Jessica Honore |
Jessica Honore ambaye ni Mtoto wa 6 na wa mwisho kuzaliwa katika familia ya kitumishi amerithi kipaji cha uimbaji toka kwa wazazi wake, kaka pamoja na dada zake. Watoto wa familia yao wengi wamekuwa ni waimbaj na wapiga vyombo vya Muziki.
Jessica alianza uimbaji akiwa na umri wa miaka 6. Alikua akiimba
kwaya ya watoto Kijitonyama Pentecoste, na baadae Mwananyamala Pentecoste. Huko ndiko alikokukuzia huduma iliyokua ndani
yake. Mnamo Mwaka 2005 akiwa darasa la 7 Jeesica akasikia habari za mashindano ya Uimbaji(Gospel Star Search).
Jessica akiwa na baadhi ya Washiriki wa Gosprl Star Search ya Mwaka 2005 |
Jessica anasema "Wakati huo sikuwa katika mazingira ya kuniruhusu
kushiriki shindano hilo, ila kwa msukumo uliokuwa ndani yangu juu ya uimbaji na kwa ruhusa na
ushirikiano wa Mama yangu, niliweza kwenda katika usahili na
kushiriki shindano hilo. Baada ya mchakato mrefu sana, ulio jumusha washiriki toka
mikoa mingine ya tanzania kama mitatu hivi, ndipo nikafanikiwa kuibuka mshindi."
"Hapo
ndipo nilipoanza safari rasmi ya uimbaji. Nilifanikiwa kupata gari na kusomeshwa elimu ya sekondari mpaka kidato
cha 4 kupitia Ushindi ule chini ja usimamizi wa Walezi Ruge Mutahaba na Michael Nkya. Pia Mwaka huo huo wa
2005 nikafanikiwa kutoa track yangu ya kwanza iliyojulikana kama "Mungu Yupo" na ikafanya vyema katika vyombo mbalimbali vya habari, ingawa bado sikuwa tayari
kuingia deep kwenye maswala ya Muziki kwani nilikuwa bado ni Mwanafunzi na nilikua chini ya uongozi ambao haukuhitaji kunipeleka puta, maana waliona nahitaji kukua
kiuimbaji, kielimu na kiakili." Aliongeza Jessica.
Jessica akiwa Studio |
Baadaye akafanikiwa kutoa nyimbo nyingi sana akiwa
bado anasoma, chini ya usimamizi wa Mlezi wake
Rugemalila. Baadhi ya Nyimbo hizo ni kama Sitaogopa, Mtumikie, Sifuni, Sitahofu na nyingine
nyingi ila hakutengeneza album. Mnamo Mwaka 2010 baada ya kumaliza shule Jessica alifanikiwa kutengeneza album ya Tenzi za Rohoni, ila kwa sababu
mbalimbali haikuweza kutoka.
Baada ya kumaliza kidato cha 4, Jessica alitamani sana
kwenda shule ya Uandishi wa Habari(School of Journalisim) ila haikuwezekana kwa kipindi hicho na ndipo akaanza rasmi kazi ya Muziki. Wakati huo alianza kwa kufanya Matangazo
mbalimbali na Jingles pia hasa za Clouds Fm,
na zikapendwa sana na watu. Pia alifanya Matangazo ya Kampuni za simu kama Vodacom na Zantel.
Jessica akiwa katika Utengenezaji wa Video yake ya Napokea |
Jessica anasema " Pia nimekuwa nikiitwa kwenye hafla mbalimbali kuhudumu kama Harusi, Misiba na Sherehe mbalimbali huku nikitumia Keyboard pamoja na Mpigaj aitwae Isaya, na
kwahiyo niliweza endesha Maisha yangu vyema. Nilipendelea pia maswala ya Modeling na Designing na Wakati mwingine nimekuwa nikichora
designs za nguo kwa mitindo mbalimbali."
Jessica alianza jitegemea mwaka 2010, na Mwaka 2011 Emmanuel Mabisa alimfuata na
kumshirikisha swala la Glorious Celebration. Jessica anasema, "Sikusita maana nilikuwa napenda sana kushirikiana na waimbaji wengine ila ilikuwa ni kwa makubaliano ya kua nitapotaka
anza rasmi simamia maono yangu nitatoka Glorious Celebration na kuanza simamia kitu kilicho ndani
yangu. Pia mwaka huo huo nikapata nafasi katika kanisa la Word Alive Center kwa kufundisha Praise Team na kuanza kusali pale baada ya kua Christ Embassy kwa miaka
mitatu.
Jessica akiwa na Glorious Celebration |
Mwaka jana(yaani 2012) Mwezi wa 5 au wa 6 alianza chukua hatua ya Maono
yake huku akiendelea shughurikia album yake aliyokua ameitelekeza
kwa muda mrefu. Jessica anasema ilikua ni changamoto maana alikuja gundua kuwa alikua akua kiuimbaji hivyo ikabidi aanze kuziimba upya Nyimbo za kwenye Album hiyo. Jessica anaendelea kusema kuwa amekuwa na maono ya
muda mredu ya kua na team maalum ya kuhudumu nayo mahali mbalimbali kwa kufanya Live Music, kuwa na shule ya Muziki, pamoja na eneo ambalo watu wanaweza kuwa
wakilitumia katika Kusifu na Kuabudu yaani Cathedral of Worship.
Jessica katika pozi |
"Pia napenda kuwa na studio kubwa ya
muziki na kwa kutambua hilo nikaanza kwa kujitoa kufundisha watu ambao
wamekua wakihitaj msaada wangu. Mwaka jana mwishoni nilifanikiwa
kuanzisha Team yangu kwa kupata mabinti walio kua na vipaji ila walihitaji
uzoefu na mafunzo ya ziada ili kukua na kuimba vizuri. Hivyo nikawafundisha na pia
nikawashirikisha baadhi ya wapigaji wa vyombo akiwemo kaka yangu wa kufuatana John na akakubali na kunisaidia kusimamisha maono yangu."
Mwaka jana
mwishoni nikaanza kuhudumu na mabinti zangu na wakaka wawili niliowafundisha mwenyewe. Baada ya kuona tumefanya vizuri katika tamasha la Holy Bass Guitor lililofanyika pale DPC mwaka jana, nikaamua kuwa serious zaidi na kujikita
kufanya huduma ikue. Kweli huduna ikaanza kukua, watu wa kufanya back up wakaanza
ongezeka pamoja na wapiga vyombo maana wakati huo bado nilikua sijapata
wapigaji maalum wa kuwa nao katika huduma. Ndipo nikawa na msukumo wa
kufanya huduma hii kwa ukamilifu zaidi."
Jessica(aliyekaa) akiwa na baadhi ya waimbaji wake |
"Baadaye nikapata msukumo wa kuandaa
tamasha la uzinduzi wa album yangu ya kwanza ili kuelezea maono yangu na
kutambulisha team yangu nitakayokuwa nikihudumu nayo kwa jina la THE
JESSICA MUSIC. Na kwa mwaka huu nikaanza mikakati mingi kwa msaada wa Pastor mmoja
toka Nchini Zambia Pastor John Mumba aliyeguswa na huduma yangu na kuamua kunisaidia kupanua ufahamu
wangu kufikia ndoto zangu, na akawa
bega kwa bega pamoja na Mume wangu mtarajiwa Boniphace Magupa mpaka kufikia hapa."
Jessica akiwa na Mume wake Mtarajiwa Boniphace Magupa |
Kwa sasa The Jessica Music ina member wasiopungua 10 ikiwa ni waimbaji na wapiga vyombo. jessica anasema "Namshukuru Mungu kwa kuwa nao mana ni Baraka katika Maisha yangu na kwangu ni
ushuhuda mkuu wa Mungu alikonitoa". Sasa The Jessica Music inaelekea katika
tamasha la ZIMA UKIMYA NA JESSICA HONORE, Tamasha litakalofanyika pale City Christian Centre - Upanga Machi 24, Mwaka huu kuanzia Saa 9 Alasiri - Saa 1 Usiku. Kiingilio katika tamasha hilo kitakuwa ni Tshs. 15,000. USIKOSEEE!
Hii ni Video ya Wimbo wa Jessica Honore unaojulikana kama Napokea