MTUME Moses Bakilana amesisitiza kuwa, unabii uliotolewa na
Mchungaji Stephen Umaru Bugwegwe wa Uganda, kwamba kati ya mwaka 2012 na 2015
jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania, litamezwa na bahari utatimia kutokana na
watu, wakiwemo viongozi wa kanisa kuonekana kuupuuza unabii huo.
Juni mwaka jana, Mchungaji Bugwegwe alikuwa nchini Tanzania ambapo alidai kuwa alileta ujumbe usemao: ‘Tanzania Itubu kwa maovu yake’. Alidai kuwa Kanisa la Tanzania ambalo lilitegemewa kuwa lingekuwa msaada kwa sasa ni kama Yona kwani limemezwa na joka na linatakiwa kutapikwa.
Alisema viongozi wengi wa kanisa waliotegemewa kusimama na kuomba kwa ajili ya Taifa na kukemea maovu wameuza kanisa kwa
wanasiasa kwa ajili ya kutafuta misaada. Alidai kuwa, viongozi wa kanisa
wanaenda kwa waganga kutafuta nguvu za ushirikina, na wamejaa kiburi wakionywa
hawasikii. Mchungaji Bugwegwe alisema kuwa, baadhi ya wachungaji na
viongozi wa kanisa kazi yao kubwa imekuwa nin kuangalia sadaka na matoleo tu na
sio roho za watu.
“Viongozi hao hao wa dini (kanisa) ni washerati, wanafanya uzinzi na kusema uongo. Wanashindwa kusimama katika nafasi zao ili kuikomboa nchi na kuiombea rehema”, alisema Mchungaji Bugwegwe katika ujumbe huo uliosambazwa kwa watu mbalimbali.
Aliongeza kusema : “Nchi iko katika ukiwa na matatizo makubwa kwa sababu waliotegemewa kuisimamia ndio walioiuza. Mungu amechukizwa sana na mauaji ya albino kwa ajili ya kafara kwa Shetani. Watu wameabudu miungu, wamejiuza kwa Shetani, wachawi na ulozi. Wanasiasa nao badala ya kumtegemea Mungu wanategemea wachawi na ulozi kwa sababu wamekosa msaada na ushauri wa viongozi wa kiroho. Kanisa halina mwelekeo wala nguvu za Mungu tena kwa sababu limeshiriki maovu.
Kutokana na haya Watanzania wasipotubu matukio yafuatayo
yatatokea katika kipindi cha miaka mitatu, yaani 2012 hadi 2015; njaa kubwa
isiyo na mfano wake; magonjwa yasiyo na tiba; vita itakayowafanya Watanzania
kuikimbia nchi yao na kuwa wakimbizi, jiji la Dar es Salaam kumezwa kabisa na
bahari, na Mungu ataipa nchi hii taifa lingine liitawale na kuufaidi utajiri
aliokuwa amewaandalia Watanzania”. Alisema kinachotakiwa ni Watanzania kufanya toba ya kweli,
kutiririsha machozi ya kweli, kuomboleza na kuacha kabisa maovu. Alinukuu 2
Nyakati 7:14.
Tangu ujumbe huo utolewe kumefanyika toba mara mbili tu;
Moshi na Arusha. Lakini hakuna matokeo makubwa, wachungaji na maaskofu hawakuitikia wito. Pale Moshi Toba ilifanya kwenye uwanja wa Mashujaa, na alikuwapo pia Waziri Mkuu mstaafu, Frederick
Sumaye. Kule Arusha walifanya Redio Safina pale uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Ilikuwa toba ya ajabu lakini jambo hili
linatakiwa lifanyike nchi nzima.
Chanzo: Funguka Sasa
Chanzo: Funguka Sasa