Adolph
Robert Nzwalla ni Kijana wa Kwanza kwenye Familia ya Marehemu Bishop
Robert Nzwalla na Bishop Irene Nzwalla kutoka katika kanisa la Hosanna
Christian Centre lililopo Ghana, jijini Mwanza. Addo kama ajulikanavyo na wengi ,
anao wadogo zake wapatao wanne ambao ni Priscilla na Gladyce hawa ni
mapacha na mdogo wao wa Mwisho anaitwa Joseph Robert Nzwalla.
Adolph Robert Nzwalla akipiga Keyboard wakati wa Ziara ya John Lisu jijini Mwanza |
Adolph
Nzwalla ni Mtangazaji wa redio ya kikristo ijulikanayo kama HHC Alive
Fm yenye makazi yake maeneo ya Kirumba jijini Mwanza inayorusha
matangazo yake kupitia masafa ya 91.9 Fm. Tofauti na utangazaji Addo pia
ni Music Director wa Hosanna Praise team ya Jijini Mwanza. Kwa muda
mrefu sasa amekuwa akijishughulisha na muziki wa injili akiwa kama
muimbaji, mpigaji na mshauri kwa makundi na matukio mbalimbali
yafanyikayo jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla.
Slim B |
Adolph
Nzwalla alianza rasmi kujishughulisha na muziki akiwa mwanafunzi wa
darasa la saba katika Shule ya Msingi Nyanza na baada ya hapo alijiunga
na shule ya sekondari Mwanza(Mwanza Sec). Baada ya kumaliza elimu yake ya Sekondari, Addo alipata nafasi ya Kwenda kusoma Nchini Marekani katika
Chuo cha Word of Life School of Ministry ambacho kiko katika Jimbo la
Delaware na baada ya kumaliza masomo alirejea Nyumbani na kuunda kundi la
Hosanna Praise Team ambalo ndilo anafanya nalo kazi hivi sasa Kama Music
Director na Worship Leader wa kundi hilo.
Mwaka 2009 Addo alikuwa ni mmoja wa majaji katika shindalo la Kusaka
Vipaji kwa kanda ya Ziwa lijulikanalo kama “Zaburi Gospel Star Search”
ambalo lilikuwa likirushwa na kituo cha Television cha Star Tv cha
jijini Mwanza. Mwaka juzi Addo alikuwa miongoni mwa watumishi
walio-organise ujio wa New Life Band katika jiji la Mwanza. Katika ujio
huo kulifanyika Tamasha kubwa la kihistoria katika viwanja vya Furahisha
lililohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza pamoja na mama Diana
Mwakasege kutoka Arusha.
Adolph Nzwalla akirun show ya Cross Rythm ndani ya Hhc Alive Fm |
Addo
anauwezo mkubwa wa kupiga Gitaa la solo, Keyboard, drumz na tumba, lakini
kwa muda mwingi huonekana akipiga keyboard. Katika Huduma hii ya Uimbaji
amefanya Huduma na Waimbaji wakubwa kama Jackson Benty, John Lisu, Miriam
Lukindo, Pastor David Yared pamoja na waimbaji wengi wa sifa na
kuabudu. Katika jiji la Mwanza Addo amekua akiandaa na wakati mwingine
kushirikishwa katika kuandaa matamasha mbalimbali ya kusifu na kuabudu.
Adolph Nzwalla akiongoza worship pamoja na mtumishi Ihano Nestory wakati wa ThanksGiving Concert |
Tazama Video hii ambapo Addo alikuwa aki'lead Wimbo wa Ahsante Yesu.