Mimi nikiwa Kidato cha Kwanza. Hiyo ilikuwa Mwaka 2003.
Kwahiyo tukaimba pamoja nao kwa Mwaka 1 na Kisha wakaondoka na kuniacha peke yangu. Baadaye nikaunda Kundi nikiwa na Marafiki zangu tulilolipa Jina la LTS mpaka tunamaliza Kidato cha 4.
Nilibahatika kufaulu kidato cha 4 na hivyo kuchaguliwa Shule ya Serikali lakini sikujiunga na shule hiyo ya sekondari ya serikali na hivyo nikaamua kwenda shule Binafsi ya Ikizu High School sababu walikuwa wanafundisha somo la Muziki.
Emmanuel akiwa na Harris Kapiga katika kipindi cha Gospel Tracks kupitia Clouds Fm |
Kwa bahati mbaya huko nako nikakuta Mwalimu wa Somo la Muziki kaondoka lakini palikuwa ni sehemu sahihi pa kukuza
vipaji hasa vya Muziki mana kulikuwa kuna Talents Night, na pia uimbaji ulipewa kipaumbele
sana.
Hapo shuleni nilikutana na Rafiki yangu aitwaye Gerlad Saul (kwa sasa yupo IFM) na kisha tukaunda kundi la "The Two Brothers" tukiwa wawili tu. Kwakweli tulikuwa tunafanya vizuri sana mpaka tunamaliza shule.
Baada ya hapo nikafanikiwa Kufaulu Masomo yangu na Kujiunga na Chuo Kikuu cha Mt. Augustino kilichopo Mwanza, Tanzania na kuendelea na Shughuli za Uimbaji mimi peke yangu."
ALBUM YAKE MPYA YA SASA
Emmanuel amefanikiwa kurekodi Album yake yenye Jina la NINARUDI, Albam aliyoifanya katika Studio ya 3J Studio ya Jijini Nairobi, chini ya Producer Allan Mayindo ikiwa katika Mfumo wa Audio Cd na Sasa anamalizia Video ya Nyimbo zake hizo katika Mfumo wa DVD na Muda wowote kuanzia Sasa itapatikana Madukani.
Album hiyo ina Nyimbo 7 zikiwemo Nyimbo kama Touch me, Wanataka kunitoa Roho, What do we do na Nyinginezo. Album hiyo itakuwa na Nyimbo zilizoimbwa kwa lugha 2 ya Kiswahili na Kiingereza. Na anasema aliamua kuimba kwa kutumia lugha ya kiingereza kwasababu ana lengo la kufanya muziki wa Kimataifa.
MALENGO YAKE YA BAADAE
Kwa Upande wa Malengo yake ya baadae, Emmanuel anasema anatamani sana Kufanya Muziki wa Injili katika level ya Kimataifa, na Pia anatamani sana kufanya Kazi na Mwimbaji wa Kimataifa wa Nyimbo za Injili Don Moen.
Kwa Maelezo zaidi, wasiliana Nae;
Email; e.nyambita@gmail.com
Facebook Account; Emmanuel Nyambita
JIANDAE KUJIPATIA NAKALA YAKO!!!