Advertise Here

Sunday, February 24, 2013

Dokii azungumzia ulokole wake!

Dokii
Bwana Yesu asifiwe Dokii.

Dokii: Ameeen!

Swali: Siku za nyuma ilisemekana uliokoka na kuachana na matendo maovu na ukafanikiwa kutoa albamu moja ya nyimbo za injili lakini nasikia umepotoka, kulikoni?

Dokii: Nani kasema nimekengeuka. Mimi ni mlokole safi hata Mungu anajua hilo. Hata mimi nasikia watu wanasema nimeachana na wokovu lakini hawajui suala la wokovu ni la mtu binafsi na Mungu wake.

Swali: Unahisi kwa nini wanasema umeachana na wokovu?

Dokii: Nafikiri kwa sababu ya kuona nimerejea katika masuala ya sanaa ambayo ndiyo yalinifanya nijulikane mpaka leo hii. Watu wengine huwa wananishangaa kuona nimesuka aina fulani ya mtindo ambao huwa hawaupendi.

Swali: Inasemekana umekuwa ukienda kwenye majukwaa ya kumbi za burudani na kufanya mambo ambayo ni chukizo mbele za Mungu na kuonekana kama huna wokovu ndani yako. Je, ni kweli?

Dokii: Siyo kweli. Mimi huwa siwaelewi watu wanaojiita walokole kwa kufuatilia maisha ya mtu. Hata maandiko yanasema asiyefanya kazi na asile. Sasa mimi nikifanya kazi ya sanaa naonekana ni mtenda dhambi. Wangapi ambao wanafanya mambo ambayo ni machukizo mbele za Mungu na hawasemi chochote? Nimesoma sana Biblia sijaona sehemu inapomuelekeza mtu kazi ya kufanya bali imesema asiyefanya kazi na asile. Ninachojua mimi nafanya kazi ambayo ni halali hata Mungu anaitambua, wanaosema mimi nimekengeuka wananikosea heshima.

Swali: Kwa nini uliamua kuachana na uimbaji wa nyimbo za injili ukaanza kuimba nyimbo nyingine?

Dokii: Mimi bado ni mwimbaji wa nyimbo za injili na mpaka sasa ninaimba katika kwaya moja maeneo ya Mwananyamala, ukifika hapo ndiyo watakwambia kama kweli mimi nimeacha wokovu.

Swali: Unaimba katika kwaya gani?

Dokii: Ninaimba katika kwaya moja maeneo Upanga katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG).


Swali: Kwa nini uliachana na muziki wa Injili na kurejea upande wa pili?


Dokii: Muziki wa Injili unahitaji utulivu sana na pia unahitaji kuwa na mtaji wa kutosha ili ufanye promosheni. Nililazimika kukaa pembeni kwa sababu najua kama ningeamua kujikita zaidi huko, leo hii nisingekuwa hapa nilipo.

Swali: Kama ni hivyo kwa nini usingebaki katika ulokole huo na kucheza sinema za kilokole ili kuponya roho za watu wengi zinazoangamia?


Dokii: Sawa lakini wakati wa kufanya hivyo haujafika na ipo siku nitafanya hivyo.


Swali: Staili zako za unyoaji na mavazi yako ndivyo huwafanya watu washindwe kukuamini kama kweli umeokoka. Unalizungumziaje hili?


Dokii: Ni kweli kabisa, lakini kila nikisoma maandiko matakatifu sioni kama yanaelekeza jinsi ya uvaaji ama unyoaji. Nawashangaa wanaonisema juu ya uvaaji wangu.

Hayo ndo yalikuwa Mazungumzo kati ya Mwandishi wa Habari hii na Dokii.

- George Kayala -