Advertise Here

Wednesday, October 31, 2012

Boko Haram waua waumini 7 wa Kanisa Katoliki Nchini Nigeria.

http://www.ibn-tv.com/wp-content/uploads/2012/10/Nigeria5.jpg
Mji wa Kaduna Nchini Nigeria
 TAKRIBAN watu saba wameuawa nchini Nigeria na wengine wengi wakijeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga katika kanisa la kikatoliki Kaskazini mwa Nigeria.

Maafisa wanasema kuwa gari lililokuwa limebeba mabomu liliingia katika kanisa hilo na kulipua mabomu huku athari zake zikitoboa shimo katika paa la kanisa hilo.

Shambulio hilo lilitokea mjini Kaduna, eneo ambalo limekuwa likilengwa sana na wapiganaji wa Boko Haram kwa mashambulizi katika siku za hivi karibuni.

Rais Goodluck Jonathan ameahidi kongeza juhudi za kupambana na ugaidi na vurugu nchini humo. Aidha Rais Goodluck alitaja shambulizi hilo kama kitu kisicho kubalika na ambacho kinatishia usalama na uthabiti wa nchi hiyo.

Mwandishi wa BBC mjini huko aliarifu kuwa shambulio hilo lilitokana na bomu lilotegwa kwenye gari lililopuliwa na mtu aliyejitoa mhanga na kugonga gari hilo kwenye ukuta wa kanisa.

Anasema uharibifu mkubwa ulitokea ndani ya jengo na kwamba mapaa ya maduka na nyumba za karibu yaling’oka.

Afisa mmoja wa kanisa hilo alisema watu kama wanne waliuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Kumetokea mashambulio kadha ya kidini katika jimbo hilo, mengi yamefanywa na kundi la wapiganaji wa kiislamu, Boko Haram.

Tuesday, October 30, 2012

Video Shooting ya Album ya "U Mwema Rafiki" ya Noel Mlabwa, Felix Mshama, na Barnabas Shija.

Papaa Noel Mlabwa(Wa Kwanza Mbele), Felix Mshama(Nyuma Kushoto) na Barnabas Shija(Nyuma Kulia)
"U MWEMA Rafiki" ndiyo project inayoendelea hivi sasa chini ya Noel Mlabwa(Papaa), Felix Mshama, na Barnabas Shija. Project hii ni ya Utengenezaji wa Album ya Audio na Video kwa Pamoja.

Jana zilirekodiwa Video za Nyimbo nyingine 3, ambapo Blog hii ilishuhudia zoezi zima la ku'shoot Video hizo. Sasa Tazama Picha hizi ili kujua nini kiliendelea katika zoezi hilo liliochukua muda wa kama Masaa 9 hivi.
Kinye kazini akiwa anaisaka shot moja kali sana

Vijana hawa wote ni Mazao ya Tanzania Fellowsip of Evangerical Students(Tafes) ya Chuo Kikuu cha Mt. Agustino - Mwanza.
 
Video ya Kwanza ya U Mwema ilishatengezwa na Kampuni ya Kinye Media chini ya Video Producer Wynjones a.k.a Kinye, Kampuni ambayo inasimamia utengenezaji wa Video za Nyimbo zote zilizopo kwenye Audio album yao.
Video Producer Wynjones a.k.a Kinye
 Baadhi ya Nyimbo zitakazokuwepo kwenye Video Albam hiyo ni Rafiki, U Mwema, Mungu si Mwanadamu, Amani, Yatima, Utukufu na Cha Kutumaini.
 Kwa Maelezo yao wanasema mpaka kufikia Mwishoni mwa Mwezi Novemba, Audio na Video Albam zote zitakuwa tayari, na zitaanza kupatikana katika maeneo ambayo watayataja pindi Albam hizo zikikamilika.
Cameraman Julius Mahela akijaribu kupata Closeup Shot ya Felix
 Hii ndiyo Video ya wimbo wa U Mwema ya Noel, Felix na Barnabas iliyofanywa na Kinye Media

Sunday, October 28, 2012

Mwanza Gospel Team yawachakaza Vijana wa Gilgal kwa Ushindi wa Goli 2-1.

Kikosi cha Mwanza Gospel Team
 JANA katika Viwanja vya Kanisa la Baptist Jijini Mwanza, ulifanyika mpambano mkali wa kupimana nguvu kati ya Mwanza Gospel Team na Vijana wa Kanisa la Gilgal.
Kikosi cha Vijana wa Kanisa la Gilgal
Vijana wa Kanisa la Gilgal ndio waliokuwa wa Kwanza kuzifumania nyavu za Mwanza Gospel Team katika dakika ya 27 ya kipindi cha Kwanza. Matokeo yalibaki hivyo mpaka kuisha kwa Kipindi cha Kwanza.
Mechi ikiendelea
Kipindi cha Pili kilikuwa cha tofauti kidogo kwani Mwanza Gospel Team walifanikiwa kupata goli la kusawazisha katika dakika ya 68. Hii ni baada ya Kocha kufanya mabadiliko katika safu ya ushambuliaji.
Benchi la Ufundi la Mwanza Gospel Team
 Dakika ya 73 Mwanza Gospel Team ilifanikiwa kupata Goli lake la Pili na kufanya Matokeo yawe Goli 2 kwa 1.

Mashambulizi yakizidi kwenye Ngome ya Vijana wa Kanisa la Gilgal
Mashabiki nao hawakuachwa nyuma, walikuwa makini sana kufuatilia mpira mwanzo hadi mwisho.
Mashabiki
 Na kila goli lilipokuwa likiingia nyavuni, Mashabiki nao morali ikawa inapanda.
Mashabiki wakishangilia
 Ilipokuwa ikitokea foward kukosa goli, mambo yalikuwa hivi.....
Mashabiki wa Gilgal wakishangaa baada ya foward yao kukosa goli la wazi kabisa
Huyu ni moja ya Beki machachari sana wa Mwanza Gospel Team
Yusuph Magupa baada ya kutoka Uwanjani
 Zuli a.k.a Mwarabu, ndiye kocha aliyehakikisha Mwanza Gospel Team inapata Ushindi. Team hii inaundwa na Watangazaji wa Radio za Kikristo za Jijini Mwanza pamoja na Waimbaji wa Nyimbo za Injili wa Jijini Mwanza.
Kocha wa Mwanza Gospel Team, Zuli a.k.a Mwarabu
 President Maganga James Gwesaga toka Living Water Fm(103.3Mhz), ndiye Team Captain wa Mwanza Gospel Team. Baadhi ya wachezaji wengine kutoka Radio za Kikristo za Jijini Mwanza ni kama Joshua Dede na Jackson(Kwa Neema Fm), Fabian Fanuel(Living Water Fm), Adolph Nzwalla, Sowane Emmanuel, na Erasto Juma(HHC Alive Fm).
Maganga James Gwensaga
Mpaka mwisho wa Mechi unafika, Mwanza Gospel Team waliibuka kidedea kwa kuwafunga Vijana wa Kanisa la Gilgal Magoli 2 kwa 1.

Saturday, October 27, 2012

T.B Joshua: Don't Give Up.

Semina Maalum ya Mabinti Jijini Mwanza.

KANISA la New Vine International kupitia New Vine International Ministries wanakuletea Semina Maalum kwa Ajili ya Mabinti iliyopewa Jina la Ladies Evening.

Semina hiyo itafanyika Jumapili ya Kesho yaani Octoba 28, 2012 kuanzia Saa 9:00 Alasiri - 1:00 Usiku katika Kanisa la New Vine International lililoko maeneo ya Nyegezi, ndani ya Tema Hotel(Ukumbi Mkubwa).

Wanenaji katika Semina hiyo ni Pastor Goodluck Kyara(Rais wa New Vine International Ministries) na Lucy Ikachoi(Mhasibu wa Constech Co. Ltd).

Hakuna Kiingilio, na Mabinti wote wa Jijini Mwanza Mnakaribishwa sana.

- Vaa Upendeze -

Friday, October 26, 2012

Kesi ya DECI, Mch. Mtares akiri BOT iliwakataza kupokea fedha.

Viongozi wa DECI wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Wa pili kushoto ni Mch. Jackson Mtares
MKURUGENZI wa Taasisi ya Kusimamia na Kuendesha Upatu (DECI), Mchungaji Jackson Mtares amekiri kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) iliwakataza kupokea fedha kutoka kwa mwanachama yeyote wa taaasisi hiyo.

Mtares alieleza hayo juzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati akitoa ushahidi katika kesi ya kuendesha shughuli za upatu bila kibali inayomkabili pamoja na wakurugenzi wenzake wanne.

Akihojiwa na Wakili wa Serikali Prosper Mwangamila, Mtares alidai katika barua ya majibu ya kuomba leseni ya kufanya shughuli za taasisi hiyo, BOT iliwatakaza kupokea fedha kutoka kwa mwanachama yeyote iwe kwa hiari au kwa lazima.

Hata hivyo alipoendelea kuhojiwa na kupewa barua hiyo ambayo imepokelewa mahakamani hapo kama kielelezo cha upande wa mashitaka, Mtares alidai kuwa Mkurugenzi mwenziye ambaye pia ni mshitakiwa ndiye atakayetoa maelezo zaidi.

Awali Mtares aliwasilisha kielelezo ambacho ni barua ya maombi waliyoandika kwa Gavana wa Benki Kuu (BOT) kuomba leseni ya kufanya shughuli za taasisi ambazo ni kusaidia watu wenye kipato cha chini kujikimu kimaisha.

Akiongozwa na Wakili wake wa utetezi Hudson Ndusyepo, Mtares alidai hakuhusika kupokea fedha wala kutoa risiti kwa wanachama na hata katika ushahidi uliotolewa mahakamani na upande wa mashitaka hakuna shahidi aliyedai yeye alipokea fedha.

Mtares aliendelea kudai kuwa,  Benki ya Afrika (BOA) ilikataa kuhifadhi fedha za taasisi hiyo hivyo walizihamishia katika akaunti ya kanisa lake la Jesus Christ  deliverance iliyopo katika Benki ya Wananchi Dar es salaam (DCB) ambayo ilikutwa na zaidi ya Sh bilioni 1.3 baada ya shughuli za Deci kusimama.

Alipoulizwa sababu za benki hiyo kukataa kuhifadhi fedha hizo alidai hajui bali walipewa taarifa kuwa wanatakiwa watoe fedha hizo haraka ndipo bodi ya wakurugenzi ilipoamua fedha hizo ziwekwe kwenye akaunti ya kanisa lake.

Aliendelea kudai kuwa wanachama walikuwa wanalipa kiingilio cha Sh 30,000 na baadaye wanaweka fedha na kupata uwezeshwaji (riba) ya asilimia 150 ya fedha ambayo mwanachama ameweka.

Alipobanwa kwa maswali na upande wa mashitaka, Mtares alidai fedha za riba  zilitokana na fedha walizokuwa wanaweka wanachama kwasababu Deci ilikuwa haijishughulishi na biashara yeyote zaidi ya kuwasaidia watu wenye kipato cha chini.

Hakimu Stewart Sanga aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 8 mwaka huu, wakatakapoendelea kusikiliza ushahidi wa upande wa utetezi.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Wachungaji wa makanisa tofauti ya Pentecoste ni, Dominic Kigendi, Samuel Mtares, Timotheo Ole Loitingye na  Arbogast Francis.

Wanadaiwa katika tarehe tofauti mwaka  2007 na  Machi 2009 katika Makao Makuu ya Deci, Mabibo Dar es Salaam walikusanya fedha kutoka kwa wananchi  wakiwaahidi kuwa watapata faida ya riba kubwa, katika mpango huo waliouita kupanda na kuvuna pia walifanya shughuli hiyo bila leseni.

- Flora Mwakasala -

Thursday, October 25, 2012

Ikulu yachemka kwa kuandika pongezi kwa Papa Benedict XVI kwenda Vatican.

Rais Jakaya Kikwete
KWANZA nianze kwa kuwashukuru watu walioleta thread ya Ikulu ikionyesha barua iliyoandikwa kwenda Vatican kumpongeza Pope Benedict kwa kile Ikulu yetu ilichokiita {Inauguration of the Pontificate of His Holiness Pope John Paul II}.

Thread yenyewe inasomeka hivi;


“His Holiness Pope Benedict XVI,

Vatican City,


HOLY SEE.


Your Holiness,


On behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, and on my own behalf, it gives me great pleasure to congratulate you most sincerely on the occasion of the Inauguration of the Pontificate of His Holiness Pope John Paul II.


Tanzania and the Holy See enjoy good bilateral relations. Over the years we have worked closely. The celebration of your country’s National Day offers me yet another opportunity to reaffirm our commitment to continue working with you in further consolidating and strengthening the ties of friendship and cooperation that exist between us.

 

Please accept, Your Holiness, my best wishes for your personal good health, prosperity and many more years of service to the Church”.

ISSUED BY:
MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION,
DAR ES SALAAM.
22ND OCTOBER, 2012

Thread hii inapatikana HAPA
 

Kwa tunaojua kwanza nimeshtushwa na headline. Baada ya kushtushwa na headline nikashawishika nisome details zaidi nikiamini nilichokiona nitakuta kimerekebishwa ndani ya maelezo.

Narudia, baada ya kusoma barua yote kwenda Vatican kwa Papa, nikaridhika kabisa haya ni makosa yanayostahili kurekebishwa, na Jamii Forum kumejaa wataalamu wa kuona makosa na kurekebisha. Je! Kosa ni nini hapa kwenye barua hii?


Kulijua kosa inabidi kwanza tuanze kujua terms za Kanisa Katoliki. Neno "Pontificate" linatumika kwa mambo yanayofanywa na Askofu lakini likitajwa peke yake basi linamaanisha Askofu wa Roma yaani Papa.


Hivyo "Pontificate" ni utawala wa Papa. Kwa kiingereza tungesema ni "reign". Pontificate ni kipindi chote cha huyo mtu kuwa Papa yaani tangu siku aliposimikwa kuwa Askofu wa Roma hadi atakapofariki au ku-resign.


Tunajua kwamba Papa huchaguliwa na mkutano wa makardinali uitwao "Conclave". Lakini Papa kama askofu wa jimbo lolote haishii kuchaguliwa tu, bali siku yake ya kwanza ya uaskofu wa askofu au upapa wa Papa (Pontificate) ni siku ile anapokaa kwenye kile kiti cha askofu kwenye Kanisa kuu liitwalo "Cathedral".


Narudia hii ni kwa kila askofu wa Kanisa Katoliki duniani akiwemo Papa. Hivyo "Pontificate" yaani siku ya kwanza ya utawala wa Papa yoyote huanza siku hii.


Narudi kwenye mshangao wangu, ni kwamba niliposoma ungedhani kuwa kuna Papa mpya ambaye upapa wake umeanza (Pontificate) na hivyo Ikulu yetu imetuma salamu za pongezi kwa kuanza upapa huo yaani {
Inauguration of the Pontificate}.

Kibaya zaidi pametamkwa {
Inauguration of the Pontificate of His Holiness Pope John Paul II}, ambapo kwa kiswahili sahihi ni {kuanza kwa Upapa wa John Paul II}.

Haikutakiwa kuandikwa hivi. Je, kilitakiwa ni nini?


Kilichotakiwa ni kuchunguza kwanza ni nini kinaendelea kabla ya kuandika. Kinachoendelea ni kumbukumbu ya kilichotokea miaka 34 yaani Jumapili, October 22, 1978.


Hii ndiyo siku John Paul II alipouanza upapa wake kwa kuendesha misa na kukali kile kiti {Cathedral} kilichomo kwenye Kanisa Kuu lake ambalo linaitwa {
Archbasilica of St. John Lateran}. Najua baadhi, na ikibidi wengi wanaishia kulijua lile {St. Peter's Basilica}.

Lakini Kanisa hasa la upapa ni hili {
St. Peter's Basilica} kama pale D'Salaam lilivyo kanisa la St. Joseph}.

Sasa, kilichotokea wiki hii pale Vatican, kinahusiana na mchakato wa kumtangaza John Paul II awe mtakatifu kwani yeye sasa tayari kikanis ayuko hatua kubwa zaidi kuliko ilivyo kwa Julius Nyerere kwa mchakato huohuo. John Paul II sasa yeye anaitwa "Beata" yaani "Mwenyeheri". Amebakiza ngazi moja tu kutangazwa mtakatifu.


Kutangazwa mtakatifu au mwenyeheri ni hatua moja inayoambatana na kuwekwa kwa siku maalumu ya kumkumbuka mtakatifu huyo. Watakatifu wengi hasa mashahidi wa dini siku yao huwekwa kuwa ni ile waliyokufa kama wale mashahidi wa Uganda. Lakini baadhi si lazima iwe siku hiyo.


Pope JOhn II alitangazwa mwaka jana kuwa "Beata", na hivyo kukawa na debate kuwa je, siku yake iwe lini. Ndipo kabla ya kumtangaza Vatican ikaamua kwamba siku yake iwe ni siku alipouanza upapa wake yaani October 22.


Hivyo, October 22, ni maalum kwa Beata John Paul II kama ilivyo siku ya mtakatifu au mwenyeheri yoyote unayemjua.


Hivyo, kilichofanyia juzi, zutio wake wa kwanza kabisa ni makanisa duniani kuadhimisha kwa mara ya pili siku ya Mwenyeheri John Paul II.


Lakini tukio hili limegongana na mambo kadhaa ambako maaskofu wengi akiwemo Polycarp Pengo wako Vatican kwa shughuli iliyoanza wiki mbili zilizopita iitwayo Synod. Hivyo, hilo limeongeza populality ya jambo hili kuonekana ni special kwa kiasi fulani.


Haishangazi kuwepo kwa meseji ionyeshayo {
Inauguration of the Pontificate}. Lakini kama umeshasoma hadi hapa utakuwa umeelewa ni kwamba Vatican haina mpango wa kusherehekea siku ya Papa ambaye tayari ameshakua lakini cha msingi dunia kukumbushwa siku ya "Uenyeheri" wake na ikitokea akatangazwa utakatifu itakuwa ni siku ya "Utakatifu" wake kuadhimishwa makanisani.

Sasa, barua ya Ikulu ambayo imetolewa na Wizara ya mambo ya nje inaonyesha kama kwamba ni uzinduzi wa Upapa, tena wa Papa aliyekwisha kufa.


Nafahamu Salva Rweyemam ni mkatoliki lakini nafahamu Bernard Membe si tu kwamba ni mkatoliki tu bali alipita seminari na meseji kama hii angeweza kugundua hiki ninachoeleza.


Nawatakia usomaji mwema.

- Jamii Forum -

Wednesday, October 24, 2012

Dotnata Posh sasa Kufungua Kanisa.

Dotnata Posh
MWIGIZAJI na aliyewahi kuwa Mwanamuziki Dotnata Posh, amesema kwa sasa ameaokoka kabisa na kuamua kufungua kanisa kubwa lengo likiwa kuwashawishi wasanii wenzake kuachana na  maasi na hatimaye kumrudia Mungu.

Dotnata ambaye alianza kwa kufafanua jina lake, alisema watu wengi wamezoea kumwamwita jina hilo bila kujua msingi wake, kwamba yeye jina lake ni Doto na ameunganisha na jina lake la ubatizo Illuminate ambapo akachukuwa jina la kwanza la Dot na kuunganisha jina la mwisho na  nate na kupata Dotnata.
T.B Joshua

Safari yake ya Nigeria
Dotnata anasema aliamua kwenda Nigeria  kwa Mtume T.B Joshua ambaye ni maarufu sana Afrika na Dunia nzima, ili kwenda kuchukua baraka kwaajili ya kuanzisha Kanisa hilo.

Alisema baada ya kurudi kutoka Nigeria na kupata baraka hizo za kufungua kanisa, hivi sasa anasomea masomo ya Biblia ili baadae aje kuwa  Mchungaji. Kwasasa yeye ni Mama wa Kanisa. Aidha aliongeza kwa kusema kuwa, kwa sasa kanisa lake litakuwa na wahubiri kutoka Nchi mbalimbali na baada ya hapo ataanza kutoa elimu kwa wasanii waweze kuokoka ili kumrudia Mungu.

Dotnata pia amesema kwa sasa hawezi kumlaumu msanii ambaye anafanya mambo ya ajabu ajabu kwakuwa anaamini ni ujana unamsumbua na ukifika muda atabadilika. Alizidi kusisitiza kuwa katika Kanisa lake anategemea pia kuwachukua wasanii Ray C na
Asha Madinda, ambao nao wameokoka.

Mwisho alimalizia kwa kusema Kanisa hilo kwa hivi sasa lipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili, ingwa pia limeruhusiwa kuendelea na kazi zake za ibada.


- Bongo Unit -

Tuesday, October 23, 2012

T.B Joshua atabiri kutokea kwa Mafuriko Nchini Nigeria.

T.B Joshua
MTUME T.B Joshua kutoka Kanisa la Synagogue Church of All Nations(SCOAN) la Nchini Nigeria, ametabiri kutokea kwa mvua kali zitakazosababisha Mafuriko nchini humo.

Akizungumza katika Ibada ya Jumapili iliyopita na kurushwa live na Kituo cha luninga cha Emmanuel Tv kinachomilikiwa na Kanisa hilo, T.B Joshua alisema "It is always sensitive to talk about our country. Before you know it, they will say that is another thing. May God forgive us."

Amesema kuwa mvua hizo zitasababisha mafuriko makubwa sana ambayo yataleta uharibifu katika baadhi ya maeneo ya Nigeria. Baadhi ya watu watapoteza Nyumba zao na wengine watakufa kutokana na Mafuriko hayo.

Amewaomba wananchi wa Nigeria kuomba sana kwa ajili ya Jambo hilo ili Mungu aepushe Mafuriko hayo kwani Viongozi wa Nchi hiyo wanapuuzia Jambo hilo.

Tazama Video hii kuona alichokizungumza T.B Joshua katika Ibada hiyo...

Sunday, October 21, 2012

Butimba Gospel Fellowship waja na Album ya "Halleluya".


Sowane Emmanuel akiwa anafanya Mahojiano na Wanakwaya wa Butimba Gospel Fellowship katika Kipindi cha Gospel Sound
HAWA ndiyo wanakwaya wa Butimba Gospel Fellowship kutoka Chuo cha Ualimu cha Butimba Teachers Training College kilichopo maeneo ya Butimba, Jijini Mwanza.

Mwalimu wa Kundi hili ni Bahati Kihayile kutoka Kihayile Group. Na kwasasa Kwaya hii ina Album Moja ijulikanayo kama Halleluyah ambayo bado haijaanza kusambazwa rasmi.
Wanakwaya wa Butimba Gospel Fellowship wakiwa Studio za HHC Alive Fm ya Jijini Mwanza. Wa kwanza Kushoto ni Bahati Kihayile(Mwalimu wa Kwaya)
Waliyasema hayo wakiwa katika Kipindi cha Gospel Sound kinachoruka kila Siku ya Jumamosi kuanzia Saa 8:00 - 10:00 Jioni, kupitia Radio ya Kikristo ya HHC Alive Fm(91.9Mhz) ya Jijini Mwanza.

Album hiyo ina Jumla ya Nyimbo 10, na baadhi ya Nyimbo hizo ni kama Injili, It is Good, Halleluya, Tujipe Moyo na Nitayainua. Malengo yao ni Kununua vifaa vya Muziki vitakavyowawezesha kuimba live katika Matamasha na Huduma Mbalimbali.

Saturday, October 20, 2012

Hiki ndicho kilichofanyika Jana katika Campus Night ya Tafes Saut.

USIKU wa kuamkia leo, ulikuwa ni Usiku wa Praise & Worship ulioandaliwa na Tanzania Fellowship of Evangerical Students(TAFES) tawi la Chuo Kikuu cha Mt. Augustino kilichopo Jijini Mwanza wakishirikiana na Radio ya Kikristo ya Jijini Mwanza HHC Alive Fm inayosikika kupitia Masafa ya 91.9Mhz na Online kupitia www.hhcalivefm.org.

Kwaya na Band mbalimbali zilihudumu wakiwemo wenyeji Tafes Saut Praise & Worship Team, Revival Mission Band(Wana wa Uzao wa Daudi), Casfeta Tayomi, Kingdom Worship, Huima Saut, Tafes Choir, Kihayile Group na wengine wengi.

Shughuli ilianza mida kama ya Saa 3 Usiku, huku Mnenaji katika Ibada hii maalum akiwa ni bishop Eugine Murisa kutoka Kanisa la High Way of Holiness Cathedral lililopo maeneo ya Ilemela Kanisani, Njiaa Kuu ya Kuelekea Airport.

Sasa tuambatane pamoja katika kutazama picha hizi zifuatazo ili upate picha halisi ya jinsi Tamasha hilo lilivyokuwa.........
Kijana wa Yesu Felix Mshama
Blogger Baraka Samson (Mjap Inc Blog)
Noel Mlabwa kwenye Drums
Kijana Sephon kwenye Keyboard
Yesu Juuuuuuuu..............! (Tafes Praise Team)
Wapi Vick Bongeeeeeee! a.k.a Photogenic
Pipooooooooooooooooooo............!
Kweli kwa Yesu ni Raha tupu!
Kingdom Worship on Stage
Pastor Goodluck Kyala wa Kanisa la New Vine International Church akiombea Matoleo
Wana wa Uzao wa Daudi waite Revival Mission Band Wazee wa Roboko
Bishop Eugine Murisa akitoa Neno
Maombi pia yalikuwepo
Sala ya Toba ikiendelea
Hawa ni Huima Saut
Bugando Praise & Worship Team
Kukosea Step ilikuwa ni Kosa la Jinai
Wana wa Kihayile a.k.a Kihayile Group
 Daima Mungu atukuzwe kwa Ukuu wake!