Askofu mkuu na balozi wa Papa hapa nchini Fracinsco Padilla akiwa na mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi wakikata utepe wa jengo la kutolea huduma ya Mama na Mtoto katika hospital ya Ndala - Tabora |
Askofu Fracinsco
Padilla alitoa Kauli hiyo baada ya kufungua majengo ya kutolea
huduma kwa mama na watoto, pamoja na chumba cha upasuaji chenye vifaa vya kisasa ambavyo vyote vimegharimu
jumla ya shilingi milioni 465.
Balozi huyo wa papa hapa nchini alisema kwamba huduma nzuri
za afya kwa watanzania ndio kitu muhimu sana kwani bila afya hakuna amani, hakuna upendo
na hakuna chochote ambacho wananchi wanaweza kupata kumbukumbu ya kuwepo kwake
hospital hiyo hata baada ya miaka 50 ijayo.
Aidha aliwataka watoa huduma wote wa hospitali hiyo kufanya
kazi kwa Moyo wa kujitolea kwa watanzania wote wanaofika katika hospitali hiyo
kupata huduma ya matibabu ili kutimiza malengo ya Mungu kwa kutoa na
kupokea.
Hata hivyo alisema kwamba hospitali ya Ndala kutimia miaka 50
ikiwa inaendela kutoa tiba kwa wananchi wa Tanzania, ni jambo zuri la kujivunia
na la mafanikio makubwa sana kwa kanisa na waumini wake.
Awali Sista mkuu wa Hospitali hiyo Bernadette Kessy wakati
akisoma risala kwa barozi wa papa nchini Askofu mkuu Fracinsco Padilla Kessy alisema kuwa mbali ya ukosefu huo wa fedha pia
wanakabiliwa na ukosefu wa chumba chenye ukubwa wa kutosha kwa ajili ya
kutolea huduma za maabara ya magonjwa ya binadamu.
Pia alisema kwamba hospitali hiyo inaukosefu wa gari la huduma
kwa wagonjwa waliombali na hospitali gari ambalo hutumika kusarisha wagonjwa
mahututi katika hospitali za rufaa.
Hata hivyo Sista Kessy alimweleza Balozi huyo wa Vatcan nchini
kuwa pamoja na kuwepo kwa changamoto hizo lakini wameweza kuboresha
miuondombinu ya majengo ya zamani na kuyafanya kuwa ya kisasa .
Aidha amebainisha kwamba mbali na kuboresha majengo hayo,
wameanza kujenga majengo mengine manne mpya ambayo ni jengo la huduma ya
upasuaji, jengo la huduma ya tiba kwa watu wanaoishi na VVU, jengo la huduma ya
afya ya mama na mtoto pamoja na jengo la wodi ya wagonjwa wa kifua kikuu.
Aidha hospitali hiyo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki jimbo kuu la Tabora licha ya kutimiza miaka 50 tangu ianze kutoa huduma ya afya kwa jamii mwaka 1963, bado inakabiliwa uhaba mkubwa wa fedha za kununulia madawa ya kutosha, vifaa tiba, vitendanishi na upungufu wa Watumishi wa kada zote.