Neema Decoras |
Neema Decoras (Amezaliwa Tarehe 27 Julai 1984) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo za Injili za Kikristo mwenye kipawa na hodari kutoka nchini Tanzania ambaye amejitoa kuwa chombo imara cha Uinjilisti na kutumikia kusudi la Mungu katika wakati wake. Alizaliwa katika jiji la Mbeya, Tanzania na ni watatu kuzaliwa katika familia ya watoto saba.
Neema Decoras ambaye kwa sasa ni mama wa watoto wawili wa kike na mke
mpendwa wa mume mmoja alianza uimbaji wa nyimbo za injili akiwa mdogo
sana katika shule ya Jumapili ya Kanisa La Pentekoste Tanzania (KLPT) kabla ya kuokoka na kubatizwa na mchungaji Mwakanyamale wa Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) ya Ilembo, Airport, Mbeya.
Neema Decoras aliendelea na huduma ya uimbaji katika kipindi chote
alichokuwa akisoma, kuanzia shule ya msingi hadi sekondari. Akiwa
anachukua elimu ya sekondari alikuwa mwanachama na mwalimu wa kwaya ya Christ's Ambassadors Students Fellowship Tanzania (CASFETA) katika shule yake na muimbaji wa nyimbo za kusifu na kuabudu katika kikundi cha kusifu na kuabudu na Kwaya ya Tumaini ya Kanisa La Pentekoste Tanzania (KLPT).
Ni katika kipindi hicho ndipo alipoanza kuwa na haja ya kukitumia
kipawa cha uimbaji na utunzi wa nyimbo na kufanya huduma ya uimbaji kama
muimbaji wa kujitegemea.
Haja ya kuwa muimbaji wa kujitegemea ilianza kutimia mwishoni mwa
mwaka wa 2012 Neema Decoras alipofanikiwa kurekodi wimbo wake uitwao
“Mungu ni Mwema” katika studio iitwayo Twins Records iliyopo Riverside,
Ubungo jijini Dar es Salaam chini ya mtayarishaji wa muziki aitwaye
Gabriel Maulana.
Mnamo January mwaka wa 2013 mume wake alimpeleka kwa mtayarishaji wa
muziki aitwaye Ambangile Mbwanji anayejulikana sana kama Amba ambaye ni
mmiliki wa studio iitwayo Amba Records iliyoko Ukonga, Jijini Dar es
Salaam, Tanzania.
Katika studio hiyo alifanikiwa kurekodi na kutoa albamu yake ya
kwanza mwezi Julai mwaka wa 2013. Albamu hiyo iitwayo “Milele Nitalisifu
Jina Lako” ina nyimbo nane ambazo zote ameziimba kwa lugha ya Kiswahili.
Nyimbo zilizomo katika albamu hiyo ni; Milele Nitalisifu Jina Lako,
Mikononi mwa Mungu, Unapojaribiwa, Nione Leo, Mungu ni Mwema, Rejea kwa
Yesu, Ninaimba Sifa na Hakika Nimejua.
Akiongozwa na Neno kutoka katika Zaburi 145:1-2 “Ee Mungu wangu,
Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi Jina lako milele na milele. Kila siku
nitakuhimidi, Nitalisifu Jina Lako Milele na Milele” Neema Decoras
anasema kamwe hawezi kuacha kulisifu Jina la Bwana kwa kuwa Bwana ndiye
mkuu mwenye kusifiwa sana.
Kwa sasa Neema Decoras anaishi jijini Dar es Salaam
ambapo amefanya maonyesho yake mengi sana japo yuko tayari kutumika
katika Ibada, Matamasha na Mikutano ya Injili, Semina, Sherehe, na
matukio mbalimbali ambayo yanahubiri Neno la Mungu popote pale ndani na
nje ya Tanzania.
Sikiliza Wimbo wake huu wa Milele Nitalisifu Jina lako Bwana
Wasiliana Nae Sasa
Simu: +255 658 027 515
Email: neemadecoras@yahoo.com