Advertise Here

Wednesday, February 19, 2014

Safu ya James Kalekwa; Mwisho tangu Mwanzo: Usuri wa njozi kwenye maisha binafsi. - Part 2

James Kalekwa
Msisitizo wa mwenendo wa somo:
Kusudi – ni sababu kuu ya kuwepo kwako. Hii hujibu swali la “Kwanini ninaishi?” mfano: Ninaishi ili kuudhihirisha utukufu wa Mungu kwenye kizazi changu.

Maono – ni taswira/picha kubwa uionayo juu ya mwisho wa maisha yako. Ni mkusanyiko wa mwisho wa maisha yako. Hii hujibu swali la “ninakwenda wapi?” mfano: … Kumtukuza Mungu kwa kufanya ugunduzi, uvumbuzi na utatuzi chanya wa mahitaji ya kizazi changu.

Dhamira – ni namna gani utafanya ili kuyafikia maono hayo kivitendo. Hii hujibu swali la “Namna gani nitatekeleza?” Mfano: … Kufungua taasisi ya utafiti wa uwezo wa mwanadamu na uelimishaji wa vijana.

N.B Unaweza kuwa na dhamira zaidi ya moja… Hakuna ukomo ilimradi tu dhamira zinafanikisha ufikiaji wa maono yako.

Malengo/Mipango – ni kuweka namna/njia za kivitendo na zinazopimika ili kufanikisha dhamira yako/zako Mfano: … Kufanya usajili wa taasisi yangu ifikapo March 28 ili kuanza utendaji rasmi.

Mkakati – ni mchanganuo wa hatua kwa hatua na uratibu wa rasilimali ili kufanikisha malengo yako. Hii hujibu maswali mengi “Nifanye nini, nifanye wapi, wakati gani?...” Mfano: …

Taswira: Chombo cha Kusudi
Moyoni mwangu nimewiwa kuweka jambo hili kwa msisitizo mkubwa sana juu ya “Chombo cha kusudi”. Jifunze kutoka kwenye taswira hiyo na kutafsiri kwenye maisha yako binafsi.

Usuri ni nini?
Usuri (essence) ni jibu moja juu ya mjumuiko wa maswali mengi juu ya jambo, hoja, kitu au mtu fulani. Ni mara nyingi sana utawasikia watu wakitoa maelezo ya kina juu ya utumizi wa kifaa fulani cha umeme. Na kwa wanafunzi ni jambo lililozoeleka kukariri tafsiri (definition) na sifa za kitu au jambo fulani. Kuna aina ya watu ambao huvutika kufahamu sifa za kimwonekano za jambo fulani pasipo kujua tafsiri au utumizi wake.

Kwa ujumla wake, usuri hujibu maswali yahusianayo na maana na tafsiri ya jambo, sifa za kimwonekano, utumizi na huenda mbali na kujibu kwanini jambo fulani lipo na ni kwanini lipo vile lilivyo!
Kwahiyo, usuri wa maono si tafsiri/maana ya maono, si sifa za maono, si mwonekano na wala si utumizi wa maono…. Bali ni mjumuiko wa hayo yote! Karibu ujifunze kwa upana na urefu ujumla wa jambo hili muhimu sana katika maisha ya mwanadamu yeyote.

Njozi (Maono) huleta “mipaka” ya maisha
Ili kuupanua wigo wa kujifunza na kuvuta maarifa kutoka katika andiko hili, nitaleta tafsiri mbalimbali za lugha ya kiingereza na kuzitafsiri ili kutusaidia kupata upana wa maana ya hekima hizi.
“Where there is no revelation, people cast off restraint…”  (NIV)
“Where there is no prophetic vision the people cast off restraint…” (ESV)
Tafsiri yangu ya ujumla “Pasipo maono, watu hukosa/huvuka mipaka…”
Ukisoma kwenye historia ya agano la kale utaona kuwa miji mikubwa ilikuwa imezingirwa na kuta kubwa sana kuilinda miji hiyo; Mfano mji wa Yeriko, Yerusalemu. Hata kwenye historia ya kale, nchi kama China ya kale (Ancient China) utaona ujezi wa ukuta wa namna hiyo, ukuta mkuu wa China (The Great wall of China) ni moja kati ya kuta maarufu sana za miji.

Sababu kubwa ya ujenzi wa kuta hizo ilikuwa ni kuleta ulinzi wa uhakika kwa waishio ndani ya kuta hizo dhidi ya maadui walio nje ya kuta hizo. Ukuta uliweka mipaka baina ya walindwao dhidi ya wasiolindwa na ukuta huo; raia dhidi ya maadui wa jamii husika.

Mhubiri 10:8, “Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.”
Njozi huweka bayana mipaka ya mtu ama jamii ibebayo njozi hiyo. Kimsingi, njozi kama ilivyo ni mipaka tayari. Njozi inaweka ukuta wa muda na wakati (season) ya kukamilika kwake, kwahiyo unapaswa kujua kuwa huna muda wote duniani kutimiliza njozi hiyo… Njozi imefungwa ndani ya muda. Kwenye kitabu changu cha kwanza nimeeleza kwa upana na kwa lugha nyepesi kuhusu sifa ya muda ya njozi. Njozi zote zina ukomo wa muda na kuna sababu katika hilo.
Ukisoma Habakuki 2:3, “ Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwakuwa haina budi kuja, haitakawia.” Utaona Mungu anasema na huyu ndugu kitu cha msingi sana juu ya “wakati ulioamriwa” na anasisitiza kuhusu mitazamo miwili; mtazamo wa kibinadamu na mtazamo wa kiMungu.

Kwamba katika macho ya kibinadamu njozi inaweza kuonekana inakawia lakini katika macho ya Mungu ipo katika wakati kwakuwa haina budi kuja. Hebu tazama hii sentensi ambayo Roho Mtakatifu aliweka kwa msisitizo sana ndani ya moyo wangu “…ijapokawia, ingojee; kwakuwa haina budi kuja, haitakawia.”.

Ukitazama utagundua hii ni kama sentensi yenye kujipinga yenyewe kwasababu inazungumza mawazo mawili tofauti yasiyoafikiana “… ijapokawia…. haitakawia”. Kitu gani ninataka uone katika eneo hili ni tofauti ya kutazama muda wa njozi iliyomo ndani ya mwanadamu na Mungu. Isaya 55:8-9, “Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu ya nchi.

Kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.” Mungu anataka kusema namna ya kufikiri kwake ilivyo tofauti na juu ya namna yetu. Rejea Mhubiri 3:1, “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.” Na muendelezo wa mifano ya kila jambo na wakati wake mpaka mstari wa 8.

Somo hili litaendelea Jumatatu Ijayo
  
Mafundisho haya yameandaliwa na James Kalekwa
Mwanataaluma, Mwandishi wa vitabu na Mwalimu wa Neno la Mungu
+255 714 762 669
+255 754 917 764

Sunday, February 16, 2014

Tazama wimbo wa Joepraize - Mighty God.

Namna Uzinduzi wa FRIENDS' BARBECUE(FB) ulivyofana Jijini Mwanza.

Ijumaa ya February 14, 2014 ilikuwa ni siku ya Uzinduzi wa Event ya FRIENDS' BARBECUE(FB) Mkoani Mwanza ambapo shughuli hiyo ilifanyika Royal Sunset Beach Resort maeneo ya Malimbe, Jijini Mwanza.

Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Maandalizi, Noel Mlabwa a.k.a Papaa alisema kuwa |Lengo hasa la kuanzisha FRIENDS' BARBECUE(FB) ni baada ya kuona Vijana wengi wa Kikristo hasa wa Jijini Mwanza hawana sehemu ya kwenda kufurahi kwa pamoja kama Vijana wa kipendwa, hivyo ujio wa Event hii utakuwa unawakutanisha Vijana na kupata Nyama Choma, Vinywaji, Mafundisho mbalimbali ya Kikristo hasa ya vijana na Live Music.

Siku ya tukio watu wengi walionekana kufurahia tukio huku wengine wakiomba tukio hilo liwe ni la Mara kwa Mara.

Sasa Tazama namna mambo yalivyokuwa
Noel Mlabwa akielezea Maana ya FRIENDS' BARBECUE na Umuhimu wake
Ma Mc wa Event hiyo Sowane Emmanuel na Kabula Siza
Ma Mc wakipata picha ya pamoja na Best Couple
Ufunguzi wa Shampein
Raha ya Shampein tuone mapovu
Shampein
Mc Kabula(Kushoto) akiwa na Muimbaji Ester Nyanda
Happy People
Ni zaidi ya Furaha
Best Couple ikipokea Zawadi yao
Bw. James Kalekwa akiwa eneo la tukio
Victoria Napiya(Kushoto) akiwa na Deborah Shija(Kulia) wakiwa na Furaha ya kutosha
Ester Nyanda akiimba
Papaa Noel Mlabwa akienda sawa wakati Ester Nyanda akiimba
Mazungumzo na Majadiliano
Papaa Noel akijibu baadhi ya Maswali kutoka kwa Mc
Baadhi ya waliohudhuria event hiyo wakiwa makini kufuatilia kilichokuwa kikiendelea
Bw. James Kalekwa akijibu Maswali kutoka kwa Mc
Deborah Shija akijibu Maswali kutoka kwa Mc
Kamati iliyoandaa Friends' Barbecue ikiimba wimbo Maalum
Mc Sowane Emmanuel akilonga Jambo
So Happy
Chakula kwa Tumbo, Tumbo kwa Chakula
Soft Music ikiendelea
Watu wakiendelea kula
Supu pia ilikuwepo
Mc Sowane na Lilian Mhando
Baadhi wa waliohudhuria
Ilikuwa ni Valentine Day
Very funny! Vick akinywa Shampein kwenye chupa


Wapo pia waliokuwa wakilia Jikoni

Hapo kila mtu alikuwa busy kupiga picha
Kaa tayari kwa FRIENDS' BARBECUE(FB) nyingine baada ya uzinduzi rasmi wa Event hiyo jijini Mwanza.

Friday, February 14, 2014

Alichokiandika Mwimbaji John Lisu kuhusu watoto wake Mapacha watatu.

Wednesday, February 12, 2014

PCT walalamikia kukosa uwakilishi Bunge la Katiba.

Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania, Askofu David Butenzi, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani), wakati Baraza la Maaskofu wa kanisa hilo lilipotoa tamko lao kuhusu kutopata nafasi
Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania (PCT), limesema limefedheheshwa na kusikitishwa kwa kunyimwa uwakilishi wa  kushiriki katika Bunge maalum la Katiba licha ya kuwasilisha  majina ya wajumbe wake.

Limesema kitendo cha kushindwa  kupewa fursa ya kushiriki katika Bunge hilo,  ni kuwanyima haki za msingi Watanzania wengi wanaowakilishwa na Baraza hilo, kama ilivyo kwa Watanzania wengine.


Akisoma tamko la baraza hilo mbele ya waandishi wa habari jana, baada ya kufikiwa katika mkutano ulioshirikisha Maaskofu wakuu wa Madhehebu ya Kipentekoste jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa PCT,  David Mwasota,  alisema wameamua kutoa tamko hilo ili kuonyesha namna ambavyo wamesikitishwa na kitendo hicho.


“Tumewaita leo (jana) ili mtusaidie kufikisha masikitiko yetu kwa viongozi, Watanzania  na waamini wa Kipentekoste kutokana na kitendo cha serikali yetu tunayoiheshimu, kuipenda na kuiombea, kwa kutubagua na kututenga katika bunge maalum la Katiba, huku  tukiwa ni  miongoni mwa taasisi kubwa za kidini na makundi mengine ya kijamii,” alisema na kuongeza:


“Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Rais aliagiza makundi mbalimbali ya kijamii na taasisi za kidini kupendekeza majina ya watu wanaoona wanafaa kuchaguliwa kushiriki katika bunge maalum la Katiba na kwa kuzingatia wingi wa wanachama wetu tulipendekeza majina  tisa ya watu tulioona wanafaa kutuwakilisha, lakini cha kushangaza hakuna hata mmoja aliyeteuliwa.”


Aidha, aliongeza kuwa ikiwa serikali itaendelea kunga`ng`ania msimamo wake wa kutaka wajumbe wa baraza la PCT wasihusike katika Bunge hilo, Baraza litaitisha mkutano mkuu wa dharura wa kitaifa utakaojumuisha maaskofu wote wa kitaifa, Kanda na jimbo, mitume na manabii na  wachungaji zaidi ya 30,000 ili kutafakari kwa pamoja na kuamua hatua za kuchukua.


Mjumbe wa TCP ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la  Full Gospel  Bible Fellowship,  Zacharia Kakobe,  alisema Katiba ni haki ya Watanzania wote hivyo haoni sababu ya wengine kubaguliwa.

- Nipashe -