Kuna Ushindi katika Kusamehe.
Bwana Yesu asifiwe sana, namshukuru Mungu kwa fursa hii tena ninapokukaribisha katika somo letu linalohusu Msamaha.
Ndugu yangu, Dhana ya Kusamehe inaweza kufasiliwa kama hali ya
huachilia, yaani kupuuza, hili ni jambo ambalo kila mmoja wetu analijua
na pengine kila mmoja wetu limemkuta, aidha kwa kusamehe au kusamehewa! KWA UFUPI, GHARAMA YA MSAMAHA HUWA NI YA ANAYESAMEHE, JAPO ANAYELIPA NI
ALIESAMEHEWA.
Naomba unielewe vizuri, unaposamehe, kwako huna
dukuduku, ila aliyesamehewa hubaki na maswali aghalabu kama hakutegemea
kusamehewa.Hii inadhihirisha kuwa, mara unaposamehe, anayesamehewa
anabaki na maswali kichwani kuwa kweli kasamehewa au la, na hii ndiyo
gharama halisi.
Wengine husema, katu siwezi kusamehe, na hata
nikisamehe siwezi kukusahau, lakini Biblia inatueleza (Mathayo
6:12)"Msipowasamehe wengine Makosa yao,wala Baba yenu hatawasamehe ninyi
makosa yenu" Hii ina maana gani? Hapa Mungu anatudhihishia kuwa, Kanuni
anayotumia katika kukusamehe, ni ile ile uliyotumia katika kuwasamehe
wengine; Yaani kwamba, kama hujawasamehe wengie, hata wewe huwezi
kusamehewa
Ni wazi kuwa kumsamehe mtu aliyekuumiza sio jambo la
mzaha na wala si suala la dogo lakini hapo hapo ndipo Mungu anapotaka
kuona utu wako na uvumilivu wako. Wengine machoni pa watu hudiriki
kusema "Yameisha" mara nyingi baada ya USULUHISHO, lakini ndani ya mioyo
yao bado hajasamehe.
Rafiki, naomba ujue kuwa, kabla mtu
hajakuudhi, kuna nguvu inayokuwa nyuma yake ambayo humwongoza ili
akuumize! Usipojua hilo, utaangamizwa na nguvu hiyo, kwasababu nguvu
hiyo ni ya roho iliyotumwa kukuangamiza hata kupitia hasira, chuki na
kutokusamehe.
Angalia mfano huu wa gari linapomgonga mtu serikali
haishtaki gari bali anayeshtakiwa ni dereva. Hii ina maana kwamba,
anayekukosea huwa ana anayemhimiza kufanya hivyo! Vivyohivyo ukiumizwa
unatakiwa uangalie ile nguvu iliyopo nyuma ya aliyekuumiza. Kimsingi
kuna nguvu inayotenda kazi nyuma ya aliyekuumiza na usipoijua hiyo nguvu
utajikuta unashindwa kusamehe.
Usichoke kusamehe, kwa kuwa
neno linasema samehe saba mara sabini tena kwa kwa kutwa, tena
linaongeza, usichoke kutenda wema maana Bwana atatulipa tusipozimia
mioyo, Naomba unielewe vizuri hapa, Hii inamaana kuwa, kwanza una kheri
wewe uliyepewa ufunuo hata ukajua kuwa yule kakutendea uovu, je si kazi
yako kumsamehe na ndipo uanze kumuelimisha?
Hili linaenda hata Kwa
wazazi, nawaombeni watoto wenu wanapowakosea wakati mwingine mtumie njia
mbadala kuwaadhibu na siyo kuwachapa tu, kwani huyu pengine hajui kama
ametenda kosa na pengine ni bahati mbaya tu, kwani sisi kama tungekuwa
tunaadhibiwa mara tutendapo dhambi hata kwa kiboko kimoja tu, si wengine
tungekuwa hatuna ngozi kabisa?
Mpendwa, naomba nikwambie
kuwa, kwa kusamehe, unajipatia kibali mbele za Mungu na kukuondolea
magonjwa yako yote. Zaburi 103:3 "Akusamehe maovu yako yote, Akuponya
magonjwa yako yote".
Magonjwa haya si lazima uwe hoi kitandani, pengine
unaweza hata ukawa na hasira tu, basi wee samehe ili Mungu akuondolee
hasira hiyo, Samehe ili Mungu afute kumbukumbu ya ulivyokosewa na wala
usije ukakumbuka tena. Tena ukimsamehe ongea nae vizuri, mtolee ushuhuda mzuri na umwombee sana ili Mungu amrehemu-Haleluya!
Nawasiki,tuepuke misamaha ya kinafiki ya kusema eti sitakusahau, huu si
msamaha wa kweli., msamaha huu hautoki kwa Mungu, huu umetoka kwa
shetani.Epuka na mizigo hiyo. Kumbuka Isaya 1:18,....dhambi zenu
zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji, zijapokuwa
nyekundu kama bendera, zitakuwa nyeupe kama sufu, na kama mkikubali na
kutii, mtakula mema ya nchi. Rafiki yangu, inakuwaje wewe ukisamehe
ukumbuke, ebu uache moyo wako mweupe usio na madoamadoa, usio na
kinyongo!
Kwanini Mungu amesema dhambi zako zitakuwa nyeupe wala si
njano, orange au hata kahawia? Yesu anataka aweke utukufu ndani yako
kupitia msamaha, achilia moyo wako, ili Bwana aingie akuponye magonjwa
yote, aoundoe BP zako zote, aondoe vidonda vya tumbo katika jina la Yesu
Kristo. Samehe uwekwe huru.
Waefeso 1:7 Katika yeye huyo (YESU) kwa
damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha (yaani mingi na mikubwa) ya
dhaambi sawa sawa na wingi wa neema yake. Nakuomba usihesabu makosa bali
uhesabu utukufu wa Mungu unaoupata kupitia Masamaha.
WEWE ULIYEGUSWA MAFUNDISHO HAYA RUDIA SALA HII HAPA CHINI.
Baba katika Jina la Yesu Kristo ninaomba nguvu ya msamaha wako; leo
nimetambua kuna nguvu inayotenda kazi nyuma ya mtu
aliyenikwanza,ninawasamehe wote walionikwaza katika Jina la Yesu.
Ninatangaza msamaha, ninavunja madhabahu ya makwazo na kutokusamahe
ndani yangu katika jina la Yesu Kristo. Baba ninaomba uniponye na
matatizo yaliyoingia ndani yangu kwasababu ya kutokusamehe katika Jina
la Yesu.
BASI BAADA YA KUPOKEA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU NAOMBA NIKUOMBEE SASA ILI UDUMU KATIKA PENDO LA KRISTO.
Baba katika Jina la Yesu Kristo ninakushukuru kwa neno lako na msamaha
wako kwa watoto wako, Ahsante Yesu kwa wote waliokili ujumbe huu!Baba
naomba rehema zako ziwe juu yao tangu sasa, katika jina la Yesu Kristo,
uwajaze roho ya msamaha na upendo. Ondoa magonjwa yao yote yaliyowatesa
siku zote, futa visasi na laana za kutokusamehe katika Jina la Yesu
Kristo mwana wa Mungu uliye hai.
Kwa Mawasiliano zaidi.......
Mwl. Sospeter Simon,
S.L.P. 568
Tukuyu.
Email: sos.sesi@yahoo.com
+255 784/757 464 141
+255 712 909 021