James Kalekwa |
Utangulizi
wa somo:
Mathayo 7:24-27
“Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na
mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha,
mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana
misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu
asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya
mchanga; mvua ikanyesha, afuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile,
ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.”
Kwa muda mrefu nimekuwa nikizunguka sehemu mbalimbali, makanisani na
mikusanyiko, nikifundisha na kuwezesha semina, makongamano ndani ya nchi ya
Tanzania. Moja ya msisitizo wangu ni kwamba wokovu si dini, wokovu si tamaduni
au mapokeo (tradition).
Hii ni baada ya uchunguzi wangu wa kina na mapito
kwenye maisha yangu binafsi ambapo niligundua ya kwamba kuna uelewa tofauti
sana miongoni mwa watu juu ya wokovu (hata miongoni mwa watu waliookoka).
Uelewa wako juu ya jambo fulani, ndiyo huamua kiwango cha maisha yako juu ya
jambo hilo… Kama una uelewa mdogo, uelewa potofu, uelewa finyu… Ndivyo kiwango
cha maisha yako kitakavyokuwa… “Your attitude determines your altitude.”
Kama
unataka kutambua uelewa wa mtu binafsi kuhusu wokovu, tazama maisha yake ndani
ya wokovu au sikiliza msimamo wake kuhusiana na wokovu… Ukikuta ni maisha ya
dini, mapokeo/tamaduni… Basi tambua huo ndiyo uelewa wake. Kama asemavyo mfalme
Sulemani “Maana aonavyo mtu nafsini mwake, ndivyo alivyo.”
Pia, kuna watu ambao bado hawajaokoka na hawataki kuokoka kwasababu bado
hawajapewa taarifa sahihi kuhusu wokovu. Hii inamaanisha ya kwamba uelewa wao
juu ya wokovu, umeyaathiri maisha yao. Laiti kama angetokea mtu wa
kuwasikilizisha habari njema, basi
uelewa wao ungebadilika na kisha wangeuelekea wokovu – Mungu atusaidie
tuwasikilizishe wengine taarifa sahihi kuhusu wokovu.
Naamini unaelewa kuna taasisi au makusanyiko ya watu ambao wanajitahidi
kujimilikisha wokovu kuwa ni mali yao binafsi yaani kama wewe si mshiriki au
mmoja wa wanachama wao basi ni dhahiri kwamba wewe hujaokoka – hujapata wokovu!
Wao huamini hakuna mtu mwingine aliyeokoka isipokuwa aliye ndani ya taasisi au
makusanyiko yao… Pia upande wa pili
vivyo hivyo kuna wale ambao wamekuwa na juhudi nyingi sana kuukataa wokovu… kwa
wao wokovu si dini yao, wokovu si utamaduni wao...
Kwa mtazamo wao, kuokoka ni
kujifuta ushirika katika taasisi au makusanyiko yao. Pande zote hizi mbili,
wanaoumiliki na wanaoukataa wokovu, wote wapo katika tatizo moja: tatizo la
uelewa juu ya wokovu!
Ni heshima kubwa sana mbele za Mungu na mbele zako kwamba ninakukaribisha
kujifunza ili kuulekeza uelewa wako juu wokovu. Karibu na uwajulishe na wengine
juu ya mafundisho haya! Karibu na Mungu wa amani, Yesu Krsito aliye asili ya
wokovu, akufungue macho yako ya ndani upate kuelewa mafundisho haya.
Tujenge
uelewa wa pamoja
Naomba
nikurejeshe kwenye andiko nililoanza nalo hapo awali:
Mathayo 7:24-27
“Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na
mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha,
mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana
misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu
asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya
mchanga; mvua ikanyesha, afuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile,
ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.”
Ili kuweza
kutembea pamoja katika mfululizo wa mafundisho haya, ni vyema tukajenga uelewa
wa pamoja juu ya andiko hilo amabalo ndilo msingi wa mafundisho haya. Bwana
Yesu Kristo anazungumza juu ya wajenzi wa aina mbili, mjenzi mwenye busara na
mjenzi mpumbavu. Ukitazama kwa umakini kwenye maandiko hayo utagundua ya kwamba
maisha ya wajenzi hawa waiwili twaweza kuyafupisha hivi:
Mambo
waliyofanana
|
Mambo waliyotofautiana
|
|
Mwenye akili
|
Mtu mpumbavu
|
|
1.
Wote walifanya shughuli ya ujenzi wa nyumba
|
Alijenga nyumba juu ya Imwamba
|
I
Alijenga nyumba kwenye mchanga
|
2. Wote walipata misukosuko
inayofanana kwenye nyumba zao.
|
Nyumba yake haikuanguka
|
Nyumba yake ilianguka
|
Kilichoamua
tofauti ya hawa ndugu ni kitu kimoja tu, nacho ni mahali walipochagua kujenga
nyumba zao- mmoja alijenga kwenye mwamba na mwingine alijenga kwenye mchanga.
Biblia imekaa kimya juu ya viwango vya ubora vya nyumba hizi, lakini imetueleza
kwamba japo zilipitia misukosuko inayofanana lakini nyumba moja ilianguka na
nyingike ilidumu (haikuanguka)…
Kwanini nyumba moja ianguke na nyingine
isianguke wakati zote ni nyumba na zimepitia hali zinazofanana? Jibu ni rahisi
sana, tofauti imeamuliwa na mahali nyumba zilipojengwa: kwenye mwamba na kwenye
mchanga.
Naomba
usisahau kwamba Bwana Yesu alitumia wajenzi kama mfano tu kuelezea dhana
tofauti kabisa… Lengo lake lilikuwa ni ili kwamba watu waweze kujenga taswira
(mental picture) ya anachokizungumza. Pia, ni hekima kama tukiirejea dhana ya
Bwana Yesu huku tukiwa na taswira ya ndugu wajenzi ndani ya mawazo yetu.
Yesu
anasema “mtu asikiaye maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa…” kisha
anasema, “Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa…” Kwahiyo
basi, dhana iliyo ndani ya moyo wa Bwana Yesu ni: kusikia maneno na
kuyachukulia hatua (kuyatenda au kutoyatenda).
Nitamanicho kiumbe ndani ya moyo
wako na maisha yako ni kwamba ni wajibu wako kusikia neno na kulitenda kwasababu
ni kwa njia hiyo tu ndiyo utafanana na mtu aliyejenga juu ya mwamba.
Kwakuwa
sasa tumejenga uelewa wa pamoja, naomba uniruhusu nikuchukue kwenye mambo ya
msingi (ambayo ni mwamba) yatakayokusaidia kuukulia wokovu… Kumbuka tunajenga
wokovu wetu kwenye neno la Mungu na si mitazamo ya kidini, mapokeo au mifumo ya
kimazoea. Ninaamini Mungu ana jambo kwaajili yako unapoendelea kufuatilia
maswala haya ya msingi!
Somo litaendelea Jumatatu Ijayo....
Mafundisho haya yameandaliwa na James Kalekwa
Mwanataaluma, Mwandishi wa vitabu, na Mwalimu wa Neno la Mungu
+255 714 762 669
+255 754 917 764
jameskalekwa@gmail.com
Mwanataaluma, Mwandishi wa vitabu, na Mwalimu wa Neno la Mungu
+255 714 762 669
+255 754 917 764
jameskalekwa@gmail.com