Advertise Here

Friday, October 4, 2013

Mwimbaji Mtanzania Fay Destiny apata Tuzo Marekani.


Mwimbaji wa Nyimbo za injili kutoka Tanzania mwenye asili ya Zanzibar Fay Makame Haji almaarufu kama Fay Destiny ambaye alibadili Dini kutoka Uislamu na kuwa mkristo, ameibuka kidedea katika nafasi ya tatu katika Tuzo za Uimbaji wa Nyimbo za Injili Kimataifa kwa Nchi za Afrika zilizofanyika huko Maryland, Marekani.

Fay amekamata nafasi hiyo baada ya kuchuana vikali na Waimbaji wengine kutoka Mataifa mbalimbali Afrika kama vile Nigeria, Liberia, n.k

Wakati huo huo Fay Destiny anatarajia kuzindua Album yake mpya Jumamosi hii, ambapo Uzinduzi huo utasindikizwa na Waimbaji mbalimbali kama J Sistres na wengine.

Hebu Msikilize hapa akinadi Uzinduzi wake

Thursday, October 3, 2013

Watu zaidi ya 20 warudishwa kutoka kwenye Misukule huko Arusha kwenye Mkutano wa Mch. Gwajima.

Mch. Gwajima akifundisha katika Mkutano

Ni siku nyingine kubwa ambayo Mchungaji Josephat Gwajima ameendelea kutumiwa na Mungu katika Mkutano Mkubwa wa Injili mkoani Arusha. Ikiwa ni siku ya sita leo hii kumetokea mambo ya Ajabu kupita akili za watu kwani watu zaidi ya ishirini ambao walikuwa wamechukuliwa msukule na kupelekwa mikoa mbali mbali kurudishwa.

Akiongozwa na Roho Mtakatifu kuomba kwa kuita watu waliokuwa wamechukuliwa; Mchungaji Gwajima aliomba maombi ya nguvu na kuamuru wote waliochukuliwa warudi. Zifuatazo ni shuhuda mbalimbali za siku ya leo na mambo ambayo Mungu ametenda siku ya leo.

Baadhi ya watu waliorudishwa kutoka kwenye Misukule
Wa kwanza kutoa ushuhuda alisema kuwa yeye anaitwa Neema, alikua amechukuliwa na kupelekwa zanzibar ametoka huko kwa kuruka na alichukuliwa na mke wa shemeji yake.

Mwingine ambaye jina lake halikupatikana kwa haraka alidai kuwa yeye alichukuliwa na kupelekwa Unga Limited.

Mtu wa tatu kutoa ushuhuda; yeye alisema kuwa alikuwa amechukuliwa na bibi yake na kwa jina anaitwa Mary. Kazi yake huko alikuwa analima viazi na walikuwa wanakunywa damu za watu.

Flora na Emmanuel Mbasha wakihudumu katika Mkutano huo
Ushuhuda mwingine uliovuta hisia za wengi ni wa binti wa kiislam aliyeitwa Mwajuma; yeye alisema kuwa alikuwa tabora, ghafla akiwa huko akasikia sauti ikimwita NJOOO akajiona anapaa hadi uwanjani, Arusha. Wakati anasikia sauti hiyo alikuwa katika kazi za kawaida huko za kulima na kazi nyingine aliyokuwa anafanya msukuleni ni kusababisha ajali. Chakula cha huko kilikuwa ni nyama za watu na damu. Mwajuma alisema hataki tena kuwa Muislamu na wachawi wapigwe kwakuwa wanatesa watu wengi maana kuna wengine amewaacha huko wengi.

Ushuhuda mwingine ni wa binti anayeitwa Husna; yeye alikuwa tanga na alichukuliwa msukule na shangazi yake baada ya kulishwa sumu na kufa, ndugu zake waliona amekufa kumbe yeye alikuwepo msukuleni.

Mwingine aliyepata nafasi ya kutoa ushuhuda anaitwa Pendo; yeye alikuwa makaburini alichukuliwa na mama mmoja ambaye hakumkumbuka kwa haraka bali alisema; mama huyo alikuwa mrefu. Mama huyo alimwambia kuwa anampenda na akamchukua akawa anafanya kazi ya kusafisha makaburi ndipo alipopata nafasi ya kumchukua na kumweka msukuleni kwenye makaburi hayohayo aliyokuwa akisafisha.

Baadhi ya Umati wa watu wakiwa Mkutanoni
Mwingine aliyerudishwa alisema kuwa anaitwa Nipha na alichukuliwa akapelekwa Moshi. Akiwa msukuleni akasikia sauti ikimwita NJOO akapaa kutoka moshi; ambapo huko aliwekwa kwa mganga wa kienyeji kwenye kobe ya kuagua.

Msichana mwingine pia alitoa ushuhuda wake kuwa alikuwa Tanga, na jina lake anaitwa Zerina; binti huyo alisema huko Tanga alikuwa anakaa kwenye maji kwenye maji, huko alipelekwa kwa babu mmoja anaitwa hussein alikua hali chakula na alikaa kwa mateso sana.

Mwingine aliyepata nafasi ya kutoa ushuhuda alikuwa anaitwa Rose ambaye yeye alichukuliwa msukule na kupelekwa kibosh. Jina lake ni Rose; alikuwa analishwa nyama za watoto wadogo. Rose alichukuliwa na mke wa mwisho wa baba yake anaitwa Magreth, alisikia sauti kutoka huko akajiona anapaa hadi mkutanoni.

Wa mwisho kushuhudia alisema yeye alikuwa anaitwa Esther na alichukuliwa msukule na kupelekwa Sumbawanga. Yeye alichukuliwa na jirani yake hapo katika mtaa anaoishi.

Na huu ni Umati uliohudhuria Mkutano huu wa Arusha chini ya Kanisa la Ufufuo na Uzima

- Ufufuo na Uzima & Gospel Kitaa -

Happy Mkamwa ‘Nyatawe’ alilia Mtoto, Aamua Kuokoka.

MSANII wa maigizo kutoka Kundi la Msanii Afrika, Happy Mkamwa ‘Nyatawe’ ameamua kuokoka baada ya kuhangaika kwa muda mrefu akitafuta mtoto bila ya mafanikio.

Akizungumza kwa huzuni na paparazi wetu, Nyatawe ambaye anasali kwa Mchungaji Antony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ alisema kuwa yuko ndani ya ndoa kwa miaka mitatu lakini hajabahatika kupata mtoto na ameshahangaika katika hospitali mbalimbali.

“Kila tukichukuliwa vipimo na mume wangu, wote tunaonekana hatuna matatizo, pia nimetumia madawa ya kienyeji lakini hakuna mafanikio yoyote.

Kutokana na hilo msanii huyo ameona ni heri aokoke na kuwaomba wasanii wenzake wamuombee kwa sababu anatamani sana kuitwa mama.

“Nilishawahi kushika ujauzito lakini ukatoka na mpaka leo sijashika tena, mume wangu amekuwa akinifariji na kunipa moyo kwamba siku moja tutapata mtoto lakini nimekata tamaa,” alisema Nyatawe.

- Global Publishers -

Wednesday, October 2, 2013

Sikiliza Mafundisho ya Mwl. Christopher Mwakasege - Sadaka Part I.

Mwl. Christopher Mwakasege
Sikiliza Sehemu ya Kwanza ya Mafundisho haya kuhusu "Sadaka" kutoka kwa Mtumishi wa Mungu Mwl. Christopher Mwakasege aliyofundisha katika Semina iliyofanyika Jijini Dar es salaam, Mwezi September 2013 katika Viwanja vya Jangwani.

Kama Unahitaji CD za Mafundisho haya, Wasiliana na Huduma ya MANA kwa Mawasiliano yafuatayo:

Simu: 0736581861 
Facebook: Christopher & Diana Mwakasege(Mana Ministry). 
Postal Address: P. o Box 2166, Arusha,Tanzania Fax: 0736581862 
Email: tasoet@nexusdigital.co.tz
 
Usikose kufuatilia Sehemu ya Pili ya Mafundisho haya kutoka kwa Mtumishi wa Mungu Mwl. Christopher Mwakasege Jumatano Ijayo kupitia Mtandao huu.

Timu ya Praise & Worship yaendelea na Mazoezi kwa ajili ya Ibada ya Kusifu na Kuabudu ya Octoba 6.

Zikiwa zimebaki Siku 4 ifike siku yenyewe ya Ibada Kubwa ya Kusifu na Kuabudu katika Kanisa la New Vine Christian Centre lililopo Tema Hotel, Nyegezi-Mwanza, Mtandao wa Gospel News Media jana usiku ulifika Kanisani hapo na kukuta Vijana wa Praise & Worship Team wakiendelea na Mazoezi ya Kunoa Sauti zao pamoja na Upigaji wa Vyombo, tayari kabisa kuongoza Ibada kubwa ya Kusifu na Kuabudu itakayofanyika Jumapili ya October 6, 2013.

Hizi ni baadhi tu ya Picha tulizofanikiwa kukuletea ili Japo uone ni kwa namna gani Maandalizi ya Ibada hii kubwa yanavyoendelea.

Mazoezi yakiendelea
Masha Makaya - Basist
David - Keyboard No. 2
Jema - Keyboard No. 1
Solomon kwenye Tumba
Sauti ya 3 Wanaume
Sauti ya 3
Mwl. Boaz akifundisha
Chombo cha Habari(Blogger) Baraka Samson kwenye Drums
Baadhi ya Wana'Praise
Mwl. Boaz akitoa maelekezo kwa Mpiga Keyboard
Sowane Emmanuel na Charles Ernest
 Kumbuka tu kwamba Tshirt za event hii zinapatikana bado. Piga Simu Sasa: 0712 113305 na 0754 030789.