JANA tulielezea Mambo ya kuangalia katika Msichana afaaye kuwa Mke. Sasa leo tutazame Mambo
ya kuangalia katika Mvulana afaaye kuwa
Mme.
Kabla Msicha yeyote hajatoa mkono wake kwa Mvulana, kwanza
na ajiulize kama Yule mvulana wanayekaribia kuoana anafaa ama vipi. Mwenendo
wake na tabia yake ya Siku zilizopita ilikuwa ya namna gani? Maisha yake ni
Masafi? Upendo anioneshao unatoka Moyoni na Unaonesha heshima na tabia njema?
Ama ni Upendo wa hivi hivi tu?
Anao mwenendo ambao utanifanya kuwa na Furaha? Mimi kama Mke
nitaweza kuwa na Furaha niwapo kwake? Ataniruhusu kudumisha tabia yangu nzuri
na kunipa Uhuru, ama itanilazimu kutupilia mbali yote na kuangukia katika
Mamlaka yake?
Nikiwa nae kama Mme wangu, nitaweza kumuheshimu Mwokozi
wangu kama Mkuu katika yote? Mwili na Roho, Matendo na Mawazo vitaweza
kuhifadhiwa katika hali timilifu na takatifu? Maswali haya kama yakizingatiwa
kwa Busara yatakuwa ya Manufaa sana katika Maisha yajayo ya Msichana
anayetarajia kuolewa.
Kila Msichana anayetumainia kuwa na familia yenye furaha na
Amani ambayo haitajua Udhaifu wala Huzuni katika siku za mbele na ajiulize
Maswali haya kabla ya kutoa ukubali wake wa Upendo.
Je! Mpenzi wangu ana Mama?
Tabia ya Mama yake ikoje? Anatambua wajibu wake kwa Mama yake? Anajali Upendo
na Furaha ya Mama yake? Ikiwa hajali wala Kumuheshimu Mama yake, Je! Kweli ataweza
kuonyesha Heshima na Upendo, Wema na Usikivu kwa Mkewe?
Shani ya harusi itakapokwisha, atakuwa na Huruma kwa Makosa
yangu ama atakuwa akinikosoa mara kwa mara akiwa Mgomvi na Mkali? Katika
kuyajibu Maswali haya, shauku nyingi yaweza kupishia Mbali Makosa na Kasoro za
Mchumba wako lakini Upendo wa kweli hautaficha Neno.
Mkubali afaaye kwa Tabia
Katika kuchagua Mwenzi wa Maisha, Msichana na achague
Mvulana aliye na Tabia na Mwenendo safi wa kibinadamu, aliye na bidii,
Mwangalifu, Mwenye heshima, na aliye Mwaminifu na mnyoofu. Yule ampendaye na
kumuogopa Mungu.
- Ellen G. White -
- Ellen G. White -