Samwel Batenzi maarufu sana kwa jina la Sam Batenzi,
ni Mwimbaji Chipukizi wa Nyimbo za Injili anayekuja kwa kasi ya Ajabu
katika tasnia ya Muziki wa Injili Tanzania, kutokana na Uimbaji wake un
avyowabariki watu wa Mungu. Kwa mara ya Kwanza, nilikutana na Sam Jijini
Mwanza katika kituo cha Kazi yaani HHC ALIVE FM (91.9Mhz), na ndipo hapo nilipopata shauku ya Kumfahamu zaidi.
HISTORIA YAKE KIMAISHA
Sam alizaliwa miaka 25 iliyopita katika Mkoa wa Mwanza, katika familia
ya kikuhani ya Bishop David Batenzi na Mama Batenzi. Sam ni mtoto wa 3
kati ya watoto 4 wa Askofu Batenzi, na kabila lake ni Mnyamwezi kwa
Upande wa Baba, na Msukuma kwa Upande wa Mama.
HISTORIA YAKE KIMUZIKI
Sam alianza kujishughulisha na Maswala ya Kimuziki Mwaka 2000, lakini
katika kujifunza vyombo vya Muziki huko Mkoani Mwanza. Na alianza rasmi
uimbaji Mwaka 2004 huko Tabora katika shule moja iliyojulikana kama
Umoja Secondary School.
Nilipotaka kufahamu ni Kwanini aliamua kuimba Muziki wa Injili na Si
aina Nyingine ya Muziki, Sam alisema; “Nimeamua kumtumikia Mungu katika
Uimbaji wa Muziki wa Injili kwa sababu Muziki wa Injili ndio muziki
ambao umekuwa ukigusa maisha yangu kwa aina moja au nyingine, lakini
naweza sema pia nilizaliwa katika familia ya kikristo na kukulia katika
Malezi ya Kikristo.Na pia nilipompokea kristo kama mwokozi wa maisha
yangu, ndipo nilipogundua nini Mungu amenizawadia, nami nikatumia zawadi
hiyo kufanya kazi yake.”
Vipi kuhusu vikundi/kwaya ambazo Sam ameimbia?
Hapa Sam anasema; “Nilipokuwa shule niliimbia kikundi kimoja
kilijulikana kama LPP (Long Pray Praise) ambacho naweza sema ndo
waliendeleza kile Mungu ameweka ndani yangu, lakina pia nimewahi imbia
Dar es Salaam Gospel Choir DGC ya Dar, na nimewahi kuwa member kwa muda
katika kundi moja la kusifu na kuabudu linajulikana kama New Wine la
Dar.
Nini ambacho Sam anafanya kwa Sasa?
“Kwasasa nimekuwa nafanya kazi za Uimbaji na vikundi ambavyo vimekuwa
vinatengenezwa kwa muda kwa ajili ya kazi fulani tu baadae kinaisha
baada ya hiyo kazi.
Kuhusu aina ya Muziki ambao Sam anaupenda sana ni African Music kama
Zouk,Rhumba,Qwato,Sebene,Tradition music, lakini pia napenda pia Black
Gospel,Jazz,RnB,Soul, na Soft rock.
Ni Mwimbaji gani wa Gospel unaempenda zaidi kwa Hapa Nyumbani?
“Mwimbaji wa Gospel kwa hapa nyumbani naweza sema Jackson Benty, Minza
na John Lisu zaidi ya hapo labda vikundi kama Next Level, Sowers, Holy
of Holies, Calvary Band, UGM. Ila napenda zaidi makundi.
Vipi ulishawahi kurekodi Wimbo wowote?
“Nilipoanza muziki tulirekodi na hilo kundi ambalo nilijiunga nalo la
LPP, mbali ya hapo nimekuwa nafanya na watu tu, ila ndo nimeanza
taratibu za kuandaa album yangu ya kwanza maana sikupenda sana muziki wa
kurekodi studio. Napenda sana muziki wa live, na hata kama ni kurekodi
iwe live on stage maana naamini ndo unakuwa na mguso wa aina yake na
kuwa karibu na Mungu at a particular time”
Mbali ya Uimbaji, ni Kazi gani Nyingine unayojishughulisha nayo?
“Mbali ya Uimbaji, nafanya kazi ya Video Shooting pamoja na Editing. Maana nda Taaluma yangu hiyo.”
Vipi umeshajiunga na Chama cha Waimbaji wa Nyimbo za Injili?
“Kiukweli bado sijajiunga na chama cha waimbaji, maana sikuwa asilimia
zote kwa muziki maana nimekuwa na shughuli zingine hasa za kimasomo
labda kwa sasa ndo naweza kuanza taratibu za kujiunga.”
Ni aina gani ya Muziki unaofanya?
“Mimi nafanya muziki wa asili ya kiafrika ambao nimeupa jina la African
Christian Soul (Afrocso), na hii ni kutokana na kugundua sisi Tanzania
tumebarikiwa na miziki mbalimbali ya asili ambayo ikifanyiwa kazi,
inakuwa mizuri sana badala ya kuanza kucopy nchi za magharibi. Kkwahiyo
huo ndo aina ya muziki ambao mimi naimba katika kumtukuza Mungu.”
Ni vyombo gani vya Muziki unavyoweza kupiga?
“Napiga vyombo mbali kama bass guitar, acoustic guitar, kinanda, solo
guitar na drums kidogo, ila zaidi chombo changu ni Bass guitar.”
Nini Malengo yako ya Baadae?
“Malengo yangu ni kumtukuza Mungu katika anga za kimataifa, na kundi
ambalo nililianzisha mwaka jana kwa jina la “The Psalmists” ambalo hadi
sasa tumeshafanya matamsaha mawili moja lilifanyika Dar 9 – 1 – 2011
katika kanisa la FPCT Kurasini, na la pili Mwanza 8 – 1- 2012 katika
kanisa la FPCT kitangiri pia naanda matamasha mengi zaidi ambayo sasa
hivi yatakuwa na muziki wa asili zaidi ili ku’promote such kind of music
which is much blesses much”
Sasa sikiliza Mahojiano aliyoyafanya Sam Batenzi na Radio France International, April 13, 2013 akiwa na Mwimbaji wa Nyimbo za Injili toka Congo, Nyumba ya Mungu.