Goodluck Gozbert a.k.a Goody ni Mwimbaji wa Nyimbo za Injili
toka Mkoani Mwanza, Tanzania ambako ndiko alikozaliwa. Goodluck alizaliwa April
12, Mwaka 1991 katika hospitali ya Bugando, Mwanza. Akiwa ni Mtoto pekee wa Bw.
Gozbert Rweyemamu pamoja Janeth Gozbert, Goodluck alilelewa na Mama yake pekee
baada ya Baba yake mzazi kufariki huku Goodluck akiwa na Umri wa Mwaka 1.
Goody anasema alianza kazi za uimbaji Mwaka 2005 akiwa na
Tumaini Choir (K.K.K.T- Imani Mwanza). Baada ya Miaka 3 yaani 2008, Goody alianza
kuimba nyimbo zake pekeyake huku akiwa bado ni miongoni mwa waimbaji wa Kwaya
ya Tumaini (K.K.K.T- Imani Mwanza).
Goody alitoa Album yake ya Kwanza Agosti 19, 2008
aliyoifanya katika Studio ya Ujumbe Records chini ya Meneja wake Abraham
Nyantori. Katika Utengenezaji wa Album hiyo, Goody alifanya kazi na Maproducer
mbalimbali wa Jijini Mwanza kama Selemani Muyomba, na Charles Sokoro.
Mwaka 2012 Goody alianza kurekodi Album yake ya 2 aliyoipa
Jina la NIMEUONA, ambalo ni Jina la Moja ya Nyimbo zinazopatikana katika Album
hiyo. Katika Album hiyo kuna Nyimbo kama vile Nimelipiwa Deni, Nimeuona na Wa
Moyo(Wimbo unaopendwa sana na Watu wengi na ni Wimbo Unaofanya vizuri sana
katika vituo mbalimbali vya Nyimbo za Injili Kanda ya Ziwa).
Mbali ya Uimbaji Goody anauwezo mzuri wa kupiga Kinanda,
Drums, Guitar, na Trumpet, Vyombo alivyojifundisha yeye Mwenyewe akiwa kanisa
la K.K.K.T- Imani chini ya Tumaini Choir. Goody pia ni Mwandishi wa
Nyimbo, Mtayarishaji wa Nyimbo(Audio
Producer), Mwandishi wa Script, Muongozaji wa Filamu na Pia ni Muigizaji.
Baadhi ya Nyimbo katika Album yake ya 2 amezitengeneza yeye Mwenyewe kuanzia
Utunzi, Utengenezaji wa Beat pamoja na Kufanya Mixing.
Tazama Video hii ya Goodluck Gozbert, Jina la Wimbo ni
Nimelipiwa Deni
Mawasiliano ya Goodluck Gozbert
0762486168