- Jina lake Kamili ni Ruth Lyanga George. Alizaliwa Mwezi Novemba 1986 huko Musoma Mkoani Mara. Ni Mtoto wa 4 kuzaliwa kati ya Watoto wanne wa Mr. George Manase Lyanga, na Mama alikuwa anaitwa Neema Manase (Alifariki Mwaka 2004). Kwa upande wa Kabila, Ruth ni Mnyiramba toka Singida.
Ruth Lyanga George |
- Elimu yake ya Msingi aliipata kwenye shule ya Msingi Kapolo iliyopo Ifakara, Morogoro (1994-2000), Elimu ya Sekondari aliipata Kwenye shule ya Sekondari Kilombero (2001-2004), Elimu ya Kidato cha 5 na 6 aliipata kwenye Shule ya Sekondari Bahari Beach (2007-2009). Na kwasasa Ruth anasomea Shahada ya Mahusiano ya Umma na Masoko (Ba. Public Relation and Marketing) mwaka wa 2 katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustino, campus ya Mwanza.
Ruth Lyanga akiimba katika Tukio la Uzinduzi wa Kitabu cha "Wokovu ni Uhakika wa Maisha ya Sasa na ya Baadaye" kilichoandikwa na James Kalekwa. |
- HISTORIA YAKE KIUIMBAJI
Ruth alianza
kuimba katika kwaya ya Sunday School, na baadae alianza kuimba katika
Kwaya ya Kanisa la Kapolo EAGT Morogoro. Mwaka 2005 wakaanzisha kundi la
King Jesus Family likiwa na Waimbaji kama Eliana, Witness, Penina, Pendo, Lyanga, Ruth Mwenyewe pamoja na David.
Mwaka huo huo 2005, Ruth, Lyanga, pamoja na Witness walishiriki Gospel Star Search wakiiwakilisha King Jesus Family toka Mkoani mbeya ambapo walikuwa Washindi wa Mkoa hivyo Waliiwakilisha Mbeya katika Mashindano hayo ya Gospel Star Search.
Ruth akiwa na Praise Team iliyohudumu Siku ya Uzinduzi wa Kitabu |
- Mshindi wa Kwanza katika Gospel Star Search hiyo ya Mwaka 2005 alikuwa ni Jesca Honore, wa 2 alikuwa Jonsia Njamanse, na wa 3 alikuwa ni Lwiza John. Washiriki Wengine wa Gospel Star Search hiyo ya Mwaka 2005 ni kama Betty Lucas, Victor Aron, Meshack Mwakyebula na Charles Thobias.
Mwaka 2007 Ruth akiwa na King Jesus Family
walitoa Albam ya Kwanza kama Kundi iliyo05 ni kama Betty Lucas, Victor Aron, Meshack
Mwakkuwa na Jina la “Twende Nawe”
iliyokuwa na Nyimbo kama Sema nami, Hosanna, Yahwe pamoja na Twende
nawe. Na kwasasa kundi hili lilikuwa linaundwa na Waimbaji toka familia
Moja yaani Ruth, Lyanga pamoja na David.
Lyanga ni Mwimbaji na pia ni Audio Producer katika Studio yake Mwenyewe inayojulikana kama Icon Production iliyopo Maeneo ya
Bandari Jijini Dar es saalam. Kwasasa ni Kiongozi wa Glorious Celebration ya Jijini Dar es salaam na pia yuko katika Mchakato wa Kumalizia Album yake ya Pili ambayo itatoka sambamba na Video baada ya album yake ya Kwanza ya "Umenishika Yesu" kufanya vizuri.
Tafes Saut (Praise and Worship Team)
toka katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustino campus ya Mwanza, ndipo ambapo
Ruth anaendelea na Huduma yake ya Kumtumikia Mungu kupitia Uimbaji kwa
sasa.
Ruth katika Pozi |
Hii pia ilikuwa ni Sehemu ya Mazungumzo yetu kati ya Gospel News Media na Ruth Lyanga…….
Gospel News Media; Ni Mwimbaji gani wa hapa Nyumbani Tanzania unayevutiwa na uimbaji wake?
Ruth Lyanga;
Ni wengi, lakini hasa ni Upendo Kilahiro, Jackon Benty na Marehemu
Fanuel Sedekia kwasababu wao ni waimbaji walioegemea sana katika Upande
wa Nyimbo za Kuabudu.
Gospel News Media; Na kwa Upande wa Nje ya Nchi Je!?
Ruth Lyanga; Kwa Nje ya Nchi navutiwa sana na Benjamin Dube pamoja na Kirk Franklin
Gospel News Media; Je! Una mpango wa kuwa Solo Artist kwa baadae?
Ruth Lyanga;
Yah! Mpango huo upo, lakini ntakuwa nashirikiana na Waimbaji wengine
kama wanavyofanya waimbaji kama Cece Winans, na Benjamin Dube.
- Gospel News Media; Nini Matarajio yako ya Baadae?
Ruth Lyanga;
Natarajia kuwa Mwimbaji wa Kimataifa, na Mtumishi wa Mungu katika eneo
la Kufundisha Neno lake kama alivyo Joyce Meyer. Na si kwa baadae tu
bali hata hivi sasa Mimi na Mtumishi wa Mungu na Bwana anaendelea
Kuniandaa.
Gospel News Media; Nini Malengo yako ya Baadae?
Ruth Lyanga;
Kwa baadae nina Malengo ya kuja kufungua Taasisi itakayojishughulisha
na Utoaji wa Elimu kwa Vijana, na hasa Elimu ya Kumjua Mungu pamoja na
Elimu ya Ujasiriamali, Muziki na Uimbaji.
Gospel News Media; Nashukuru sana kwa Ushirikiano wako!
Ruth Lyanga; Nashukuru pia!
Tazama Video hii, Ruth Lyanga aki’lead Wimbo wa “Katikati ya Wafalme”