Advertise Here

Friday, October 18, 2013

Changia Ujenzi wa Kaburi la Askofu Dr. Mosses Kulola.

Marehemu Askofu Dr. Mosses Kulola enzi za Uhai wake.
Ikiwa imepita Miezi kadhaa baada ya Kufariki kwa Shujaa wa Injili Askofu Dr. Mosses Kulola, Ujenzi wa Kaburi lake lililopo Kanisa la EAGT Bugando - Mwanza Umeanza ili kuhifadhi Kaburi hilo katika hali nzuri.
Ujenzi wa Kaburi ulipofikia
Kupitia Ukurasa wake wa Facebook, Mtoto wa Askofu Mosses Kulola ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya - Mwanza, Mch. Daniel Kulola amesema Ujenzi huo Umeshaanza lakini kwa sasa wamesisima ili kuvuta nguvu kwanza ya kumalizia Ujenzi huo.

Sehemu iliyobaki ni Ripu, Matofali ya Kuziba mahali walipopanga, vigae vizuri, Cement, Rangi, n.k. Kama utaguswa na Ujenzi wa Kaburi hili, na utapenda kuchangia chochote kwa ajili ya Ujenzi wa Kaburi hili, Waweza kutumia Mpesa Namba: 0767 749040 na Kwa walio mbali waweza kutumia Huduma ya Western Union na Maelezo ya siri ya Muamala huo ukatuma kwenda kwenye Email:
Muonekano wa Kaburi kwa ndani
Karibu tushiriki Pamoja katika Kujenga Kaburi la Shujaa wa Imani Tanzania mpendwa wetu Askofu Mosses Kulola.

Waliodaiwa kuchoma kanisa la KKKT Mbagala waachiwa.

Vitu vilivyoharibiwa katika Kanisa la KKKT Mbagala baada ya Kuchomwa Moto
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewaachia huru, Hamed Sekondo na wenzie wanane waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha, kisha kulichoma moto Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Mbagala, baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu.

Uvamizi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema, ambaye alianza kwa kuikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo ya jinai namba 294/2012 ilikuwa imekuja kwa ajili ya mahakama kutoa uamuzi wa ama kuwaona washtakiwa wana kesi ya kujibu au la.

Akisoma uamuzi wake, Lema alisema upande wa Jamhuri katika kuthibitisha kesi yao, ulileta mashahidi 14 na kwamba awali kesi hiyo wakati inafunguliwa mahakamani hapo mwaka jana, ilikuwa na jumla ya washtakiwa 10.

Alisema kuwa hivi karibuni mshtakawa mmoja, Ramadhan Mbulu, alifariki dunia na hivyo kufanya kesi hiyo kubakiwa na washtakiwa tisa ambao kwa kipindi chote walikuwa wakiishi gerezani kwa sababu kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha lililokuwa likiwakabili halina dhamana.
Namna vitu vilivyokuwa vimeharibika
Washtakiwa hao walikuwa wakitetewa na wakili wa kujitegemea, Yahya Njama.

“Baada ya kusikiliza na kuchambua ushahidi na vielelezo vilivyotolewa na upande wa Jamhuri, mahakama hii imefikia uamuzi wa kuwaona washtakiwa wote hawana kesi ya kujibu, hivyo inawaachilia huru kwa sababu upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi yake,” alisema.

Lema aliongeza kuwa ushahidi wote walioutoa ni dhaifu na umeshindwa kuishawishi mahakama iwaone washtakiwa wana kesi ya kujibu.

Upande wa Jamhuri ulikuwa ukiwakilishwa na Wakili Mwandamizi, Tumain Kweka na Inspekta wa Polisi, Hamis Saidi.

Mwaka jana eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam lilikumbwa na vurugu kubwa zilizodaiwa kufanywa na baadhi ya waumini wa Kiislamu, ambao walikuwa wakipinga dini yao kudhalilishwa kwa kukojolewa kitabu cha Kurani, hatua iliyosababisha kuchoma moto makanisa.

- Tanzania Daima -

Thursday, October 17, 2013

Happy Birthday Adela Mwampamba.

Adela akiwa Studio
Leo ni birthday ya Adela Mwampamba ambaye ni Mtangazaji wa Kituo cha Redio ya Kikristo ya HHC ALIVE FM(91.9Mhz) ya Jijini Mwanza.

Adela ni Mtangazaji wa Kipindi cha Mid Day Melody na Alive Xpress, vipindi vinavyoruka Kupitia HHC ALIVE FM kila Jumatatu mpaka Ijumaa.
Adela akiwa katika studio za Hhc Alive Fm
Mtandao huu unamtakia Baraka tele na Mafanikio Katika Maisha yake yote.

Revival Flames Campus Night ndani ya SAUT - Mwanza.

Wednesday, October 16, 2013

Rose Muhando ashindwa kuhudhuria Tamasha la uimbaji Masasi.

SAM_0540
Askofu Oscar Mnung'a akitoa Tamko la Watu kurudishiwa Pesa zao baada ya Rose Muhando kushindwa kufika Viwanja vya Boma, Masasi
Katika hali isiyo ya kawaida, Madai mbalimbali ya kutokuhudhuria Matamasha yamezidi kumkumba Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Rose Muhando baada ya Mwimbaji huyo kutokuhudhuria Tamasha lililoandaliwa na Umoja na Akina Mama Wakikristo Masasi, Tamasha lililokuwa na lengo la Kukusanya Pesa kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Watoto Yatima huko Masasi.

Habari hiyo imeandikwa leo na Mtandao wa Lindi Yetu, huku kutokuhudhuria kwa Rose Muhando katika Tamasha hilo kukitajwa kuleta tafrani kwa Mashabiki waliokuwa tayari washachangia Tamasha hilo, huku Waandaaji wa Tamasha hilo wakilazimika kurudisha Pesa hizo kufutia hakikisho lililotolewa na Meneja wa Mwimbaji huyo Bw. Nathan Wami.
SAM_0517
Baadhi ya Mashabiki waliofika Viwanjani hapo kushuhudia Tamasha hilo
Mch. Carlos Raphael Marcus ambaye ni Makamu Askofu Dayosisi ya Masasi amesema kuwa, Wao walishakamilisha Malipo ya Tshs. Millioni 4 ambazo walilipa kwa Awamu 2, na Stakabadhi wanazo kuhakikisha walifanya hivyo, na ilivyotokea hivyo walimtafuta Meneja wa Rose Muhando Bw. Nathan ambaye aliwaomba radhi waandaje na kuomba arudishe Pesa hizo.

Kufuatia hali hiyo ya kutokutokea kwa Rose Muhando katika Viwanja vya Boma Masasi, Viongozi wa Dini akiwemo Askofu Oscar Mnung'a wa Dayosisi ya Kanisa Anglican Newala walilazimika kutoa Tamko la Mashabiki walioingia Uwanjani hapo kurudishiwa Pesa zao, zoezi lililomalizika kwa Amani licha ya Mashabiki wengi kusikitishwa na Kitendo hicho.