Mkurugenzi wa Sifa Group Foundation, Sifa John |
Sifa Group Foundation ni taasisi iliosajiliwa kisheria, inajishugulisha na maswala ya
kusaidia watoto yatima na watoto wa mazingira magumu. Pia kituo hiki husaidia vijana wasio na
ajira ili wapate cha kufanya na wasiwe tegemezi.
Mkurugenzi wa Sifa Group Foundation, Sifa John akiwa Ofisini kwake |
Kituo hiki kilichopo Bunju B, Mtaa wa Sun Nsiro - Jijini Dar es salaam na kilichoanzishwa na Mwimbaji wa Nyimbo za Injili toka Nchini Tanzania Sifa John, mpaka sasa kimekwisha saidia vijana kumi na tatu(13) kwa kuwapa mafunzo ya ushonaji
na sasa wamejiajiri wenyewe. Vijana wengine saba(7) wamejua computer, na vijana wa tano(5)
wanajishughulisha na miradi ya chips na vinywaji.
Darasa la Cherehani linalomilikiwa na Sifa Group Foundation |
Pia kituo hiki kina jumla ya watoto 105
ambao ni yatima na wale wanaotoka kwenye mazingira magumu. Vijana hawa wanasaidiwa katika swala
zima la elimu, chakula na mavazi. Na kwa wale ambao hawajawahi kusoma
kabisa, kituo kimewatafuta walimu na kimeanzisha madarasa ambayo vijana hao wanapewa
elimu.
Baadhi ya Watoto wanaohudumiwa na Sifa Group Foundation wakipokea zawadi ya Nguo kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo hicho Sifa John |
Watoto 17 kati ya hao huishi hapo hapo kituoni na wengine hurudi
majumbani kwao jioni. Mkurugenzi wa kituo hicho Sifa John anasema, "Pamoja na kuruhusu watoto hawa warudi Majumbani kwao, roho yangu huniuma sana kwa sababu najua mahali
wanakoenda kulala palivyo pabaya, ila sina jinsi sababu sijapata nyumba
kubwa ya kuwatosha, lakini niko katika kutafuta jinsi ya kununua kiwanja
ambacho kipo tayari na kinahitaji pesa taslimu Sh. Milioni kumi na Sita, ili
tuweze kujenga shule pamoja na hosteli kwaajili ya kulala watoto hawa".
Hivi ndivyo Sifa Group Foundation inavyohakikisha kuwa Watoto wanaoishi kwenye Mazingira Magumu wanapata Elimu. |
"Pia maombi yangu
kwa mtu yeyote yule mwenye roho ya Huruma juu ya Watoto hawa, atowe msaada wowote alionao ili tuweze kupata
mahali pa kuwaweka watoto hao 115, na waweze kusoma na kuishi maisha mazuri kama wanayoishi watu wengine" Aliongeza Sifa John.
Mkurugenzi wa Sifa Foundation, Sifa John(Wa Pili Kulia) akiwa na Baadhi ya watu walinaojitolea Misaada mbalimbali katika kituop hicho |
Kwa
msaada wowote, Tumia namba hizi;
Tigo Pesa: 0652 562347
M-Pesa: 0766 91 37 80.
Account No: 010 - 00 175 951 (Benki ya Posta)
email: sifagroupfoundation13@yahoo.com
Au Tembelea; www.sifagroupfoundation.blogspot.com
Mungu akubariki sana wewe
utakayeguswa kwaajili ya jambo hili.