Mwl. Patrick Sanga |
Septemba 2011, Mwanafunzi mmoja wa shule ya Sekondari
alinitembelea nyumbani kwangu hapa Dodoma. Alipofika nilimkaribisha
ndani nikajua amekuja kunisalimia tu. Baada ya muda akaniambia kaka
Sanga nina swali nahitaji msaada wako sana. Tukatoka nje mahala penye
utulivu ndipo akaniambia tamaa za mwili kwa maana ya uasherati/zinaaa
zinanitesa nifanye nini ili kushinda? Jambo hili linanitesa kiasi kwamba
nahisi kama vile sijaokoka kutokana na vita niliyonayo katika fahamu
zangu na mwilini mwangu.
Kwa kuwa vijana wengi wamekuwa wakiuliza swali hili kwa namna tofauti
tofauti na kwa njia mbalimbali, nimeona ni vema nikaliweka somo hili
kwenye ‘blog’ hii kwa kuwa tunao vijana wengi ambao changamoto hii
inawakabili pia. Naam yafuatayao ni mambo ya msingi kuzingatia ili
kijana aweze kuwa na ushindi dhidi ya tamaa za mwili (dhambi) nk.
- Kwa kutii na kulifuata neno la Mungu
Biblia katika Zaburi 119:9 inasema ‘Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako’. Ukisoma Mstari huu katika tafsiri ya Biblia ya Kiingereza ya GNB unasema ‘How can young people keep their lives pure? By obeying your commands’.
Mtazamo wa tafsiri hii ya kiingerza ni kujaribu kutafuta ufumbuzi wa
namna ambayo vijana wanaweza kuishi maisha ya utakatifu na yenye
ushuhuda. Inawezekana mwandishi huyu wa Zaburi aliona namna vijana
wanavyohangaika katika eneo hili, ndipo ikabidi amuulize Mungu, ni jinsi
gani kijana aisafishe njia/au anaweza kusihi maisha ya utakatifu?
Kipengele cha pili kinatupa jibu la swali la kwanza kwamba ni kwa kutii, akilifuata neno lako.
Naam hii ina maana ni lazima kwanza kijana achukua hatue ya kuliweka
neno la Mungu moyoni mwake kwa wingi, maana hawezi kutii neno ambalo
halimo ndani yake au hajalisoma na kulitafakari. Zaburi 119:11 inasema ‘Moyoni mwangu nimeleiweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi’.
Maana yake ni kwamba, kama kijana atajijengea tabia ya kuhakikisha
analiweka neno la Bwana moyoni mwake kwa kulitafakari kila siku, kwa
vyovyote vile lazima atakuwa na ushindi dhidi ya tamaa za mwili na kazi
zote za Shetani. Naam usiishie tu kuliweka moyoni mwako bali fuatilia
sauti ya neno uliloliweka ndani yako, ukaiitii.
- Kuacha michezo ya mapenzi na kuwa makini na nini unatazama/unasikia.
Michezo ya mapenzi (foreplay) ni maalumu kwa ajili ya wanandoa. Kwa
bahati mbaya vijana wetu nao sasa wamekuwa wakifanya mambo haya ambayo
kimsingi si yao. Michezo ya mapenzi ni sehemu ya vitendo vyvyote ambavyo
hupelekea ashiki ya kufanya tendo la ndoa hii ni pamoja na kushikana
shikana/kugusana maeneo mbalimbali ya mwili na pia kunyonyana ndimi.
Zaidi Katika dunia ya sasa Shetani ametumia teknolojia iliyopo kuteka
fikra za vijana wengi. Vijana wengi kupitia simu, computer, video nk
wanaangalia picha chafu za ngono na kusoma jumbe za aina hiyo kitu
ambacho kinaharibu fahamu zao bila wao kujua. Na kwa kufanya hivyo
wanakuwa wanayachochea mapenzi na kuamsha tamaa zao za mwili. Naam mambo
haya ni hatari tena kinyume na mapenzi ya Mungu. Na kwa bahati mbaya
vijana wetu tena waliokoka baadhi yao bado wamefungwa katika kufanya
mambo haya.
Katika kile kitabu cha Wimbo Ulio Bora 2:7 Biblia inasema ‘Nawasihi,
enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee
mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe’.
Kulingana na mstari huu tunajua kwamba, kumbe mapenzi yanaweza
kuchochewa na kuamshwa, naam na hili ni jambo hatari sana kama
litafanywa na wahusika ambao si wanandoa kwa maana ya (foreplay) hata
kama wana kiroho cha iana gani.
Jambo la msingi kuepuka hapa ni kuwa kwenye mazingira ambayo yanaweza
yakawashawishi kufanya mambo haya. Vijana ambao si wanandoa
kutembeleana mahali wanaposihi kwa maana ya eneo ambalo wako pekee yao,
au kwenda guest na maeneo yote ya namna hii eti kwa lengo la kupanga
mipango yenu. Fahamu kwamba kitendo cha vijana wawili ambao si wanandoa
kukaa katika mazingira ya aina hii ni kumpa Iblisi nafasi ya kuwamaliza,
naam kijana uwe makini usifanye ujinga huu, Shetani asije akakumaliza.
- Kuenenda kwa Roho.
Mtume Paulo alikutana na kesi ya aina hii kwa wandugu wa kanisa la
Galatia. Moja ya ufumbuzi juu ya suala hili aliwataka waenende kwa Roho
ili wasisitimize kamwe taamaa za mwili. Wagalatia 5:16 ‘Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili’.
Kuenenda kwa Roho kukoje? Ni kuishi/kuenenda kwa kufuata
utaratibu/uongozi wa Roho Mtakatifu maishani mwako (Zaburi 32:8). Jambo
la msingi ni kuwa mtiifu kwa Roho Mtakatifu, naam atakusaidia kushinda
dhambi kama alivyomsaidia Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani.
- Kujitenga na marafiki/makundi mabaya
Zaburi 1;1 inasema ‘Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri
la wasio haki; Wala hakusiamama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi
barazani pa wenye mizaha’. Jiulize muda wako mwingi unautumia
kwa kufanya nini? Na kama ni marafiki ni marafiki wa aina gani? Siku
zote wale unaokuwa nao karibu wanachangia sana kujenga (kushape) mfumo
wa maisha yako.
Biblia katika 1 Wakorinto 15:33 inatuambia ‘Msindanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema’.
Naam kama utakuwa na marafiki wabaya basi tegemea na mazungumzo yao
yatakuwa mabaya na hivyo tegemea na wewe kuwa na tabia mbaya. Jambo la
msingi ni kujitenga nao usiende katika shauri lao, wala njia yao na pia
kuketi katika baraza yao.
Mtume Paulo akizungumza na kijana wake Paulo alimwambia hivi ‘Mtu
awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio,
katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi’ 1
Timotheo 4:12. Wazo ninalotaka ulipate hapa ni kwamba kama Paulo
angejua kwamba vijana hawawezi kuishi maisha ya utakatifu na yenye
ushuhuda katika dunia hii, asingemwambia Timotheo afanye haya. Basi kwa
kuwa alijua inawezekana, ndiyo maana Roho Mtakatifu alimwongoza kuandika
haya ili kumwagiza Timotheo na sisi vijana wa leo katika jambo hili.
Naam uwe kielelezo katika shule, chuo, kanisa, kazini nk ili Mungu aone
sababu ya kuendelea kukutumia kwa utukufu wake.
Kama unataka KUOKOKA hivi sasa, Bofya Hapa
Neema ya Mungu iwe Nawe!
Mwl. Patrick Samson Sanga
+255 755 816 800