Advertise Here

Saturday, November 17, 2012

Mapadre wa Kanisa Katoliki Iringa wavamiwa na kujeruhiwa vibaya.

PAROKO wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani, wilayani Iringa Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake Herman Myalla (36) wamenusurika kufa baada ya kuvamiwa na majambazi waliokuwa na silaha za moto, mapanga na nondo.
Picture
Paroko Angelo Burgeo
 Mbali na kupigwa risasi katika ubavu wake wa kushoto na kujeruhiwa vibaya katika tukio hilo lililotokea majira ya 4.45 usiku wa kuamkia jana, Padri Burgeo alijeruhiwa vibaya nyuma ya kichwa chake baada ya kupigwa na nondo.

Akizungumza na wanahabari katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambako viongozi wamelazwa kwa ajili ya matibabu, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Faustine Gwanchele alisema Padri Myalla amejeruhiwa vibaya kichwani baada ya kupigwa kwa panga na nondo.
Picture
Msaidizi wa Paroko, Bw. Herman Myalla
 "Walifikishwa majira ya saa sita usiku wa kuamkia jana, na wakaanza kupatiwa matibabu wanayoendelea nayo mpaka sasa," alisema na kuongeza kwamba Padri Bergeo alianza kufanyiwa upasuaji jana ili kuondoa vipande vya risasi vilivyopo ndani ya mwili wake.

Tukio hilo limetokea ikiwa siku moja tu baada ya mlinzi wa Kanisa Katoliki Kihesa Iringa Mjini, Bathelomeo Nzigilwa (64) kujeruhiwa vibaya na majambazi waliovunja kanisa hilo na kufanikiwa kuiba mali mbalimbali zikiwemo fedha taslimu zaidi ya Sh 500,000.

 Dk Gwanchelle alisema hali ya Nzigilwa ni mbaya kwasababu majambazi waliomjeruhi walimvunja mfupa wa sehemu ya nyuma ya kichwa chake.

Friday, November 16, 2012

Kanisa Katoliki Parokia ya Kihosa lavamiva. Mlinzi ajeruhiwa vibaya.

Muonekano wa Nje wa Kanisa Katoliki Porokia ya Kihesa
WATU wasiofahamika usiku wa kuamkia Jana wamevamia Kanisa Katoliki Parokia ya Kihesa Jimbo la Iringa, Mkoani Iringa na kuiba baadhi ya mali huku mlinzi wa Kanisa hilo Bathlomeo Nzigilwa akijeruhiwa vibaya na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa.
 
Akizungumzia tukio hilo Sista Lucy Grace Mgata amesema aligungua kuwa kunauvamizi majira ya  alfajiri alipofika kanisani hapo kwa ajili ya ibada ya Misa za kila siku zinazoanza saa 12:00 asubuhi.

“Mimi nilifika hapa kanisani saa 11:40 alfajiri, na nilipofungua mlango wa kanisa kwa ajili ya misa nilishangaa mlango ukiwa wazi na kumuona  mlinzi amekaa kwenye kiti huku kichwa chake kikiwa kimeinamishwa chini na kufunikwa kofia, nilijua amelala kumbe alikuwa ameumizwa na hajitambui," Alisema Sista Mgata. 
Ndani ya Ofisi baada ya Uharibifu
Amesema  alipomsogelea mlinzi huyo aliona damu inatiririka chini na mwili wake ukiwa umelowa kwa damu na hapo ndipo alipokwenda kugonga nyumba ya padre kutoa taarifa.

Pamoja na kuvunjwa kwa Kanisa hilo ofisi ya parokia nayo ilivunjwa huku vitabu, na kumbukumbu mbalimbali zikiwa zimechanwa na kuwa mavazi ya ibada na vifaa mbalimbali vya ibada vimeharibiwa vibaya,  Taberenakulo ndogo nayo ikiharibiwa, msalaba kuvunjwa pamoja na Hostia Takatifu zikimwagwa kila mahali.

Damu zilizovuja baada ya mlinzi kupigwa
Sista Mgata  amesema hela za watumishi wa Artare walizokuwa wakichangishana pamoja na fedha za chama cha kitume cha utume wa Fatima zimechukuliwa japo bado hazijajulikana ni kiasi gani.

“Pia wamechukua hela ambazo watumishi wa artare walikuwa wakichangishana kwa ajili ya matumizi ya umoja wao, na fedha za chama cha kitume cha utume wa Fatima nazo wamechukua ingawa sijajuwa ilikuwa ni kiasi gani mpaka wao wenyewe waje waeleze kulikuwa na shilingi ngapi," Alisema sista Mgata.
Muuguzi mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa Rustica Tung'ombe akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mlinzi aliyeumizwa na kufukishwa hospitalini hapo leo
 Kwa upande wake Katekista Agustino Luhama mhudumu wa ofisi ya Parokia alisema hela anazozikumbuka kwa harakaharaka ambazo zimechukuliwa na wavamizi hao ni zaidi ya shilingi laki tano.

“Hela ninazozikumbuka kwa harakaharaka ambazo zimechukuliwa ni zaidi ya shilingi laki tano lakini zingine sijapata idadi kwa sababu nilikuwa sijazijumlisha na zingine nilizipokea jana kutoka kwa waamini mbalimbali” alisema Kat. Luhama.

Padre Aloyce Mdemu ambaye pia ni Makamu wa Askofu wa jimbo hilo alisema bado ni mapema kujua thamani ya uharibifu uliofanyika kwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi wa vifaa vingine na maeneo mengine ambayo huenda hayajagundulika.
Mlinzi aliyejeruhiwa akiwa hospitali
“Ni kweli tukio hili limetokea na kutushtua sana hata kuumizwa nuzura kuuawa mlinzi wetu lakini bado ni pame sana kujua thamani ya uharibifu wa vitu vyote vilivyoharibiwa kwa sababu tunaendelea na uchunguzi wa vitu vingine na maeneo mengine ambayo huenda nayo yameharibiwa na hayajajulikana. Tutakapokuwa tumekamilisha, taarifa zitatolewa” alisema Pd. Mdemu.

Hata hivyo Muuguzi mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Iringa Rustica Tung’ombe alikiri kumpokea majeruhi ambaye ni mlinzi wa kanisa hilo na kusema kuwa hali yake ni mbaya japo kuwa anaendelea kupatiwa matibabu.

“Tumempokea majeruhi Bathlomeo Nzigilwa mlinzi wa Kanisa ambaye ni mkazi wa kwa Semtema akiwa na hali mbaya, na bado hajapata ufahamu, ila anaendelea na matibabu,” alisema Tung’ombe.

Thursday, November 15, 2012

Semina ya Neno la Mungu katika Kanisa la New Vine International Ministries.

 KANISA la New Vine International Ministries lililopo maeneo ya Nyegezi Jijini Mwanza Chini ya Mpakwa Mafuta wa Bwana Pastor Goodluck Kyara, wanakuletea Semina kubwa ya Neno la Mungu iliyopewa Jina la "Siku 8 za Ushindi na Mafanikio".

Somo kuu katika Semina hiyo linatoka katika Kitabu cha Warumi 8:29-30 likiwa na Kichwa kinachosema "Umezaliwa Kushinda".

Semina hiyo itaanza rasmi Novemba 18 mpaka Novemba 25, kuanzia Saa 9:00 Jioni - Saa 12:00 Jioni. Ukumbi ni pale pale Kanisani maeneo ya Nyegezi karibu kabisa na Sheli ya Mafuta ndani ya Tema Hotel.

Watumishi wa Mungu mbalimbali kutoka ndani na Nje ya Tanzania watahudumu. Baadhi yao ni Mchungaji Kiongozi wa New Vine International Ministries Pastor Goodluck Kyara, Apostle Prince Mulangila(South Africa) na Apostle Paul Njoroge kutoka Nchini Kenya.

Kwa Maelezo zaidi, Piga Simu Namba;
+255 754 435 951

Watu wote mnakaribishwa!

Monday, November 12, 2012

Kilichofanyika Jana katika Tafes Jointmass Mkoa wa Mwanza, ndani ya Bugando University.

BAADA ya kutoka Chuo cha Ualimu Butimba(Butimba TTC) wiki chache zilizopita, Jana shughuli nzima ya Jointmass ilihamia Chuo Kikuu cha Bugando ambapo Wanafunzi toka Matawi yote ya Tafes Mwanza walikutana pale.
With his Presence
Vikundi mbalimbali vya Uimbaji vya Praise and Worship vilihudumu, pamoja na waimbaji binafsi pia walipata nafasi ya kuhudumu.
Sema na Moyo wako.................... (Ruth Lyanga)
Moja ya Vitu vilivyopewa nafasi kwa Siku ya Jana, ni "TAFES AWARENESS", Mada iliyowakilishwa na Tafes Staff(Former Reginal Coordinator) Dada Upendo Mwangoka. Kati ya Mengi aliyoyazungumza, pia alieleza historia ya Tafes na Kazi zake pia.
Dada Upendo Mwangoka
Kwa Upande wa Chakula cha Kiroho, Neno lilifundishwa na Mwl. Gilbert Ezekiel likiwa na Kichwa cha Somo kisemacho; "Nguvu iliyoko katika Ufahamu" na tukapitia Mistari ifuatayo; Yoh 8:31-32, Yoh 1:11, Mithali 8:9 na Waefeso 3:20.
Mwl. Gilbert Ezekiel
Wanafunzi wakifuatilia somo kwa Makini
Kusifu na Kuabudu pia kulipewa nafasi ya kutosha sana ili kushusha Uwepo wa Mungu mahali pale.
Tafes Praise Team
 Upande wa pili mambo yakawa hivi.........
Pipooooooooooooooo................!!!
Mpaka chini, Mpaka chini..................!(Ester Denisy)
Sephone Sospeter(Kwenye Keyboard) na Mutu ya watu Felix Mshama(Kwenye Guitar)
 Maombi pia yalikuwepo wa watu mbalimbali waliokuwa na Uhitaji.
Baadhi ya watu waliofanyiwa Maombi
Mungu na akupe Neema ya kutambua Nguvu iliyoko katika Ufahamu.

Sunday, November 11, 2012

Askofu Anglikana ataka wacheza kamari watoe Sadaka.

Askofu Justin Welby

ASKOFU Justin Welby, aliyeteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana, yaani Askofu wa Canterbury, amependekeza kwenye mtandao wa Twitter kwamba mtu yeyote aliyeshinda kwenye kamari kwa kubahatisha kuwa yeye ndiye atateuliwa, anafaa kutoa fedha hizo kama sadaka kwa kanisa.

Mwanzo wa juma hili makampuni ya kamari yalitangaza kuwa yamesimamisha kamari juu ya nani atakuwa kiongozi mpya wa kanisa la Anglikana, kwa sababu wengi walifikiri kuwa ni Askofu Welby, ambayo inaonesha baadhi ya maafisa wakijua kuwa jina hilo ndilo lilopendekezwa.

Askofu Welby atachukua nafasi ya Rowan Williams mwaka ujao kuwa kiongozi wa wamumini wa Kianglikana dunia nzima.

- BBC Swahili -