Tb Joshua |
Jina lake kamili ni Temitope Balogun Joshua, jina alilopewa na Wazazi wake baada ya kuzaliwa. Anajulikana sana kama Tb Joshua. Alizaliwa mnamo June 12, 1963. Leo ametimiza Umri wa Miaka 50 toka Kuzaliwa kwake.
Kwa kawaida na ilivyozoeleka ni kwamba, Mama wajawazito hujifungua
watoto baada ya Miezi 9 toka wapate ujauzito. Lakini kwa Mtumishi wa
Mungu “Wise Man” Tb Joshua, haikuwa hivyo kwani yeye alizaliwa baada ya
Miezi 15 toka Mama yake Mzazi apate ujauzito wake.
Na baada ya Miezi hiyo 14 (yaani Mwaka 1 na Miezi 2) kutimia, ndipo alipozaliwa mnamo June 12, 1963 katika Mji wa Arigidi, nchini Nigeria. Kwa sasa Mtumishi huyu anaishi katika Mji wa Lagos, Nigeria.
Tb Joshua ni Kiongozi na Mwanzilishi wa Huduma ya “The Synagogue, Church of All Nations(SCOAN)” inayoendesha Kituo cha Luninga kijulikanacho kama Emmanuel TV, kituo kinachopatikana kupitia satelaiti na kwenye Mtandao wa Internet.
Tb Joshua amekuwa akitoa Misaada mbalimbali kwa watu wasiojiweza, wajane, yatima, walemavu, kuwalipia ada wanafunzi mbalimbali, nk. Kwa kutambua hili, serikali ya Nigeria imekuwa ikimpa tuzo mbalimbali kwa ajili ya kutambua mchango wake katika ustawi wa hali ya kimaisha ya wananchi wa Nigeria.
Tb Joshua amekuwa akitoa Misaada mbalimbali kwa watu wasiojiweza, wajane, yatima, walemavu, kuwalipia ada wanafunzi mbalimbali, nk. Kwa kutambua hili, serikali ya Nigeria imekuwa ikimpa tuzo mbalimbali kwa ajili ya kutambua mchango wake katika ustawi wa hali ya kimaisha ya wananchi wa Nigeria.
Tb Joshua akitoa Msaada wa Chakula kwa Wazee wasiojiweza huko Nigeria |
Katika hili la Msaada, amekuwa akisema; “Ili ubarikiwe, inatakiwa
utumie sehemu kubwa ya Mali yako kwa ajili ya wenye uhitaji wa
msaada(wajane, yatima, walemavu, nk), na utumie sehemu ndogo kwa ajili
yako”.
Katika Kanisa analohudumu Tb Joshua nchini Nigeria, linahudumia
takribani Waumini zaidi ya 15,000 katika Ibada za Kila Jumapili ambazo
huwa zinarushwa moja kwa moja na Kituo cha Luninga cha “emmanuel tv”.