Advertise Here

Saturday, June 15, 2013

Pastor Steven Wambura, James Kalekwa, Fred Msungu na Mc Pilipili wafanyika Baraka kwenye Kingdom Exploits.

Usiku wa Kuamkia leo katika Chuo cha Mt. Agustino-Mwanza, kulikuwa na Event iliyopewa Jina la Kingdom Exploits, iliyoandaliwa maalum kabisa kwa ajili ya Vijana waliopo chuoni hapo. Tukio hili lilianza Mida ya Saa 2:00 Usiku hadi Saa 5:00 Usiku huku Wanenaji wakiwa ni Bw. James Kalekwa-Mwanza, Fred Msungu-Dar na Mch. Steven Wambura-Dar.

Mchekeshaji wa Kimataifa toka Tanzania, Dar es salaam Bw. Emmanuel Mathias a.k.a Mc Pilipili alikuwepo Ukumbini hapo kuvunja mbavu za Wanafunzi wa Chuo hicho. Shughuli ilifanyika katika Ukumbi wa M10, na Praise Team iliyoundwa na Vijana wa Tafes, Casfeta, Huima na Uscf iliuongoza Umati wa Vijana waliokuwepo katika kuusogelea Uso wa Mungu.

Sasa tazama picha hizi uone jinsi Mambo yalivyokuwa chini ya Mc wa Event Bw. Barnabas Shija.
Mc wa Event Bw. Barnabas Shija
Wanafunzi waliohudhuria
Presentation ya Bw. James Kalekwa
Huyu jamaa hata kwenye Uimbaji yuko vizuri. Ni Fred Msungu

Wednesday, June 12, 2013

Leo ni Birthday ya Tb Joshua. Atimiza Miaka 50.

Tb Joshua
Jina lake kamili ni Temitope Balogun Joshua, jina alilopewa na Wazazi wake baada ya kuzaliwa. Anajulikana sana kama Tb Joshua. Alizaliwa mnamo June 12, 1963. Leo ametimiza Umri wa Miaka 50 toka Kuzaliwa kwake.

Kwa kawaida na ilivyozoeleka ni kwamba, Mama wajawazito hujifungua watoto baada ya Miezi 9 toka wapate ujauzito. Lakini kwa Mtumishi wa Mungu “Wise Man” Tb Joshua, haikuwa hivyo kwani yeye alizaliwa baada ya Miezi 15 toka Mama yake Mzazi apate ujauzito wake.
 
Na baada ya Miezi hiyo 14 (yaani Mwaka 1 na Miezi 2) kutimia, ndipo alipozaliwa mnamo June 12, 1963 katika Mji wa Arigidi, nchini Nigeria. Kwa sasa Mtumishi huyu anaishi katika Mji wa Lagos, Nigeria.

Tb Joshua ni Kiongozi na Mwanzilishi wa Huduma ya “The Synagogue, Church of All Nations(SCOAN)” inayoendesha Kituo cha Luninga kijulikanacho kama Emmanuel TV, kituo kinachopatikana kupitia satelaiti na kwenye Mtandao wa Internet.

Tb Joshua amekuwa akitoa Misaada mbalimbali kwa watu wasiojiweza, wajane, yatima, walemavu, kuwalipia ada wanafunzi mbalimbali, nk. Kwa kutambua hili, serikali ya Nigeria imekuwa ikimpa tuzo mbalimbali kwa ajili ya kutambua mchango wake katika ustawi wa hali ya kimaisha ya wananchi wa Nigeria.
Tb Joshua akitoa Msaada wa Chakula kwa Wazee wasiojiweza huko Nigeria
Katika hili la Msaada, amekuwa akisema; “Ili ubarikiwe, inatakiwa utumie sehemu kubwa ya Mali yako kwa ajili ya wenye uhitaji wa msaada(wajane, yatima, walemavu, nk), na utumie sehemu ndogo kwa ajili yako”.

Katika Kanisa analohudumu Tb Joshua nchini Nigeria, linahudumia takribani Waumini zaidi ya 15,000 katika Ibada za Kila Jumapili ambazo huwa zinarushwa moja kwa moja na Kituo cha Luninga cha “emmanuel tv”.

Monday, June 10, 2013

Watu zaidi ya 300 wahudhuria Tamasha la Kusifu na Kuabudu la "Higher Praises".

Jana katika Kanisa la New Vine Christian Centre(NVCC) lililopo Nyegezi, Mwanza(Tema Hotel-Ukumbi Mkubwa) chini ya Mchungaji Kiongozi Pastor Goodluck Kyara, kulikuwa na Tamasha Kubwa la Kusifu na Kuabudu liliyopewa Jina la "Higher Praises". Tamasha hilo lililoanza Saa 9:00 Alasiri lilimalizika Saa 1:00 Jioni na vikundi mbalimbali vya Kusifu na Kuabudu vilihudhuria Tamasha hilo ili kuwasogeza Watu katika Uso wa Mungu.

NVCC Praise & Worship Team ndo walikuwa Waandaaji wa Event hiyo na Watu zaidi ya Mia 3 walihudhuria Tamasha hilo la Kusifu na Kuabudu. Karibu kutazama Picha hizi za Jinsi Tukio lilivyokuwa........
NVCC Praise Team ikiwa Back Stage

NVCC Gentlemen wakiwa Back Stage

NVCC Ladies wakiwa Back Stage

CBCI On Stage

Baadhi ya Watu waliohudhuria Ibada hiyo

Tafes Saut On Stage

Halleluyah!!!

Uweponi Mwake

Mtu wa Mungu, Mc wa Event Mr. Eliud Mwasenga

NVCC Praise Team

Here is Tontoo. "Moja, Mbili, Tatu, Kwa Jina la Yesu, Tunakanyaga Shetaniiiiiiiiiiiii..........!"

NVCC Praise Team ikihudumu

Sowane Emmanuel kwenye Tumba

Team ya Wapiga Vyombo, Boaz(Kushoto) Adolph(Katikati) na Jema(Kulia)

Mtoto wa Bishop Irene Nzwalla, Muite Adolph Robert Nzwalla

Pastor Goodluck Kyara akisifu

NVCC Praise Team On Stage

Mikono Juu, Mikono Juu. Alama ya Ushindi.................

Kwa YESU kuna Raha Jamani

Mama Praise wa Tafes Saut, Muite Aneth

Kutoka MICC Praise Team, Huyu ni Juma Luchele. Weka mbali na Mic

Brother James Kalekwa(Kushoto) akiwa na Hilly

Team Boaz On Stage
Pastor Goodluck Kyara(Kulia)

Man of God Boaz

'Mungu wa Eliya aaaah, shusha Motooooo eeeh..............!"

Ilifika Mahala hadi Ushers(Wahudumu: Wenye nguo nyeusi Kulia) Wakaacha kazi zao na Kuamua kujiunga na Wengine

Hapo hakuna kumkanyaga Mwenzako

Utukufu Kwa Mungu

Noel(Kushoto) na David(Kulia)

Here is Man Adolph Robert Nzwalla

Wacha Weeeeeeeeeeeeeeee...........!!!

Wapi Mama Praise Aneth(Wa Katikati)

Alipoona wenzake wanafaidi, Mc wa Event Mr. Eliud(Kulia) nae akaamua kuachia Mic na Kuanza kucheza

Pastor Goodluck Kyara akifanya Maombi ya Kufunga Ibada hiyo

= Utukufu Urudi Kwake Aliye Mkuu kupita Wote =

Saturday, June 1, 2013

New Vine Christian Centre yaandaa Tamasha la Kusifu na Kuabudu.

Kanisa la New Vine Christian Centre lililopo Nyegezi Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Kiongozi Pastor Goodluck Kyara, limeandaa Tamasha la kusifu na Kuabudu lijulikanalo kama "Higher Praises" litakalofanyika June 9, 2013 katika Ukumbi Mkubwa wa Tema Hotel uliopo Nyegezi, Jijini Mwanza.

Tamasha hilo litaanza Saa 8:00 Mchana na kumalizika Saa 12:30 jioni, huku New Vine Praise & Worship Team ikiongoza Sifa na Kuabudu. Vikundi Mbalimbali vya Kusifu na Kuabudu pia Vimealikwa kama vile BCIC na MICC Praise & Worship Team.

Kwa Maelezo Zaidi waweza Kupiga Simu Namba: 0754 435951, 0712 113305.