SWALI
Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu!
Awali ya yote napenda kumshukuru Mungu kwa ajili yenu kwa huduma mnayoitoa ambayo imekuwa msaada katika maisha yangu kama mkristo na kama mwanajamii. Mungu awabariki sana.
Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu!
Awali ya yote napenda kumshukuru Mungu kwa ajili yenu kwa huduma mnayoitoa ambayo imekuwa msaada katika maisha yangu kama mkristo na kama mwanajamii. Mungu awabariki sana.
Pili naomba msaada wa maarifa juu ya namna ya Kumtambua mke ambaye Mungu ameniandalia. Nimefanya maombi ya kumuomba Mungu mke mwema tangu septemba 2008 hadi sasa lakini bado sijapokea majibu ya maombi yangu. Ninaamini ninasumbuliwa na Tatizo la upokeaji wa majibu ya maombi yangu jambo ambalo linahatarisha ustawi wangu kiroho.
Naomba kwa manufaa ya wengine pia ambao wana tatizo kama langu. Asante sana na Mungu
awatimizieni haja za mioyo yenu na kuimarisha huduma yenu ili watu wengi
zaidi waimarike kiroho.
Naitwa Lucas
Majibu;
Hello Lucas, tunakusalimu kwa jina la Bwana, ahsante kutuombea,
kututia moyo na kwa swali lako ambalo naamini majibu yake yatawafaa
wengi kama ulivyoshauri katika swali lako.
Kaka Lucas swali lako ni pana sana na ‘it is more personal’ kimajibu, lakini namshukuru Roho Mtakatifu anayeweza kutupa majibu ya kutufaa .Katika swali lako nimegundua mambo mawili ya msingi ambayo natakiwa kuyatolea ufafanuzi, moja ni namna unavyoweza kumtambua mke ambaye Mungu amekuandalia na pili namna bora ya kuomba yenye kuleta matokeo.
Katika kujibu maswali haya mawili nitazungumzia mambo manne yafuatayo ambayo naamini baada ya kuwa umeyasoma haya utapata ufahamu wa kukusaidia katika kufanya maamuzi hayo yanayokukabili;
Jambo la kwanza; Mungu hatumii njia au mfumo wa aina moja katika kukujulisha wewe mwenzi wa maisha yako (Isaya 55:8).
Oktoba 2006 naliandika kitabu kuhusu Njia kumi za Kibiblia
zitakazokusaidia kumjua na kumpata mwenzi wako wa maisha. Katika ukursa
wa nne wa kitabu hicho ndipo nilipoandika wazo hili hapo juu, kwamba,
Mungu hatumii njia au mfumo wa aina moja katika kumjulisha mtu mwenzi
wake wa maisha.
Nimeona hata sasa nianze na msingi huu na hii ni kwa sababu vijana
wengi hujaribu kuuliza wanandoa waliotangulia kwamba waliwapataje wenzi
wao wa maisha kwa dhana ya uongozi wa Mungu? Kutokana na majibu ambayo
vijana hao hupewa wengi humuomba Mungu na wanasubiri, Mungu aseme nao
kwa njia ile aliyotumia kusema na mtu mwingine.
Kibiblia wazo hili siyo sahihi kwani, Mungu ana njia nyingi sana za
kusema na watu wake katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na nani
atakuwa mwenzi wako wa maisha. Kwa mtu mmoja Mungu anaweza akasema naye
kwa ndoto, mwingine kwa sauti yake, na mwingine kwa maono, mwingine kwa
mafunuo, mwingine kwa amani ya Kristo, mwingine kwa kutumia
watumishi/wachungaji nk
Jambo ninalojaribu kukuonyesha hapa ndugu Lucas ni kwamba ‘Mungu ana namna yake ya kukusaidia kumtambua mwenzi wako wa maisha, ambayo si lazima ifanane na ya mtu mwingine’.
Na mara nyingi namna/njia hiyo haitofautiani sana na ile ambayo Mungu
hutumia kusema nawe katika mambo mbalimbali. Hivyo tafuta kujua njia
ambayo Mungu huwa anatumia kusema na wewe katika mambo mbalilmbali, naam
kwa hiyo aweza kusema na wewe hata kuhusu mwenzi wako.
Jambo la pili; Jenga na kuboresha mahusiano yako na Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu ndiye aliyepewa jukumu la kuwa Msaidizi wako hapa
duniani katika kufanya maamuzi mbalimbali. Watu wengi leo wanakwama au
wanajikuta wamefanya maamuzi mabaya kwa kosa la kutokumshirikisha Roho
Mtakatifu awasaidie. Mwambie Roho Mtakatifu nahitaji mwenzi(Mke), nisaidie kumtambua yupi ni wa kwangu, naomba uongozi wako.
Roho Mtakatifu kwa hakika atakuongoza katika njia sahihi (Zaburi 32:8).
Jambo la msingi ni kwa wewe kuboresha mahusiano yako na yake ili kuruhusu mawasilano mazuri kati yenu. Kumbuka mawasilano hutegemea mahusiano. Na jambo la msingi katika kuboresha mahusiano ni utakatifu na kutenga muda wa kuzungumza naye kwa njia ya maombi na neno.
Jambo la msingi ni kwa wewe kuboresha mahusiano yako na yake ili kuruhusu mawasilano mazuri kati yenu. Kumbuka mawasilano hutegemea mahusiano. Na jambo la msingi katika kuboresha mahusiano ni utakatifu na kutenga muda wa kuzungumza naye kwa njia ya maombi na neno.
Jambo la tatu; Jifunze kuruhusu mapenzi ya Mungu yatimie kuhusu mwenzi wa maisha yako.
Hili ni jambo lingine la msingi kuzingatia. Endapo umeamua kufuata au
kutafuta kumjua mwenzi wako kutoka kwa Bwana, basi ni vema ukaruhusu
mapenzi yake juu yako yatimie. Wengi huenda mbele za Bwana wakimuuliza
jambo hili lakini anapoleta wazo/jibu lake juu ya nani anafaa, wengi
wakishamtazama huyo muhusika kimwili na kwa vigezo vyao humkataa na
kusema si Mungu. Ni vizuri ukafahamu kwamba, kama Mungu ndiye aliyemleta
mtu wa kwanza kwako na wewe kwa sababu zako binafsi ukasema huyu si wa
kutoka kwa Bwana, maana yake umemzuia Mungu asikusaidie kwenye hilo
eneo, na hivyo usitegemee kusikia tena kutoka kwake, labda mpaka ujue
kosa lako na kuomba toba.
Kumbuka usimuombe Mungu akujulishe mwenzi wako wa maisha wakati
moyoni mwako tayari kuna mtu au watu ambao umeshadhamiria kutaka mmoja
wao awe mwenzi wako, Mungu hawezi kusema hapo. Ikiwa unataka Mungu
ahusike mpe asilimia mia moja hatafanya makosa kama Mwandamu.
Jambo la nne; Jifunze kuomba kimaswali
Najiribu kufikiri kwa nini umeomba tangu Septemba 2008 hadi sasa
Mungu asijibu? Kwa ufahamu nilionao katika Kristo nina hakika yeye
alisha-kujibu ila wewe ndiyo hukuelewa kwamba alijibu. Nina uhakika huo
kwa sababu mtu amwendeaye Mungu kutaka kujua jambo, Mungu humjibu mtu
huyo ili kumsaidia asipotee katika jambo hilo.
Naamini shida ipo kwako, huenda jibu ulilokuwa unataka wewe ni
kuambiwa fulani ndiye mwenzi wako, kumbe kwa Mungu huenda alikuwa
anasema huu si muda wake endelea kuomba maana kwa kila jambo kuna majira
yake. Zaidi huenda shida iko kwenye namna unavyoomba na namna
unavyopokea, au kuelewa Mungu anapoleta jibu.
Ili kuweza kupata ufumbuzi juu ya jambo hili jifunze kutumia mfumo wa
maswali katika maombi yako, naamini utaona matokeo yake. Jifunze
kuyatengeneza maombi yako kimaswali, omba huku ukitaka kujua/ukitafuta
ufumbuzi wa lile unaloliombea kwa Mungu.
Swali limejibiwa na;
Mwl. Patrick Samson Sanga
+255 755 816 800