Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, akiendesha ibada takatifu ya kubariki mafuta ya Pasaka na kurudiwa kwa kiapo cha mapadri, iliyofanyika Jana katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph |
Kardinali Pengo aliyasema hayo jana wakati wa misa ya sherehe ya Sakramenti ya Upadri na kubariki mafuta ya Pasaka katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini humo.
Alisema ni lazima kuwa watimilifu wa kibinadamu kwa kupitia njia ya sadaka, mateso na kifo hivyo kuwataka kuwafundisha yaliyo mema na yenye kumpendeza Yesu Kristu.
“Ili kufikia ukamilifu hatuwezi kukwepa misalaba, waumini mnatakiwa kutuombea ili kuweza kumwakilisha Yesu Kristu kwa matendo yaliyo mema na ya kumpendeza,” alisema Kardinali Pengo.
“Hivi sasa shida na mahangaiko ya dunia ni mengi lazima kumwonyesha Yesu ili aweze kutusadia na kushinda. Tukianza kuangalia chanzo cha matatizo na mahangaiko yalivyo hivi sasa hatuwezi kufika na tutaangamia,” alisema Kardinali Pengo.
Alisema njia nyingine zozote ambazo zinashabikia kama anasa na ukatili haziwezi kufanikiwa, hivyo aliwataka Mapadri hao kuwahubiria amani waumini.
- Mwananchi -