Advertise Here

Monday, August 19, 2013

Kiwewe na Matumaini waokoka.

Kiwewe na Matumaini katika Pozi
MSANII wa Kundi la Ze Komedi, Robert Augustino ‘Kiwewe’ na mwenzake Tumaini Martin ‘Matumaini’ wameamua kuacha anasa na kumrudia Mungu kwa kuokoka.

Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema kilichosababisha kuchukua uamuzi huo kwa wakati mmoja ni kutokana na manzingira waliyolelewa tangu wakiwa wadogo, yaani kumjua Mungu.

“Niliamua kufanya uamuzi sahihi ambao naamini utanibadilishia maisha yangu kwa kiasi kikubwa, kwa kufuata mambo yanayompendeza Mungu na siyo starehe za ujana,” alisema Kiwewe huku akiungwa mkono na Matumaini na wakabainisha kuwa kwasasa wanasali kwa Mchungaji Josephat Gwajima.

Wasanii hao walisema, ili kuhakikisha wanaungana na Mungu katika kila jambo, wameamua kuanzisha kundi lao la muziki wa Injili, lijulikanalo kama Comedians Gospel linaloundwa na wao pamoja na Mkono.

CHANZO: Grobal Publishers

Semina ya kubwa ya "Majira ya Urejesho" yakamilika Mwanza.

Mwl. Wilhard Mwanri (Arusha)
ILE Semina kubwa ya Neno la Mungu iliyoanza Jumapili ya tarehe 11 mwezi huu, imekamilika siku ya Jana huku watu mbalimbali wakifunguliwa na kurejeshewa vile vitu ambavyo Ibilisi aliviiba kutoka kwao.
Mwl. Mwanri akiombea watu mbalimbali wakati wa Semina
Semina hiyo iliyodumu kwa Siku 8, ilifanyika maeneo ya Nyegezi, Tema Hotel Ukumbi Mkubwa, huku wanenaji wakiwa ni Mwl. Wilhard Mwanri kutoka Arusha na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la New Vine Christian Centre.
Watu wakifunguliwa

Wednesday, August 7, 2013

Askofu Kakobe akanusha uvumi wa kulikimbia Kanisa lake.

Askofu Zakary Kakobe
ASKOFU wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship amekanusha uvumi ulio tapakaa kwa Watanzania yakuwa amewakimbia wakristo wake na kuenda nchi za nje.

Alikanusha uvumi huo baada ya kuongoza mazishi ya aliyekuwa Askofu wa kanisa la Christian Love lililopo  Kiwalani, aliyefaliki tarehe 2 Agosti mwaka huu.

Mazishi ya mchungaji huyo yaliambatana na ibaada ambayo iliongozwa na Kakobe katika makaburi ya Kinondoni juzi. Kakobe alisema kuwa yeye hajaondoka nchini kama Watanzania wengi wanavyosema. 

"Sijaondoka na siwezi kuondoka kwasababu mimi ni wa hapahapa na nitazidi kuwa hapahapa, na tutabanana hapahapa, hakuna kwingine tena. Huwa natoka kihuduma tu na huwa narudi tena, na sio kuwa nimehama", alisema Kakobe

Kumekuwa na ukimya sana kwa Askofu huyo kitu kinachowashangaza wengi, kwani walishazoea kumuona akiongea kwenye vyombo vya habari mara kwa mara.
 
Mmoja wa wakristo wake alikili kuwa kwa sasa Askofu wao amepoteza umaarufu tofauti na zamani ndiyo maana watu wengi wanafikia uamuzi wa kufikiri hayupo nchini.

Kwaupande mwingine kinachoshangaza ni kwamba ujio wake katika msiba huo wa Askofu mwenzake ilikuwa ni safari ya kutokea nchi za nje ambapo aliingia nchini siku ya jumapili ya Agost 4 mwaka huu.