Sunday, February 16, 2014
Namna Uzinduzi wa FRIENDS' BARBECUE(FB) ulivyofana Jijini Mwanza.
Ijumaa ya February 14, 2014 ilikuwa ni siku ya Uzinduzi wa Event ya FRIENDS' BARBECUE(FB) Mkoani Mwanza ambapo shughuli hiyo ilifanyika Royal Sunset Beach Resort maeneo ya Malimbe, Jijini Mwanza.
Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Maandalizi, Noel Mlabwa a.k.a Papaa alisema kuwa |Lengo hasa la kuanzisha FRIENDS' BARBECUE(FB) ni baada ya kuona Vijana wengi wa Kikristo hasa wa Jijini Mwanza hawana sehemu ya kwenda kufurahi kwa pamoja kama Vijana wa kipendwa, hivyo ujio wa Event hii utakuwa unawakutanisha Vijana na kupata Nyama Choma, Vinywaji, Mafundisho mbalimbali ya Kikristo hasa ya vijana na Live Music.
Siku ya tukio watu wengi walionekana kufurahia tukio huku wengine wakiomba tukio hilo liwe ni la Mara kwa Mara.
Sasa Tazama namna mambo yalivyokuwa
![]() |
| Noel Mlabwa akielezea Maana ya FRIENDS' BARBECUE na Umuhimu wake |
![]() |
| Ma Mc wa Event hiyo Sowane Emmanuel na Kabula Siza |
![]() |
| Ma Mc wakipata picha ya pamoja na Best Couple |
![]() |
| Ufunguzi wa Shampein |
![]() |
| Raha ya Shampein tuone mapovu |
![]() |
| Shampein |
![]() |
| Mc Kabula(Kushoto) akiwa na Muimbaji Ester Nyanda |
![]() |
| Happy People |
![]() |
| Ni zaidi ya Furaha |
![]() |
| Best Couple ikipokea Zawadi yao |
![]() |
| Bw. James Kalekwa akiwa eneo la tukio |
![]() |
| Victoria Napiya(Kushoto) akiwa na Deborah Shija(Kulia) wakiwa na Furaha ya kutosha |
![]() |
| Ester Nyanda akiimba |
![]() |
| Papaa Noel Mlabwa akienda sawa wakati Ester Nyanda akiimba |
![]() |
| Mazungumzo na Majadiliano |
![]() |
| Papaa Noel akijibu baadhi ya Maswali kutoka kwa Mc |
![]() |
| Baadhi ya waliohudhuria event hiyo wakiwa makini kufuatilia kilichokuwa kikiendelea |
![]() |
| Bw. James Kalekwa akijibu Maswali kutoka kwa Mc |
![]() |
| Deborah Shija akijibu Maswali kutoka kwa Mc |
![]() |
| Kamati iliyoandaa Friends' Barbecue ikiimba wimbo Maalum |
![]() |
| Mc Sowane Emmanuel akilonga Jambo |
![]() |
| So Happy |
![]() |
| Chakula kwa Tumbo, Tumbo kwa Chakula |
![]() |
| Soft Music ikiendelea |
![]() |
| Watu wakiendelea kula |
![]() |
| Supu pia ilikuwepo |
![]() |
| Mc Sowane na Lilian Mhando |
![]() |
| Baadhi wa waliohudhuria |
![]() |
| Ilikuwa ni Valentine Day |
Friday, February 14, 2014
Wednesday, February 12, 2014
PCT walalamikia kukosa uwakilishi Bunge la Katiba.
| Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania, Askofu David Butenzi, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani), wakati Baraza la Maaskofu wa kanisa hilo lilipotoa tamko lao kuhusu kutopata nafasi |
Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania (PCT), limesema
limefedheheshwa na kusikitishwa kwa kunyimwa uwakilishi wa kushiriki
katika Bunge maalum la Katiba licha ya kuwasilisha majina ya wajumbe
wake.
Limesema kitendo cha kushindwa kupewa fursa ya kushiriki katika Bunge hilo, ni kuwanyima haki za msingi Watanzania wengi wanaowakilishwa na Baraza hilo, kama ilivyo kwa Watanzania wengine.
Akisoma tamko la baraza hilo mbele ya waandishi wa habari jana, baada ya kufikiwa katika mkutano ulioshirikisha Maaskofu wakuu wa Madhehebu ya Kipentekoste jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa PCT, David Mwasota, alisema wameamua kutoa tamko hilo ili kuonyesha namna ambavyo wamesikitishwa na kitendo hicho.
“Tumewaita leo (jana) ili mtusaidie kufikisha masikitiko yetu kwa viongozi, Watanzania na waamini wa Kipentekoste kutokana na kitendo cha serikali yetu tunayoiheshimu, kuipenda na kuiombea, kwa kutubagua na kututenga katika bunge maalum la Katiba, huku tukiwa ni miongoni mwa taasisi kubwa za kidini na makundi mengine ya kijamii,” alisema na kuongeza:
“Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Rais aliagiza makundi mbalimbali ya kijamii na taasisi za kidini kupendekeza majina ya watu wanaoona wanafaa kuchaguliwa kushiriki katika bunge maalum la Katiba na kwa kuzingatia wingi wa wanachama wetu tulipendekeza majina tisa ya watu tulioona wanafaa kutuwakilisha, lakini cha kushangaza hakuna hata mmoja aliyeteuliwa.”
Aidha, aliongeza kuwa ikiwa serikali itaendelea kunga`ng`ania msimamo wake wa kutaka wajumbe wa baraza la PCT wasihusike katika Bunge hilo, Baraza litaitisha mkutano mkuu wa dharura wa kitaifa utakaojumuisha maaskofu wote wa kitaifa, Kanda na jimbo, mitume na manabii na wachungaji zaidi ya 30,000 ili kutafakari kwa pamoja na kuamua hatua za kuchukua.
Mjumbe wa TCP ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia Kakobe, alisema Katiba ni haki ya Watanzania wote hivyo haoni sababu ya wengine kubaguliwa.

- Nipashe -
Monday, February 10, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)