Mwl. James Kalekwa |
Utangulizi wa Somo:
Kwasababu
ya mazoea ya kufanya maamuzi mara kwa mara, watu wengi wamejikuta wamenaswa kwenye mtego wa
kutofahamu upana, kina na ukubwa wa jambo hili muhimu. Kila mwanadamu hufaya
maamuzi ya kudumu au ya kitambo (muda mfupi); maamuzi ya mara moja (sudden) au
yale yachukuayo muda mrefu kuyafikia. Kwa ujumla wake, maisha ya mwanadamu
hutawaliwa na maamuzi. Mfano kutembelea blog hii ni uamuzi, kusoma fundisho
hili kwenye blog ni uamuzi, kuamka toka kitandani ni uamuzi, ndoa ni uamuzi,
kuokoa ni uamuzi… Ungeweza kuwa tofauti na hivyo ulivyo, lakini sivyo kwasababu
ya maamuzi.
Ni
jambo la msingi sana kufahamu pia ya kwamba maamuzi huathiri si tu maisha ya
mtu husika bali huyagusa mpaka maisha ya wale wanaomuhusu sawasawa na nafasi
yake – familia, jamaa, jamii, taifa, taasisi n.k
Kwakuwa
maamuzi ni jambo la Muhimu kiasi hiki, fuatana nami kwenye mfululizo wa
mafundisho haya juu ya maamuzi ili uwe na ufahamu juu ya nini unakiendea kila
fursa ya kufanya maamuzi inapojihudhurisha mbele yako. Watu wasio na maarifa na
ufahamu hukutwa na kushangazwa na mambo (they
are caught by surprise) pindi yanapoanza kutokea. Ni maombi yangu kwa Mungu
kwamba Roho Mtakatifu akusaidie kuyatambua yote haya, kwa jina la Yesu Kristo!
Dhana ya Maamuzi kwenye Neno la Mungu
Yoeli 3:14
“Makutano makubwa, makutano makubwa, wamo
katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya BWANA i karibu, katika bonde
la kukata maneno.”
1 Korintho 6: 5
“Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo,
kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu
zake?”
Matendo ya Mitume 24:22
“Basi Feliki aliwaahirisha, kwasababu alijua
habari za Njia ile kwa usahihi zaidi, akasema, Lisia jemedari atakapotelemka nitakata maneno yenu.”
Mith. 16:10
“Kukata maneno huwa
katika midomo ya mfalme; Kinywa chake hakitakosa katika hukumu.”
Nabii
Yoeli anatutambulisha dhana muhimu sana kwenye maisha ambayo amechagua kuiita
“kukata maneno”. Nimeambatanisha mistari mingine ili kupana wigo wa uelewa juu
ya dhana ya kukata maneno. Ukiisoma mistari inayotangulia na inayofuata baada
ya hiyo niliyoambatanisha hapo, utang’amua mara moja ya kwamba kukata maneno si
dhana mpya bali ni neno linalowasilisha maana ya kufikia maamuzi ya kimahakama
(kunapokuwa na pande mbili zinazokinzana na inatakiwa pande hizo zifike uelewa
wa pamoja “consensus” juu ya jambo
fulani); kufikia neno la mwisho juu ya, ama kuhitimisha mjadala unaoendelea juu ya hoja fulani… Kwa
lugha rahisi na ya kueleweka kwa wengi, maelezo yote hayo yaliyotangulia juu ya
dhana ya kukata maneno yanaweza kufupishwa kwa neno hili: kufanya maamuzi
Pia
ukitazama kwa umakini utagundua ya kwamba Yoeli anatambulisha mahali “venue” pa kufanyia maamuzi. Si kila
mahala ni maalum kwa maamuzi… La hasha! Kuna sehemu maalum kwa shughuli hii, na
hiyo sehemu inaitwa “Bonde la Kukata
maneno”. Ili tuweze kumuelewa vyema
Yoeli, basi karibu ujifunze juu ya dhana ya mihula mitatu kwenye maisha ya
mwanadamu ambayo hiyo itatupa kujua wajibu wetu katika zoezi hili Muhimu…
Kufanya maamuzi!
Somo litaendelea Jumatatu Ijayo.....
Somo limeandaliwa na:
Mwl. James Kalekwa
0714 762669/0754917764
Email: jameskalekwa@gmail.com