Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Engeneer Evarist Ndikiro akitoa heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu |
Lilikuwa si jambo la kuamini kwa haraka kama kweli Askofu Dr. Mosses Kulola katutoka, lakini ilibidi kukubaliana na ukweli huo kwani wakati huu watu waliweza kuushuhudia mwili wa Marehemu Babu/Baba yetu ukiwa katika Jeneza.
Mwili wa Marehemu ukiwa Uwanja wa CCM Kirumba |
Watu wengi sana walifurika Uwanja wa CCM Kirumba japokuwa leo ilikuwa ni Siku ya kazi. Kila alitamani ajionee kwa macho yake ili aamini ukweli uliopo ya kuwa hatuko tena na Askofu Dr. Mosses Kulola.
Mch. Dastan Mboya akieleza namna alivyomfahamu Askofu Mosses Kulola |
Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama mbalimbali na Viongozi mbalimbali wa Makanisa tofauti tofauti waliweza kufika Uwanja wa CCM Kirumba ili kutoa heshima zao za mwisho kwa Mwili wa Marehemu wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Engeener Evarist Ndikiro.
Ndugu wa Marehemu wakiwa Uwanjani |
Maaskofu, Wachungaji na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mwanza walifika Uwanjani hapo, pia alikuwepo Mwl. Christopher Mwakasege kutoka Mkoani Arusha akiongozana na baadhi ya wanahuduma wa MANA.
Umati wa watu |
Zoezi la kutoa heshima za Mwisho lilianza mida ya Saa 2:30 Asubuh, na lilikamilika mida ya Saa 10 Jioni, huku watu wakipata fursa ya kusikiliza Wasifu wa Askofu Dr. Mosses Kulola pamoja na viongozi mbalimbali kutoa rambirambi zao pamoja maneno machache namna wanavyomfahamu Marehemu Askofu Mossas Kulola.
Bango lenye picha ya Marehemu Askofu dr. Mosses Kulola |
Sikiliza hapa chini Neno la Mungu lililotolewa leo katika kuuaga mwili wa Marehemu Askofu Dr. Mosses Kulola
Na huu hapa chini ndio Wasifu wa Askofu Dr. Mosses Kulola uliotolewa na Ndugu Limbu katika Uwanja wa CCM Kirumba
Kauli ya Mwl. Christopher Mwakasege akiwa Uwanja wa CCM Kirumba wakati wa kuwasilisha Rambirambi kwa Familia ya Marehemu
Kauli ya Askofu Eugene Murisa wa Kanisa la High Way of Holliness Cathedral akitoa rambirambi kwa Familia ya Marehemu
Mwili wa Marehemu utazikwa kesho katika Kanisa la EAGT Bugando kuanzia mida ya Saa 2:00 Asubuhi. Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina lake libarikiwe.